ChatGPT imetimiza unabii uliotolewa takriban miaka 2500 iliyopita!!

Maarifa kwa binadamu hajaanza leo na hayatokoma leo,,,ndo maana nasema kaunabii kaungaunga...
Mkuu, itafika siku yatakoma, kwa sababu kila chenye mwanzo kina mwisho.
Ndo maana nasema mwisho umekaribia kwa sababu dalili mojawapo iliyotabiriwa ni kuongezeka kwa maarifa. Maarifa yameongezeka kwa kasi sana kipindi hiki.
 
Uongezefu wa maarifa uliozungumziwa hapo ni mkubwa kuliko ulivyorelate, akili mnemba ni very basic thing kwenye maarifa halisi ambayo yamemaanishwa.

Na si kwamba ukuaji wa maarifa haujawahi kutokea duniani, umetokea zaidi ya mara moja, rejea pale sodoma na gomola pamoja na pale kwenye mnara wa babel lakini pia hata ukisoma mwanzo wa uumbaji pale wana wa Mungu walipoanza kuona wana wa Adam na kile kizazi kilichozaliwa kutokana na muunganiko huo kulikua ni kizazi chenye balaa sana ambacho kilikua kinamchallenge Mungu hadi yeye mwenyewe alikiri kwamba mwanadamu ako na mawazo mabaya Kila siku.

Kwahiyo ongezeko la maarifa halihesabiwi kama ongezeko kama halileti challenge ya moja kwa moja kwa Mungu, na hii ndio uhesabiwa kama dhambi, kwa maana nyingine ni kwamba dhambi ni kile kitendo cha kuvuka mipaka na kuanza kufanya mambo beyond uwezo wa kawaida wa mwanadamu.

Kwahiyo Dunia iko inaendelea kujitahidi kutransform knowledge kuelekea pazuri ila level uliyoizungumzia wewe bado sana hasa kwa mtu mmoja mmoja.

Na ndio maana utaona hizi AI hazijaja bahati mbaya ila zimekuja kwa kusudi na ndio maana pia utaona hizi AI hazifanyi mambo beyond uwezo wa binadamu isipokua zinatunza kumbukumbu ambazo binadamu wanazo kwahiyo zinafanya Kila kitu ambacho kinafanywa na binadamu na kuishia hapo kwa maana hazifanyi kitu chochote beyond uwezo wa kibinadamu.

Kwahiyo ili tufike huko unakosema hadi pale ambapo watatokea watu wenye uwezo mkubwa na kuanza kuleta vitu venye kufanya mambo makubwa ambayo binadamu Hana uwezo wa kuyafanya na wala Hana uwezo wa kuyacontrol kama ambavyo anauwezo wa kucontrol gari au ndege na meli na hata robots.

Sasa sodoma na gomola kabla haijaangamizwa ilikua na watu wa namna hii, mtu anaweza akakaa zake maabara akatengeneza kiumbe cha ajabu na kikawa na uwezo wa kufanya mambo ya ajabu pasipo kuamuliwa hata na yule ambae amekitengeneza (kizazi chetu hiki cha social media, ukifunua ubongo unakutana na simba, yanga, man u, liver, arsenal, mara muziki na kadhalika, hata ukikipatia miaka mia mbele hakiwezi kufika kwenye hatua unayoisemea wewe).

So kama hiko ndio kigezo chako cha kudefine mwisho wa Dunia basi endelea kufurahia kwa maana bado sana mkuu.

Oops, nataka kusahau tena... Naomba nitajie kanisa unalohudumu ili nijumuike nawe this Sunday... Thanks in advance.
 
Acha uoga. Mwisho wa dunia bado sana. Kulingana na biblia ule mwisho utakuja baada ya kila binadamu kuhubiriwa na kufahamu injili na ujio wa Yesu. Sasa jiulize kuna mamilioni mangapi ya watu wasioifahamu biblia? Wahadzabe wangapi wanajua kuhusu Yesu Kristo. Huko Afghanistan wanajua nini kuhusu injili?
 
Kulingana na biblia ule mwisho utakuja baada ya kila binadamu kuhubiriwa na kufahamu injili na ujio wa Yesu.
Biblia haisemi hivyo ulivyoandika. Biblia yangu inasema:
Mathayo 24:14 (NEN)
"Injili hii ya ufalme itahubiriwa ulimwenguni kote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote. Ndipo mwisho utakapokuja."
Kwa kasi hii ya kuongezeka kwa maarifa unafikiri itachukua miaka 100 Injili kuwafikia watu wote duniani. Sherehe tu za kuapishwa kwa Rais Trump ("Rais wa Dunia") zimefuatiliwa na mamilioni ya watu duniani. Katika sherehe hizo Rais Trump aliombewa na Wachungaji wazi wazi kwa Jina la Yesu. Huo tayari ni ushuhuda kwa watu wa Russia, Afghanistan, China na kote kwingine. Hao Wahadzabe unaowasema tayari wameishafikishiwa Injili na "wamisionari."
Kaa tayari mpendwa, "Kwa kuwa bado kitambo kidogo tu, yeye ajaye atakuja wala hatakawia.”(Waebrania 10:37 NEN)
 
kumwamini sio kuongea tu mdomoni kuna maagizo ya utii
Uko sawa. Tunatakiwa kuamini, kutii n kufuata amri zote za Mungu. Tukifanya hivyo tutabarikiwa pia.
(Kumbukumbu 28:1-19)
 
Mkuu wapi watu wameanza kukimbia huku na huko? Ukiachana na watu wanaokimbia vita na wanaoenda kula bata?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…