Tetesi: Chato kuwa mkoa mpya na jina la mkoa kutangazwa soon na Chato kuwa makao makuu ya mkoa mpya

Tetesi: Chato kuwa mkoa mpya na jina la mkoa kutangazwa soon na Chato kuwa makao makuu ya mkoa mpya

Kuna MAWE na MAJIWE sasa huyu rais sijui yupo upande upi
 
HUWA NAJIULIZA KITU KIMOJA.

NCHI YETU RAIS AKIWA MCHAGA ITAKUWAJE?

Kwa sababu kwa Tanzania, ndyo kabila linaloongoza kwa unyumbani
Pole Nyerere alikosea kupeleka watu wa labour force shule ona tunavyoaibika
 
Chato ilikuwa mkoa wa Kagera,ikamegwa ikapelekwa Mkoa wa Geita na sasa inataka kuwa mkoa.Chato kunani?
 
Duuu hii mbona kali, coz kuna mikoa ambayo ukiangalia kabisa unaona kuna ulazima wa kugawa, mfano ni mkoa wa Morogoro mkubwa sana, lakini Chato uwe mkoa hii kali
 
Iwe mkoa, nchi, region bara, country, continent, kata, ward, tarafa hainihusu! Mie nataka
amani
upendo
ukweli
haki
uhuru wa maoni
kutobambikiza kesi
kutokuwepo upendeleo wa kikanda (ubaguzi) na
kuheshimu mawazo ya wengine.
 
Naungana mkono Mkoa mpya Wa Rubondo

Pia , Morogoro iangaliwe lengo ni kusogeza Huduma jirani

Pia tupunguze wivu , haya mambo si mageni yalianza toka zamani

Tatizo kuna watu wana chuki sana
 
Deal imevuja kama namuona mhutu......bashite pambana na sisi misungwi huwe mkoa
 
Ni vyema tukajiuliza tunajadili suala la Chato kuwa sehemu ya mkoa mpya kwa sababu rais anatokea Chato na kunaonekana kupendelea kwao au tunajadili kwa sababu hakukuwa na haja ya Chato kuwa sehemu ya mkoa mpya.
Kwanini tusiangalie ugumu wanaopitia wakaazi wa hizo wilaya zinazosadikika kumegwa ili kutengeneza mkoa mpya katika kufuatlia mambo yao katika manispaa ambazo wilaya zao zipo kwa sasa, walao tujue kwamba kulikuwa na haja ya mkoa mpya kuanzishwa ama la, tunaweza tukaishia kumtizima Mheshimiwa rais katika jicho lla kibaguzi lakini kumbe anafanya hivyo kwa kuwa anajua hali wanazopitia wananchi wa hayo maeneo hasa ukizingatia amekulia miongoni mwao, je kama kuna tatizo asitatue kwa sababu tu anatokea pale na ataonekana kupendelea kwao.
Naona kuna watu wanasema acha agawe wakijitetea kwa kusema mbona kipindi Sumaye akiwa Waziri Mkuu Arusha iligawanywa, huku ni kukosa maarifa au pengine ni kuamua kutokujua historia ya sehemu husika, hivi Arusha ile kweli kugawanywa unaweza ukasema hapa watu wamekurupuka? tuache ushabiki wakuu tujadili facts.
Vyovyote iwavyo lakini sidhani kama kuna hasara ya kuanzisha mkoa mpya ila najua kuna faida kwa wakaazi wa eneo husika, Ni vyema tuseme kwanini hakukufaa kwa sasa kuanzishwa mkoa mpya na siyo kupakana matope.
Jambo ambalo nashauri ni kwamba vyombo vyetu vya usalama wasiachie tu demokrasia ya vyama viamue nani atagombea kiti cha urais, na badala yake vetting yao itumike pia kutuchagulia mgombea miongoni mwa wanachama wa chama husika mwenye sifa na historia ambazo hazitii shaka, ila mkiichia demokrasia ya vyama pekee inaweza ikatupa mtu anayetufaa na asiyetufaa hasa ukizingatia kwamba demokrasia wakati mwingine siyo demokrasia, inaweza ikampa dikteta nafasi na mbaguzi pia.
 
Hakuna Tatizo Kwa kuwa Hata Sumaye akiwa PM ndio Manyara ikazaliwa kutoka Arusha

Katavi ilizaliwa kutoka Rukwa wakati wa Pinda

Tunategemea Pia Mkoa wa Ruangwa kutokea Lindi

Tulikuwa tunamsakama Jakaya anapendelea kwao Bagamoyo sasa tumepata Mtu anaetufundisha maana ya kupendelea kwao
Hata Njombe ilitokana na yule Katibu Mkuu Kiongozi awamu ya Jakaya.
 
Hata Kinondoni ya zamani, Temeke ya zamani na Ilala ziwe mikoa kamili. Miundombinu mingine tayari ipo kama RPCs. Tuendelee kugharamia siasa na wanasiasa. Hela kugharamia siasa ipo.
 
Hata Njombe ilitokana na yule Katibu Mkuu Kiongozi awamu ya Jakaya.
Wewe unayeongelea Njombe, unafahamu mazingira yaliyokuwepo. Ukumbuke kuwa Njombe ilikuwa ni sehemu ya Iringa. Kutoka Njombe mpaka Iringa ni km 210, zaidi ya kutoka Mwanza mpaka Geita (~100km) na ni zaidi ya kutoka Mwanza mpaka Shinyanga (164km).

Mkoa wa Katavi, kutoka Sumbawanga mpaka Mpanda ni zaidi ya 200km. Lakini kutoka Chato mpaka Geita ni kama 100km tu. Huo ni umbali wa kawaida kwa wilaya nyingi kutoka makao makuu ya wilaya mpaka makao makuu ya mkoa.

Lakini ukumbuke pia kuwa Rais alisema katika kipindi chake hakutakuwa na uongezaji wa wilaya, mikoa au majimbo ya uchaguzi. Ndiyo maana siiamini hii taarifa.
 
Back
Top Bottom