Wanalaumu TEMESA bure ingekuwa wewe ungefanyaje. Umetengewa budget ya tsh 20 billion kwa sababu ya matengenezo na hela ipo kwenye account.
Bunge la budget linakaribia hela uliyopewa mwaka jana bado kiasi kirefu kipo kwenye account. Usipotumia budget inayofuata unaweza punguziwa kwa sababu inaonekana bado kuna mshiko mzuri tu kwenye account yako katika hela uliopewa mwaka uliopita.
Kwa kweli taasisi nyingi za serikali na local government duniani kote ikifika karibu na kipindi cha budget watu huwa wanatafuta matumizi ya ovyo ili hiyo hela isirudi serikali kuu au budget yao ipunguzwe kwa sababu ya kuwa na reserve.
Nchi zilioendelea ikifika mwezi wa pili na watatu utajuta ni road works zisizo na ulazima kila kona, pavement kubomolewa na kujengwa upya, shule kupakwa rangi yaani tafrani katika harakati za halmashauri kumaliza hela zilizopo kwenye account kabla ya mwezi nne, baada ya hapo kama kuna hela zimebaki katika makusanyo yako unapeleka serikali kuu.
Serikali yenyewe imetengeneza hayo mazingira, sasa kama naweza pata percentage ya hayo malipo kwanini nijali kazi nampa nani; hapo ni mwendo wa kuitoa tu hiyo hela iliyotengewa kabla ya budget nyingine.