Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 1,679
- 2,123
Miaka takriban 2500 iliyopita, Mungu alimwambia Nabii Danieli awaambie watu kuwa wakati wa mwisho maarifa yataongezeka. Tunasoma hivyo katika kitabu cha Danieli 12:4: "Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie mhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huku na huko, na maarifa yataongezeka."
Leo, tunaona wazi kutimia kwa unabii huo kupitia maendeleo makubwa ya teknolojia, hasa katika Akili Mnemba. Zamani, maarifa yalihifadhiwa katika vitabu na kupatikana polepole, lakini sasa, kwa sekunde chache tu, mtu anaweza kupata maarifa na taarifa nyingi kwa njia ya mitandao, AI, na mifumo ya kisasa ya kompyuta. Akili Mnemba si tu kwamba inachakata taarifa haraka, bali pia inajifunza, inafikiri, na hata kusaidia kufanya maamuzi magumu. Ni dhahiri, maarifa yameongezeka kama ilivyotabiriwa.
Kuongezeka kwa maarifa ni moja ya dalili za siku za mwisho. Katika Mathayo 24:3-14, Yesu alieleza ishara na dalili nyingine zitakazotokea kabla ya kuja kwake na kabla ya mwisho wa dunia. Dalili na ishara hizo karibu zote zimeishatimia. Huu ni uthibitisho wa wazi kuwa Biblia ni kitabu cha kuaminika. Kwa wanaoamini kitabu hiki, kuongezeka huku kwa maarifa ni maonyo kwamba nyakati tulizo nazo si za kawaida. Huu ni wakati wa kuwa macho, ni wakati wa kujiandaa kiroho, na kusimama imara kwa Mungu, kwa kuwa siku ya kurudi kwa Yesu imekaribia!
Ibilisi anajua wakati uliobaki ni mchache(Ufunuo 12:12), kwa sababu hiyo anafanya kila jitihada kuwashawishi watu wasiamini kuwa Mungu yupo. Anatumia mbinu nyingi kuwashawishi watu wazame katika matendo ya dhambi kama ushoga, uzinzi, ulevi, wizi, uongo nk, ili siku hiyo ikifika waachwe, maana Yesu akirudi atawachukua na kuwapeleka mbinguni wale tu waliotubu dhambi zao na kumwamini Yesu. Watakaoachwa watabaki katika dhiki kuu ambayo haijawahi kuwepo tangu kuumbwa kwa ulimwengu(Mathayo 24:21); na hatimaye siku ya mwisho wote wasioamini watatupwa pamoja na Ibilisi katika moto wa milele(Mathayo 25:41).
Wimbo huu na picha hizi zimetengenezwa kwa msaada wa chatGPT/AI