ChatGPT imetimiza unabii uliotolewa takriban miaka 2500 iliyopita!!

ChatGPT imetimiza unabii uliotolewa takriban miaka 2500 iliyopita!!

Safi. Sasa eleza mstari huo Watakatifu waliopo duniani... una maana gani kwako unayesema hakuna mtakatifu duniani
Unamaanisha Mungu anafurahishwa na watenda mema walioko humu dunian. Usisahau hata biblia inasema Roho Mtakatifu anatusaidia kuomba kusikoweza kutamkika it means hata kuomba hatujui achilia mbali huo utakatifu. Bila Roho wa Mungu sisi hatuwez chochote kwa taarifa yako.
 
Kutenda mema na utakatifu ni vitu viwili tofauti. Hata wasiomcha Mungu kabisa wanaweza kutenda mema. Kumbuka habari ya yule kadhi dhalimu. Luka 18:4-5 "...Ijapokuwa simchi Mungu wala sijali watu, lakini, kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake, asije akanichosha kwa kunijia daima."
 
Hata haya maandiko yanatuambia hakuna mkamilifu sote tuna dhambi tumepungukiwa utukufu wa Mungu.
Andiko hilo "Hakuna mwenye haki hata mmoja, hakuna mkamilifu, wote wameoza," lipo katika Warumi 3:10-12,

"Kama ilivyoandikwa: Hakuna mwenye haki, hakuna hata mmoja. Hakuna afahamuye, hakuna amtafutaye Mungu. Wote wamepotoka, wameoza wote pia; hakuna mtendaye mema, la! Hata mmoja."

Andiko hilo halimaanishi kwamba watu hawaokolewi. Badala yake, linasisitiza kwamba hakuna mwanadamu awezaye kuwa mwenye haki au mkamilifu mbele za Mungu kwa matendo yake mwenyewe. Linaonyesha asili ya dhambi ya mwanadamu na hitaji la wokovu wa Mungu kupitia Yesu Kristo.

Paulo anaposema "Wote wamefanya dhambi "– ananukuu Agano la Kale (Zaburi 14:1-3) kuonyesha kuwa Wayahudi na Mataifa wote ni wenye dhambi. Hakuna mwenye haki kwa nguvu zake mwenyewe – Wanadamu hawawezi kupata haki kwa juhudi zao binafsi. Wokovu unapatika kwa imani kwa njia ya Yesu Kristo.

Warumi 3:21-24
Lakini sasa, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria; inashuhudiwa na Torati na Manabii; ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio.... Ukitubu dhambi na kumwamini Yesu unahesabiwa haki. Unahesabiwa mtakatifu.

Paulo anaposema katika mstari wa 23 kwamba "wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu" haishii hapo. Katika mstari wa 24 anaendelea kusema "wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu"
 
Kutenda mema na utakatifu ni vitu viwili tofauti. Hata wasiomcha Mungu kabisa wanaweza kutenda mema. Kumbuka habari ya yule kadhi dhalimu. Luka 18:4-5 "...Ijapokuwa simchi Mungu wala sijali watu, lakini, kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake, asije akanichosha kwa kunijia daima."
Nakukumbusha hata Musa na Daud walitenda dhambi mzee, hata Suleman. Narudia kukuambia kuwa mtakatifu na kuishi kitakatifu ni vitu viwili tofauti, mifano ipo mingi sana kwenye biblia yako. Yule kijana tajiri aliyetaka kujua afanyejw ili arithi ufalme usisahau alikuwa anaishi maisha yote matakatifu yaliyohitajika nyakati hizo tangu utoton mwake. Lakin alipungukiwa na kimoja tu, uchoyo. Basi. Ndio maana nikakupa mfano wa Paulo yeye mwenyewe anasema hajidhanii kwamb amekwisha kufika ila na yeye anapambana ili atimize yote yaliyoanadikwa. Nyie ndio wale mnaowatajirisha watu wanaojiita manabii mnawasahau hata masikini wasiokuwa na hata mlo mmoja hapo jiran yako. Usisahau Mungu haabudiwi kanisani Mungu anaabudiwa katika roho na kweli. Biashara ya mbinguni ni yako binafsi sio jumuiya. So angalia mwenendo wako na sio andiko linasemaje basi unajihakikishia ushindi.
 
