Chato: Rais Magufuli atoa salamu za maadhimisho ya miaka 56 ya Muungano. Asamehe wafungwa 3,973

Chato: Rais Magufuli atoa salamu za maadhimisho ya miaka 56 ya Muungano. Asamehe wafungwa 3,973

Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania ametoa salamu za maadhimisho ya miaka 56 ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibari yanayotarajia kuadhimishwa siku ya kesho tarehe 26/04/ 2020.

Katika salamu hizo Mh. Rais amewataka Watanzania wote kutumia maadhimisho hayo kutafakari Muungano huo ambao uliasisiwa na viongozi wakuu Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pamoja na Hyati Sheikh Abeid Aman Karume pamoja na kumuomba Mungu dhidi ya janga la Corona.

Sambamba na hilo, Katika maadhimisho hayo Rais Magufuli ametoa msamaha kwa jumla ya wafungwa 3973 ambapo kati yao wafungwa 3717 wamesamehewa vifungo vyao wakati wengine 256 waliokuwa wakikabiliwa na adhabu ya kunyongwa wamebadilishiwa adhabu hiyo.

Mwisho, Rais ameendeleza kutoa msisitizo kwa Watanzania wote kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona kwa kuhakiksha kuwa wanaepuka mikusanyiko na safari zisizo za lazima.
Hongera sana mheshiwa Rahisi,hii itatusaidia sana kupunguza maambukizi ya corana. Imeisha hiyoo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ipo kwenye katiba kwamba ni lazima?

Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu mimi sijui sheria, lakini nachojua kwamba huo utaratibu ni desturi ya ikulu yani hata kama angekuepo rais mwingine angefanya hivo, mnapomsifia kwamba huu ni ukarimu inasound kama ni kitu cha kipekee sana kwamba ni yeye ana uwezo wa kufanya hivi kwamba wenzake hawakufanya haya
ukarimu hata JK alikua mkarimu
 
Historia haipigiwi makofi,tunaongelea jpm and not jkm
mkuu mimi sijui sheria, lakini nachojua kwamba huo utaratibu ni desturi ya ikulu yani hata kama angekuepo rais mwingine angefanya hivo, mnapomsifia kwamba huu ni ukarimu inasound kama ni kitu cha kipekee sana kwamba ni yeye ana uwezo wa kufanya hivi kwamba wenzake hawakufanya haya
ukarimu hata JK alikua mkarimu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sio ukarimu wake, hiyo ni taratibu ipo toka miaka mingi, msisifie sana mpaka naye anakuwa bored

Hao jamaa wa pale makao makuu ya kile chama kwa kujikomba tu kwa wakulu hawajambo

Utamaduni huo ni Afrika nzima kama sio duniani ila yeye anataka watu waone u"special" wa sponsor wake
 
Itapendeza sana mrembo mjane Miriam Msuya ni miongoni waliopata msamaha
 
Hakika huyu Mr ni messiah![emoji23]
RAIS MAGUFULI ATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 3,973

Rais Dkt John Magufuli ametoa msamaha kwa jumla ya wafungwa 3,973 ambapo kati yake wafungwa 3,717 wamesamehewa vifungo vyao na wafungwa 256 waliokuwa wanakabiliwa na adhabu ya kunyongwa hadi kufa wamebadilishiwa adhabu hiyo.

Msamaha huo umetolewa ikiwa kesho Jumapili, April 26 ni maadhimisho ya miaka 56 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

View attachment 1430158

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu mimi sijui sheria, lakini nachojua kwamba huo utaratibu ni desturi ya ikulu yani hata kama angekuepo rais mwingine angefanya hivo, mnapomsifia kwamba huu ni ukarimu inasound kama ni kitu cha kipekee sana kwamba ni yeye ana uwezo wa kufanya hivi kwamba wenzake hawakufanya haya
ukarimu hata JK alikua mkarimu
Tuna wapumbavu wa kusifia - siku moja watakuja kusema, angalieni Rais wetu alivyo mkarimu, ameturuhusu tuvute hata hewa.

Kule Uganda, enzi za utawala wa Kabaka, wakati ule Ukristo unaingia, miongoni mwa wale mashahidi wa Uganda alitamka, " inatupasa kumsikiliza Mungu zaidi kuliko Mwanadamu'. Basi machifu waliokuwepo mbele ya Kabaka kusikia vile, walianguka chini na kumsujudia Kabaka, kisha wakasema, "unaona? Tulikuambia kuwa ufalme wako umekwisha. Siku zote tunajua wewe ni kila kitu. Hata hewa tunayoivuta ni mali yako. Leo hawa wanasema wanamsikiliza mwingine zaidi yako".

Bahati mbaya mijitu mipumba.vu ya namna ile ya machifu waliokuwepo Uganda enzi za Kabaka, mpaka leo bado ipo Afrika.

Tangu tupate uhuru, hakuna Rais ambaye hakuwahi kusamehe wafungwa kila mwaka, lakini leo, wapumb.avu hawa wanataka kutuaminisha kuwa jambo hili limeasisiwa na Awamu ya Tano. Nina imani mijiti ya namna hii, hata Mh. Rais Magufuli atakuwa anakereheshwa nayo. Ni sawa mtu akuambie kuwa, wewe ni mtu maarufu sana, hata mvua hii inanyesha kutokana na mapenzi yako. Nina imani ukilisikia jitu la namna hilo utalifukuza, kwa sababu utajua limejaa unafiki mkubwa.

