Sango Ochwera
Member
- Mar 20, 2013
- 98
- 26
Jumuiya ya Wanafunzi wanachama wa CHADEMA Chuo Kikuu Kishirika cha Jordan (CHASO) Morogoro imepata viongozi wapya katika uchaguzi uliofanyika leo katika Hotel ya The MARBLE INN mjini Morogoro.
Uchaguzi huo umehudhuriwa na idadi kubwa ya wanachama wa CHASO ambao ni wanafunzi wa chuo hicho.Katika uchaguzi huo, Abel William Mkangwa amechaguliwa kuwa Mwenyekiti,Michael Mkushi(Katibu),Nelius Kubuhwa(Katibu mwenezi) huku Juma Kelvin Ngombo akichaguliwa kuwa Mweka hazina wa Tawi.
Akizungumza mara baada ya uchaguzi huo,Mwenyekiti wa CHASO Mkoa wa Morogoro Kamanda Godson Kagose aliwataka viongozi hao wapya kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu mkubwa na kufuata katiba ya chama na kuhakikisha kuwa wanafuta harufu ya CCM chuoni hapo.
Kagose alitumia fursa hiyo kuwataka wanachama hao kupuuza mchezo wa kuigiza wa video fake ya Lwakatare unaochezwa na maadui wa Demokrasia kuihujumu CHADEMA.Kagose alisema kuwa hiyo ndiyo kete ya mwisho ya mashambulizi ya CCM dhidi ya CHADEMA ambayo hata hivyo nayo imeshashindwa.