Andiko hilo "Hakuna mwenye haki hata mmoja, hakuna mkamilifu, wote wameoza," lipo katika Warumi 3:10-12,

"Kama ilivyoandikwa: Hakuna mwenye haki, hakuna hata mmoja. Hakuna afahamuye, hakuna amtafutaye Mungu. Wote wamepotoka, wameoza wote pia; hakuna mtendaye mema, la! Hata mmoja."

Andiko hilo halimaanishi kwamba watu hawaokolewi. Badala yake, linasisitiza kwamba hakuna mwanadamu awezaye kuwa mwenye haki au mkamilifu mbele za Mungu kwa matendo yake mwenyewe. Linaonyesha asili ya dhambi ya mwanadamu na hitaji la wokovu wa Mungu kupitia Yesu Kristo.

Paulo anaposema "Wote wamefanya dhambi "– ananukuu Agano la Kale (Zaburi 14:1-3) kuonyesha kuwa Wayahudi na Mataifa wote ni wenye dhambi. Hakuna mwenye haki kwa nguvu zake mwenyewe – Wanadamu hawawezi kupata haki kwa juhudi zao binafsi. Wokovu unapatika kwa imani kwa njia ya Yesu Kristo.

Warumi 3:21-24
Lakini sasa, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria; inashuhudiwa na Torati na Manabii; ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio.... Ukitubu dhambi na kumwamini Yesu unahesabiwa haki. Unahesabiwa mtakatifu.

Paulo anaposema katika mstari wa 23 kwamba "wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu" haishii hapo. Katika mstari wa 24 anaendelea kusema "wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika
Hiv kuabudu ni kufanya nini? Maana tuulizane maswali kwanza kabla ya kuendelea
 
Nakukumbusha hata Musa na Daud walitenda dhambi mzee,
Kuna tofauti ya kutenda dhambi na kuishi katika dhambi. Walitenda dhambi lakini walitubu.
Waebrania 10:26-27 (NEN)
Tukiendelea kutenda dhambi kwa makusudi baada ya kupokea ufahamu wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi. Lakini kinachobaki ni kungoja kwa hofu hukumu ya moto uwakao, utakaowaangamiza adui za Mungu.
 
Ndio maana nikakupa mfano wa Paulo yeye mwenyewe anasema hajidhanii kwamb amekwisha kufika ila
Kusema hajidhanii kuwa amekwisha kufika haimaanishi alikuwa anaishi katika dhambi. Wakati anasema hayo ni kweli alikuwa bado duniani.

Tazama jinsi Paulo anavyokiri kwa uhakika kuwa atapokea taji
3. 2 Timotheo 4:7-8
"Nimevipiga vita vilivyo vizuri, nimeumaliza mwendo, nimeilinda imani. Baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa katika siku ile, wala si mimi tu, bali na wote wanaopenda kuja kwake."
 
Hapo anasema kama wosia kwa yule anaemuandikia lakin mwanzo akiwa na nguvu alipambana kujilindq ndio maana hajidhanii maana kama binadam yeyote unaweza kuanguka dhambini anytime. So ndio maana biblia inatutahadharisha kuwa inatupsa kumuomba Mungu siku zote bila kuchoka maana adui kama simba anazunguka akimtqfuta mtu ili ammeze. Adui hatafuti waovu mzee ni watu wa ufalme. So ukiwa umesimama angalia kulinda sana ulichonacho asije mwovu akakichukua.
 
Kuna tofauti ya kutenda dhambi na kuishi katika dhambi. Walitenda dhambi lakini walitubu.
Waebrania 10:26-27 (NEN)
Tukiendelea kutenda dhambi kwa makusudi baada ya kupokea ufahamu wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi. Lakini kinachobaki ni kungoja kwa hofu hukumu ya moto uwakao, utakaowaangamiza adui za Mungu.
So kumbe unakiri kuna kuanguka sio. Basi hakuna aliye mkamilifu mzee.
 
