Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania ametoa salamu za maadhimisho ya miaka 56 ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibari yanayotarajia kuadhimishwa siku ya kesho tarehe 26/04/ 2020.
Katika salamu hizo Mh. Rais amewataka Watanzania wote kutumia maadhimisho hayo kutafakari Muungano huo ambao uliasisiwa na viongozi wakuu Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pamoja na Hyati Sheikh Abeid Aman Karume pamoja na kumuomba Mungu dhidi ya janga la Corona.
Sambamba na hilo, Katika maadhimisho hayo Rais Magufuli ametoa msamaha kwa jumla ya wafungwa 3973 ambapo kati yao wafungwa 3717 wamesamehewa vifungo vyao wakati wengine 256 waliokuwa wakikabiliwa na adhabu ya kunyongwa wamebadilishiwa adhabu hiyo.
Mwisho, Rais ameendeleza kutoa msisitizo kwa Watanzania wote kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona kwa kuhakiksha kuwa wanaepuka mikusanyiko na safari zisizo za lazima.
Pia, soma:
Sherehe za sikukuu ya miaka 55 ya Muungano zafutwa, TSh 988 mil zitapangiwa kazi nyingine
Rais Samia: Fedha ambazo zingegharamia Sherehe za miaka 57 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, zigawanywe sawa