CHASO chuo kikuu cha Jordan yapata viongozi wapya

Sango Ochwera

Member
Joined
Mar 20, 2013
Posts
98
Reaction score
26
Jumuiya ya Wanafunzi wanachama wa CHADEMA Chuo Kikuu Kishirika cha Jordan (CHASO) Morogoro imepata viongozi wapya katika uchaguzi uliofanyika leo katika Hotel ya The MARBLE INN mjini Morogoro.

Uchaguzi huo umehudhuriwa na idadi kubwa ya wanachama wa CHASO ambao ni wanafunzi wa chuo hicho.Katika uchaguzi huo, Abel William Mkangwa amechaguliwa kuwa Mwenyekiti,Michael Mkushi(Katibu),Nelius Kubuhwa(Katibu mwenezi) huku Juma Kelvin Ngombo akichaguliwa kuwa Mweka hazina wa Tawi.

Akizungumza mara baada ya uchaguzi huo,Mwenyekiti wa CHASO Mkoa wa Morogoro Kamanda Godson Kagose aliwataka viongozi hao wapya kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu mkubwa na kufuata katiba ya chama na kuhakikisha kuwa wanafuta harufu ya CCM chuoni hapo.

Kagose alitumia fursa hiyo kuwataka wanachama hao kupuuza mchezo wa kuigiza wa video fake ya Lwakatare unaochezwa na maadui wa Demokrasia kuihujumu CHADEMA.Kagose alisema kuwa hiyo ndiyo kete ya mwisho ya mashambulizi ya CCM dhidi ya CHADEMA ambayo hata hivyo nayo imeshashindwa.
 
Tuko pamoja kamanda!Kwa majembe tuliochagua leo Abood anatuhara!
 
Ieleweke kuwa tangu kufunguliwa kwa chuo hiki hapa morogoro mwaka 2010 chuo hiki kimekuwa mwiba mkali kwa ccm.Uwepo wa Chuo Kikuu Cha Mt. Agustino Tanzania na matawi yake nchini ni mpango wa makusudi wa Mwenyezi kuwakomboa Watanzania.
 
Safi sana makamanda....hakuna kulala mpaka kieleweka.
Pia msikisahau chuo cha sayansi ya tiba cha kule ifakara-- sfuchas, ni vema nao mkawafikia!
 
Safi sana Makamanda,imarisheni zaidi eneo hili maana elimu zaidi inahitajika kwa wakaazi wa eneo hili.
 
Jumuiya ya Wanafunzi wanachama wa CHADEMA Chuo Kikuu Kishirika cha Jordan (CHASO) Morogoro imepata viongozi wapya katika uchaguzi uliofanyika leo katika Hotel ya The MARBLE INN mjini Morogoro.

Uchaguzi huo umehudhuriwa na idadi kubwa ya wanachama wa CHASO ambao ni wanafunzi wa chuo hicho.Katika uchaguzi huo, Abel William Mkangwa amechaguliwa kuwa Mwenyekiti,Michael Mkushi(Katibu),Nelius Kubuhwa(Katibu mwenezi) huku Juma Kelvin Ngombo akichaguliwa kuwa Mweka hazina wa Tawi.

Akizungumza mara baada ya uchaguzi huo,Mwenyekiti wa CHASO Mkoa wa Morogoro Kamanda Godson Kagose aliwataka viongozi hao wapya kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu mkubwa na kufuata katiba ya chama na kuhakikisha kuwa wanafuta harufu ya CCM chuoni hapo.

Kagose alitumia fursa hiyo kuwataka wanachama hao kupuuza mchezo wa kuigiza wa video fake ya Lwakatare unaochezwa na maadui wa Demokrasia kuihujumu CHADEMA.Kagose alisema kuwa hiyo ndiyo kete ya mwisho ya mashambulizi ya CCM dhidi ya CHADEMA ambayo hata hivyo nayo imeshashindwa.

Mkiambiwa CDM mnaudin mnalalama!! Kati ya wagombea hakukuwepo muislam kweli????
 
Back
Top Bottom