Hiv kuabudu ni kufanya nini?
Kama hujui kuabudu ni nini, ina maana hata Mungu humwabudu.
Yohana 4:23-24 (NEN)
Lakini saa yaja, tena ipo, ambapo wale waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba anawatafuta watu wanaomwabudu kwa namna hii. Mungu ni Roho, na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
 
Hao wanao gundua na kutengeneza ivi vitu sijui akili zao zinakua zinawaza nn. Maana si kitu cha kawaida
 
Miaka takriban 2500 iliyopita, Mungu alimwambia Nabii Danieli awaambie watu kuwa wakati wa mwisho maarifa yataongezeka. Tunasoma hivyo katika kitabu cha Danieli 12:4: "Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie mhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huku na huko, na maarifa yataongezeka."

Leo, tunaona wazi kutimia kwa unabii huo kupitia maendeleo makubwa ya teknolojia, hasa katika Akili Mnemba. Zamani, maarifa yalihifadhiwa katika vitabu na kupatikana polepole, lakini sasa, kwa sekunde chache tu, mtu anaweza kupata maarifa na taarifa nyingi kwa njia ya mitandao, AI, na mifumo ya kisasa ya kompyuta. Akili Mnemba si tu kwamba inachakata taarifa haraka, bali pia inajifunza, inafikiri, na hata kusaidia kufanya maamuzi magumu. Ni dhahiri, maarifa yameongezeka kama ilivyotabiriwa.

Kuongezeka kwa maarifa ni moja ya dalili za siku za mwisho. Katika Mathayo 24:3-14, Yesu alieleza ishara na dalili nyingine zitakazotokea kabla ya kuja kwake na kabla ya mwisho wa dunia. Dalili na ishara hizo karibu zote zimeishatimia. Huu ni uthibitisho wa wazi kuwa Biblia ni kitabu cha kuaminika. Kwa wanaoamini kitabu hiki, kuongezeka huku kwa maarifa ni maonyo kwamba nyakati tulizo nazo si za kawaida. Huu ni wakati wa kuwa macho, ni wakati wa kujiandaa kiroho, na kusimama imara kwa Mungu, kwa kuwa siku ya kurudi kwa Yesu imekaribia!

Ibilisi anajua wakati uliobaki ni mchache(Ufunuo 12:12), kwa sababu hiyo anafanya kila jitihada kuwashawishi watu wasiamini kuwa Mungu yupo. Anatumia mbinu nyingi kuwashawishi watu wazame katika matendo ya dhambi kama ushoga, uzinzi, ulevi, wizi, uongo nk, ili siku hiyo ikifika waachwe, maana Yesu akirudi atawachukua na kuwapeleka mbinguni wale tu waliotubu dhambi zao na kumwamini Yesu. Watakaoachwa watabaki katika dhiki kuu ambayo haijawahi kuwepo tangu kuumbwa kwa ulimwengu(Mathayo 24:21); na hatimaye siku ya mwisho wote wasioamini watatupwa pamoja na Ibilisi katika moto wa milele(Mathayo 25:41).

Wimbo huu na picha hizi zimetengenezwa kwa msaada wa chatGPT/AI
View attachment 3235549 View attachment 3235550View attachment 3235551View attachment 3235552View attachment 3235553
kweli m2mishi
 
Kama hujui kuabudu ni nini, ina maana hata Mungu humwabudu.
Yohana 4:23-24 (NEN)
Lakini saa yaja, tena ipo, ambapo wale waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba anawatafuta watu wanaomwabudu kwa namna hii. Mungu ni Roho, na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
Nimekuuliza kuabudu ni kufanyaje? Nataka unielezee kile kitendo kinafanyika vip sio maelezo . Ulipata sifur darasan nini mkuu
 
Sasa wewe ulipataje 100 wakati hujui hata kitendo cha kuabudu kinafanyikaje
Ndio nakuuliza wewe kuabudu ni kufanya nini? Mbona unarukaruka kama maharage kwenye sufuria mzee. Kama hujui si useme hujui.
 
Back
Top Bottom