Chata la Tai mwenye taji kwenye malori na Siri iliyojificha

Chata la Tai mwenye taji kwenye malori na Siri iliyojificha

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Kwema Wakuu!

Kuanzia mwaka Juzi 2023 mwezi December, na mwaka Jana kukachanganya kuna ongezeko kubwa la Magari hasa malori ya Mafuta yakiwa na chata la Tai aliyevishwa Taji kichwani.

Kama utakuwa mdadisi unaweza kugundua Jambo hilo kwamba Kati ya malori matatu basi Lori Moja litakuwa na chata la Tai mwenye taji kichwani.

Sitaki kuwakosea Wakubwa kwa kusema mambo haya.
Acha niwaachie wakina Mshana Jr DR Mambo Jambo
Bujibuji Simba Nyamaume
Na wengineo wenye utaalamu na mambo ya Code, Siri, ishara na michoro.
Tunaomba ufafanuzi kwa Sababu najua lazima mtakuwa mmeliona Jambo hilo.
Je hiyo inamaanisha nini?
Kwa nini Jambo hilo limepata nguvu hasa mwaka Jana 2024 na Nina uhakika mwaka 2025 kila baada ya Lori Moja litakuwa na chata la Tai mwenye taji kichwani.

Nini maana yake. Je inaathari yoyote kwenye jamii?

Nawaachia Maiki
Karibuni

Mtibeli
 
Hood Ltd ndio muanzilishi wa hiyo chata kwenye basi zake. Kuna kampuni zina fleet ya tanker za mafuta hawajachora hiyo chata wanaweka logo ya kampuni yao, hiyo ni imani ya mtu. Huwezi kuta kampuni za Ma Singa Singa wakichora hizo wao wanaweka ishara zao

Tai wa hood ni tai ndege asiye na mambo mengi Mkuu.


Tai wa kwenye malori hasa kwenye kichwa amevalishwa Taji lenye msalaba(au Alama ya jumlisha) alafu mengine ni Yale matai yenye sura za kishetani haswa
 
Tai wa hood ni tai ndege asiye na mambo mengi Mkuu.


Tai wa kwenye malori hasa kwenye kichwa amevalishwa Taji lenye msalaba(au Alama ya jumlisha) alafu mengine ni Yale matai yenye sura za kishetani haswa
Basi hizo gari za kampuni 1, ionyeshe hiyo alama. Kampuni za wahindu na masinga Singa ndio wanatumia sana michoro hiyo. Kuna kampuni kubwa huwezi kukuta hata dereva anaruhusiwa kubandika sticker zake za Lumumba kama Fuso za Machungwa na Nyanya
 
Back
Top Bottom