Chata la Tai mwenye taji kwenye malori na Siri iliyojificha

Chata la Tai mwenye taji kwenye malori na Siri iliyojificha

1001302013.png
1001302013.png

Hii ni company Logo ya Scania huwa wanaweka pale mbele na ubavuni gari za miaka ya karibuni huwa wanaichora kwenye cabin ya truck. Wa Sweden wanachora Simba nusu na Eagle kwa juu kuonyesha nguvu na ukali wa hao wanyama kama ishara ya ubora wa gari zao.

Man Diesel zenyewe Logo yake ni Mnyama simba akiwa anatembea
 
View attachment 3216795View attachment 3216795
Hii ni company Logo ya Scania huwa wanaweka pale mbele na ubavuni gari za miaka ya karibuni huwa wanaichora kwenye cabin ya truck. Wa Sweden wanachora Simba nusu na Eagle kwa juu kuonyesha nguvu na ukali wa hao wanyama kama ishara ya ubora wa gari zao.

Man Diesel zenyewe Logo yake ni Mnyama simba akiwa anatembea

Sawasawa

Sasa vipi Yale ambayo sio kampuni Scania lakini wameweka hiyo sticker ambayo sio official
 
Kwema Wakuu!

Kuanzia mwaka Juzi 2023 mwezi December, na mwaka Jana kukachanganya kuna ongezeko kubwa la Magari hasa malori ya Mafuta yakiwa na chata la Tai aliyevishwa Taji kichwani.

Kama utakuwa mdadisi unaweza kugundua Jambo hilo kwamba Kati ya malori matatu basi Lori Moja litakuwa na chata la Tai mwenye taji kichwani.

Sitaki kuwakosea Wakubwa kwa kusema mambo haya.
Acha niwaachie wakina Mshana Jr DR Mambo Jambo
Bujibuji Simba Nyamaume
Na wengineo wenye utaalamu na mambo ya Code, Siri, ishara na michoro.
Tunaomba ufafanuzi kwa Sababu najua lazima mtakuwa mmeliona Jambo hilo.
Je hiyo inamaanisha nini?
Kwa nini Jambo hilo limepata nguvu hasa mwaka Jana 2024 na Nina uhakika mwaka 2025 kila baada ya Lori Moja litakuwa na chata la Tai mwenye taji kichwani.

Nini maana yake. Je inaathari yoyote kwenye jamii?

Nawaachia Maiki
Karibuni

Mtibeli

Alama ya Tai & Maana ya Kiroho ya Kuona Tai
Tai anawakilisha uhuru, uaminifu, ukweli na Uungu. Na kujifunza juu ya ishara ya tai kunaweza kuunda dhamana thabiti kwa mwongozo wako wa roho.
Nitaendelea
 
Tai wa hood ni tai ndege asiye na mambo mengi Mkuu.


Tai wa kwenye malori hasa kwenye kichwa amevalishwa Taji lenye msalaba(au Alama ya jumlisha) alafu mengine ni Yale matai yenye sura za kishetani haswa
Hivi bwana Robert sura ya kishetani umeijuaje kwamfano🤣
 
Tunachukua notes Mkuu
Kwa sababu Tai ni mmoja wa ndege warukao juu zaidi, Anachukuliwa kuwa Mkuu wa viumbe vyote vinavyoruka; hakika hii pia inamuunganisha tai na kipengele cha Hewa. Pia anatawala juu ya robo ya Mashariki ya uumbaji, ambayo inawakilisha upya na msimu wa kiangazi (kiroho nyakati za neema)

Mojawapo ya mafundisho ninayopenda zaidi ya tai ni "amini katika uwezo wako wa kuhimili njaa" .(changamoto) Maana yake, Tai ni hodari sana katika kuwinda na hutumia wakati mchache sana kufanya hivyo. anatumia kiasi kidogo tu cha juhudi kutafuta na kupata kile ambacho "hujaza nafasi hutamani..

Ikiwa una ndoto, ikiwa unataka kufikia lengo ambalo litafanya nafsi yako kujisikia "imejaa" zaidi, chukua mfano kutoka kwa Tai anayejiamini na "ujue" lengo lako litakuwa sawa na la kweli.

Wamisri walimwona Tai kama ishara ya Roho Mkuu na jua wakati wa mchana. Walimwona Tai akiinuka juu ya vizuizi vya kawaida katika uwanja wa ufahamu wa fumbo na maendeleo ya kiroho. Wenyeji wa Amerika wanakubaliana na tathmini hii.

Kwa Warumi na Wagiriki wa kale, Tai alikuwa mtakatifu kwa Jupiter/Zeus. Warumi walitumia Tai kuwakilisha watawala wa Kirumi, wakati Wagiriki walisema Zeus angeweza kuchukua umbo la Tai kumsafirisha mpenzi wake hadi Mlima Olympus. Wahiti walitumia picha ya Tai mwenye vichwa viwili katika vita ili kuwalinda dhidi ya maadui

Kutoka juu juu, Tai anaashiria ufahamu wa mafumbo hayo ambayo wanadamu huona kuwa vigumu kufahamu. Sehemu ya Tai inamruhusu kugundua mifumo inayotuongoza kuelekea kwenye utambuzi mkubwa zaidi
 
Back
Top Bottom