Rais ametimiza wajibu wake wa kuwasamehe wafungwa kwa mujibu wa sheria kwa kuzingatia vigezo alivyopewa.

Ombi letu ni kuwa anatakiwa kuwaangalia zaidi watu wale waliopo mahabusu kwa uonevu. Tunaomba aijiwe na hekima, na Roho ya Mungu. Awatoe watu walioonewa au kwa maelekezo yake au walionewa na wetendaji wake kwa nia ya kutaka kumfurahisha yeye. Kama upelelezi haujapatikana mwaka mzima, huo ni ishahidi tosha kuwa mtu huyo siyo mhalifu. Aachiwe huru. Kama ushahidi utakuja kupatikana dhidi yake, atakamatwa tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni baada ya tetemeko au?

Mkuu hiyo ni jadi wakati wa kusheherekea sikukuu ya Tanzania (Muungano 1964)

Congratulations to Tanzania on Union Day

Party General Secretary and President Nguyen Phu Trong on April 25 sent a message of congratulations to President of the United Republic of Tanzania John Magufuli on the occasion of the country’s 56th Union Day (April 26, 1964-2020).

Congratulations to Tanzania on Union Day hinh anh 1(Infographic: VNA)

Hanoi (VNA) – Party General Secretary and President Nguyen Phu Trong on April 25 sent a message of congratulations to President of the United Republic of Tanzania John Magufuli on the occasion of the country’s 56th Union Day (April 26, 1964-2020).

His Majesty Sultan sends greetings to Tanzania
Oman

The same day, Deputy Prime Minister and Foreign Minister Pham Binh Minh also congratulated Tanzanian Minister of Foreign Affairs and East African Cooperation Palamagamba Kabudi./.
Muscat: His Majesty Sultan Haitham Bin Tarik has sent a cable of congratulations to Tanzanian President Dr. John Magufuli on his country's National Day.

In his cable, His Majesty the Sultan expressed his sincere greetings and wishes of good health and happiness to the president and his country's people further progress and prosperity.

1587830397823.png
 
Angeanza na wale wa ushahidi haujakamilika wako ndani zaidi ya 5yrs wakisubiria ushahidi wakakamilishe ushahidi kwanza.Waafrika twatendeana mabaya kuliko hata mkoloni aliyomtendea mwafrika yaani easy tu tunacheza na maisha ya wengine eti upelelezi haujakamilika and then ikifika wakati wa ibada tumejaa kwenye nyumba za ibada hii mizigo yote ya nn kuwafurahisha wanadamu nasi tuonekane misikitini au makanisani?
Hao sio wafungwa ni mahabusu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuna wapumbavu wa kusifia - siku moja watakuja kusema, angalieni Rais wetu alivyo mkarimu, ameturuhusu tuvute hata hewa.

Kule Uganda, enzi za utawala wa Kabaka, wakati ule Ukristo unaingia, miongoni mwa wale mashahidi wa Uganda alitamka, " inatupasa kumsikiliza Mungu zaidi kuliko Mwanadamu'. Basi machifu waliokuwepo mbele ya Kabaka kusikia vile, walianguka chini na kumsujudia Kabaka, kisha wakasema, "unaona? Tulikuambia kuwa ufalme wako umekwisha. Siku zote tunajua wewe ni kila kitu. Hata hewa tunayoivuta ni mali yako. Leo hawa wanasema wanamsikiliza mwingine zaidi yako".

Bahati mbaya mijitu mipumba.vu ya namna ile ya machifu waliokuwepo Uganda enzi za Kabaka, mpaka leo bado ipo Afrika.

Tangu tupate uhuru, hakuna Rais ambaye hakuwahi kusamehe wafungwa kila mwaka, lakini leo, wapumb.avu hawa wanataka kutuaminisha kuwa jambo hili limeasisiwa na Awamu ya Tano. Nina imani mijiti ya namna hii, hata Mh. Rais Magufuli atakuwa anakereheshwa nayo. Ni sawa mtu akuambie kuwa, wewe ni mtu maarufu sana, hata mvua hii inanyesha kutokana na mapenzi yako. Nina imani ukilisikia jitu la namna hilo utalifukuza, kwa sababu utajua limejaa unafiki mkubwa.

Rais ametimiza wajibu wake wa kuwasamehe wafungwa kwa mujibu wa sheria kwa kuzingatia vigezo alivyopewa.

Ombi letu ni kuwa anatakiwa kuwaangalia zaidi watu wale waliopo mahabusu kwa uonevu. Tunaomba aijiwe na hekima, na Roho ya Mungu. Awatoe watu walioonewa au kwa maelekezo yake au walionewa na wetendaji wake kwa nia ya kutaka kumfurahisha yeye. Kama upelelezi haujapatikana mwaka mzima, huo ni ishahidi tosha kuwa mtu huyo siyo mhalifu. Aachiwe huru. Kama ushahidi utakuja kupatikana dhidi yake, atakamatwa tena.

Sent using Jamii Forums mobile app

Meseji nzito sana hii mkuu! Barikiwa
 
Wale ni mahabusu Mkuu ,Siyo wafungwa..Labda kama Jiwe apindishe sheria kama kwa Waliotuhumiwa kuhujumu Uchumi.
Nchi ngumu sana hii.
Haitokuwa ajabu kuendelea kupindisha sheria. Kuweko kwao ndani ni kupindisha sheria tayari. Umeona wapi kesi miaka 8 mtu yuko mahabusu na uchunguzi haujakamilia!
 
  • Thanks
Reactions: prs
Back
Top Bottom