Chasambi akataa milioni sita Yanga, asaini Msimbazi kwa milioni 2

Chasambi akataa milioni sita Yanga, asaini Msimbazi kwa milioni 2

Uamuzi wowote saa nyingine hauwezi kuwa sahihi Kwa kila mtu. Hata mapenzi Kwa timu Fulani nayo siyo ya kuyapuuza pia. Hata ulaya ambako ndo reference yetu Kuna wakati mchezaji anakuwa tayari hata mshahara upungue Ili mradi tu akacheze timu anayoitaka Kwa sababu zake mwenyewe.
Umemaliza mkuu.... inawezekana hata Simba au Yanga zote sio sahihi labda sehemu sahihi ilikuwa Azam vipi hapo????.....Ni suala la kumpa muda na sio kukariri kila mchezaji fulani wa nchini akienda Simba au Yanga atafeli hapana

Hata kina samatta au msuva....Ni wazawa na wamepita hizi hizi Simba na Yanga lkn wametoboa labda Ni zamu ya CHASAMBI naye Nani aijuaye kesho yake???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nimemuangalia akicheza dhidi ya Yanga na nimejiridhisha kuwa ni mchezaji wa kawaida sana. ni wale wale dizaini ya Sopu
 
Hii ni propaganda tu. Mwandishi anatakuuamisha umma kuwa;
1. Kilabu ya simba sc inahitaji wachezaji hata huyo eti akija anauhakika kuwa na nafasi ya kucheza ila kule yanga hatopata nafsi, Kutokana na ubora wa kikosi
2. Simba sc haina fedha: inalipa wachezaji mshahara Mdogo mfano huyo mchezaji mshahara ml 2. kule yanga kuna hela,mshahara ml 6.
3.Simba sc ni mbovu kiasi cha kuhitaji wachezaji sita kwenye usajili dirisha dogo.
 
Daah yaan hapo Million 6x36 ana million 216 huku ana Million 72 akicheza simba amepata hasara ya 144 Million sasa si acheze tu Yanga hata wakimtema hayo marundo atajua cha kufanya.

Sasa simba akicheza na wakamtema si inakua imekula kwake. Vipaji ulaya bhana Bongo nyoso
 
Milioni 6 hakulipwa Feisal angepewa Chasambi? Usiamini kila linalozagaa mitandaoni
 
Kama ndio huyo nmemuona mechi ya leo bado sana
 
Kama kibu d ameweza pamoja na makelele yote yale ya awali na yeye ataweza.
 
Mbona kama ni chai hivi, yanga watoe milioni 6 mchezaji ndio kwanza anatoka mtibwa..

Ila angeenda huko huko utopoloni akawa anakunja m 6 kwa mwezi, huku akipambana kupenya kikosi cha kwanza,
Hata simba nafasi ni finyu kuna wachezaji kibao wanasugua.
Angetoa sababu za kimichezo, mfano labda simba wamemuonesha anavyohitajika, labda kocha ndio kamtaka kampa plans zake, kamuhakikishia namba na vile atakavyotumika. La sivyo hata simba akifanya ujinga atasugua.
Hii ya Yanga kumpa 6m hata mimi sikubaliani nayo.
 
Amefanya jambo zuri tu. Pale simba wachezaji wengi ni vibabu. Kwa hiyo ni rahisi kwake kufikiriwa. Yanga ilipofikia kwa sasa, inahitaji mchezaji mwenye kipaji kikubwa zaidi ya hicho cha kwake.
Heri angekunja hiyo 6m kuliko kwenda kukunja hiyo 2m while hajajua Simba itakwenda kumsajili nani wa kuchuana nae ktk hiyo namba.
 
Hii ni propaganda tu. Mwandishi anatakuuamisha umma kuwa;
1. Kilabu ya simba sc inahitaji wachezaji hata huyo eti akija anauhakika kuwa na nafasi ya kucheza ila kule yanga hatopata nafsi, Kutokana na ubora wa kikosi
2. Simba sc haina fedha: inalipa wachezaji mshahara Mdogo mfano huyo mchezaji mshahara ml 2. kule yanga kuna hela,mshahara ml 6.
3.Simba sc ni mbovu kiasi cha kuhitaji wachezaji sita kwenye usajili dirisha dogo.
Twende na point ya tatu Simba hii ni Bora!?? Inahitaji maboresho au hayahitajiki!?? Kwa Maoni yako wachezaji wangapi wanahitajika na ni WA sehemu gani!?? Walisajiliwa 11 msimu uliopita na Hawachezi wote hata mechi za kawaida kabisaaaa Hawachezi ....
 
Back
Top Bottom