Ni vyema tukajiuliza tunajadili suala la Chato kuwa sehemu ya mkoa mpya kwa sababu rais anatokea Chato na kunaonekana kupendelea kwao au tunajadili kwa sababu hakukuwa na haja ya Chato kuwa sehemu ya mkoa mpya.
Kwanini tusiangalie ugumu wanaopitia wakaazi wa hizo wilaya zinazosadikika kumegwa ili kutengeneza mkoa mpya katika kufuatlia mambo yao katika manispaa ambazo wilaya zao zipo kwa sasa, walao tujue kwamba kulikuwa na haja ya mkoa mpya kuanzishwa ama la, tunaweza tukaishia kumtizima Mheshimiwa rais katika jicho lla kibaguzi lakini kumbe anafanya hivyo kwa kuwa anajua hali wanazopitia wananchi wa hayo maeneo hasa ukizingatia amekulia miongoni mwao, je kama kuna tatizo asitatue kwa sababu tu anatokea pale na ataonekana kupendelea kwao.
Naona kuna watu wanasema acha agawe wakijitetea kwa kusema mbona kipindi Sumaye akiwa Waziri Mkuu Arusha iligawanywa, huku ni kukosa maarifa au pengine ni kuamua kutokujua historia ya sehemu husika, hivi Arusha ile kweli kugawanywa unaweza ukasema hapa watu wamekurupuka? tuache ushabiki wakuu tujadili facts.
Vyovyote iwavyo lakini sidhani kama kuna hasara ya kuanzisha mkoa mpya ila najua kuna faida kwa wakaazi wa eneo husika, Ni vyema tuseme kwanini hakukufaa kwa sasa kuanzishwa mkoa mpya na siyo kupakana matope.
Jambo ambalo nashauri ni kwamba vyombo vyetu vya usalama wasiachie tu demokrasia ya vyama viamue nani atagombea kiti cha urais, na badala yake vetting yao itumike pia kutuchagulia mgombea miongoni mwa wanachama wa chama husika mwenye sifa na historia ambazo hazitii shaka, ila mkiichia demokrasia ya vyama pekee inaweza ikatupa mtu anayetufaa na asiyetufaa hasa ukizingatia kwamba demokrasia wakati mwingine siyo demokrasia, inaweza ikampa dikteta nafasi na mbaguzi pia.