Charles Kitwanga: Inanichekesha kuona kivuko chetu kinapelekwa Kenya kutengenezwa

Charles Kitwanga: Inanichekesha kuona kivuko chetu kinapelekwa Kenya kutengenezwa

Ngoma ngumu kwa ma Bushi Stars, majembe yetu mengi kama Musukuma, Bajaji, walihama timu pale team captain Pombe alipofariki. Bungeni kabaki Mpina na Bashiru ndio wanapambana na Madenge wa Nishati na Lodi Lofa wa Msoga. Juzi juzi naona kiungo Kitwanga karudi kambini kwa Ma Bushi Stars. Lakini bado.

Noma sana…

Hao ni sub usiogope…muda wowote wanaingia uwanjani
 
Inawezekana spana zinazofungua bolt haziwezi kufika tz
Maajabu hayaishi Tanzania
 
Mafundi wa TEMESA na wakandarasi waliopo nchini hawana akili ya kufanya maintenance ya hicho kivuko cha kizamani? nakubaliana na Kitwanga kwenye hili.....
Wanalaumu TEMESA bure ingekuwa wewe ungefanyaje. Umetengewa budget ya tsh 20 billion kwa sababu ya matengenezo na hela ipo kwenye account.

Bunge la budget linakaribia hela uliyopewa mwaka jana bado kiasi kirefu kipo kwenye account. Usipotumia budget inayofuata unaweza punguziwa kwa sababu inaonekana bado kuna mshiko mzuri tu kwenye account yako katika hela uliopewa mwaka uliopita.

Kwa kweli taasisi nyingi za serikali na local government duniani kote ikifika karibu na kipindi cha budget watu huwa wanatafuta matumizi ya ovyo ili hiyo hela isirudi serikali kuu au budget yao ipunguzwe kwa sababu ya kuwa na reserve.

Nchi zilioendelea ikifika mwezi wa pili na watatu utajuta ni road works zisizo na ulazima kila kona, pavement kubomolewa na kujengwa upya, shule kupakwa rangi yaani tafrani katika harakati za halmashauri kumaliza hela zilizopo kwenye account kabla ya mwezi nne, baada ya hapo kama kuna hela zimebaki katika makusanyo yako unapeleka serikali kuu.

Serikali yenyewe imetengeneza hayo mazingira, sasa kama naweza pata percentage ya hayo malipo kwanini nijali kazi nampa nani; hapo ni mwendo wa kuitoa tu hiyo hela
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Zamani wa Tanzania, Charles Kitwanga amesema “Tunachukua kivuko chetu, sijali kama ilinunuliwa kwa Bilioni 8 na inaendwa kutengenezwa kwa bilioni 7.5, tunashindwaje kuitengeneza sisi Watanzania hadi kupeleka Kenya.

“Tuangalie nani yupo nyuma wa huo mpango, inanipa usumbufu wa mawazo. Sikubaliani na suala la kuipeleka Kenya, niwaambieni hata mkitaka kuiba ibeni kisha muwekeze Tanzania ili wapate kazi”

Chanzo: Dar24
Hakuna sababu ya kulalamika, midomo yetu imejaa laana, iko sababu ya kufaidi matunda ya midomo yetu. Kazi ya kuongoza watu ni ngumu. Mtu akijitolea kuwabana watu katika mambo kama haya tunapaswq kumpongeza na kumtia moyo badala ya kumwongezea stress. Tunafundishwa kujua namna ya kuwaenzi wanaofanya kazi kwa niaba yetu
 
Sasa kama Rais anaruhusu mambo kama hayo kwanini wasipeleke.

Tusijidanganye bwana Watanzania hatuwezi lolote zaidi ya kula kuoana na kupiga umbea.
 
Back
Top Bottom