Wewe unayeongelea Njombe, unafahamu mazingira yaliyokuwepo. Ukumbuke kuwa Njombe ilikuwa ni sehemu ya Iringa. Kutoka Njombe mpaka Iringa ni km 210, zaidi ya kutoka Mwanza mpaka Geita (~100km) na ni zaidi ya kutoka Mwanza mpaka Shinyanga (164km).
Mkoa wa Katavi, kutoka Sumbawanga mpaka Mpanda ni zaidi ya 200km. Lakini kutoka Chato mpaka Geita ni kama 100km tu. Huo ni umbali wa kawaida kwa wilaya nyingi kutoka makao makuu ya wilaya mpaka makao makuu ya mkoa.
Lakini ukumbuke pia kuwa Rais alisema katika kipindi chake hakutakuwa na uongezaji wa wilaya, mikoa au majimbo ya uchaguzi. Ndiyo maana siiamini hii taarifa.