Charles Kitwanga: Inanichekesha kuona kivuko chetu kinapelekwa Kenya kutengenezwa

Charles Kitwanga: Inanichekesha kuona kivuko chetu kinapelekwa Kenya kutengenezwa

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Zamani wa Tanzania, Charles Kitwanga amesema “Tunachukua kivuko chetu, sijali kama ilinunuliwa kwa Bilioni 8 na inaendwa kutengenezwa kwa bilioni 7.5, tunashindwaje kuitengeneza sisi Watanzania hadi kupeleka Kenya.

“Tuangalie nani yupo nyuma wa huo mpango, inanipa usumbufu wa mawazo. Sikubaliani na suala la kuipeleka Kenya, niwaambieni hata mkitaka kuiba ibeni kisha muwekeze Tanzania ili wapate kazi”


Chanzo: Dar24
 
Mafundi wa TEMESA na wakandarasi waliopo nchini hawana akili ya kufanya maintenance ya hicho kivuko cha kizamani? nakubaliana na Kitwanga kwenye hili.....
Sasa wa kazi gani na wanalipwa..je wameshindwa kufanya collaboration na baadhi ya wataalam badala ya kupeleka kivuko chote nje?

Zamani hatukujua kama meli inaweza kujengwa hata tanzania. Ila awamu ya tano tumeona maajabu mengi mno. Yote yanawezekana kumbe tanzania ila ni utashi wa aliyepo juu tu.
 
Wanalaumu TEMESA bure ingekuwa wewe ungefanyaje. Umetengewa budget ya tsh 20 billion kwa sababu ya matengenezo na hela ipo kwenye account.

Bunge la budget linakaribia hela uliyopewa mwaka jana bado kiasi kirefu kipo kwenye account. Usipotumia budget inayofuata unaweza punguziwa kwa sababu inaonekana bado kuna mshiko mzuri tu kwenye account yako katika hela uliopewa mwaka uliopita.

Kwa kweli taasisi nyingi za serikali na local government duniani kote ikifika karibu na kipindi cha budget watu huwa wanatafuta matumizi ya ovyo ili hiyo hela isirudi serikali kuu au budget yao ipunguzwe kwa sababu ya kuwa na reserve.

Nchi zilioendelea ikifika mwezi wa pili na watatu utajuta ni road works zisizo na ulazima kila kona, pavement kubomolewa na kujengwa upya, shule kupakwa rangi yaani tafrani katika harakati za halmashauri kumaliza hela zilizopo kwenye account kabla ya mwezi nne, baada ya hapo kama kuna hela zimebaki katika makusanyo yako unapeleka serikali kuu.

Serikali yenyewe imetengeneza hayo mazingira, sasa kama naweza pata percentage ya hayo malipo kwanini nijali kazi nampa nani; hapo ni mwendo wa kuitoa tu hiyo hela iliyotengewa kabla ya budget nyingine.
 
Sasa wa kazi gani na wanalipwa..je wameshindwa kufanya collaboration na baadhi ya wataalam badala ya kupeleka kivuko chote nje?

Zamani hatukujua kama meli inaweza kujengwa hata tanzania. Ila awamu ya tano tumeona maajabu mengi mno. Yote yanawezekana kumbe tanzania ila ni utashi wa aliyepo juu tu.

Sasa kama wanaweza kutengeneza meli, kivuko ndio kiwashinde?
Uwizi mwingine unatia aibu walahi[emoji35]
 
Back
Top Bottom