Chato wajiapiza 2025/2030 watamchagua Katwale. Kalemani hajaleta mradi wowote tangu Dkt. Magufuli afariki dunia

Chato wajiapiza 2025/2030 watamchagua Katwale. Kalemani hajaleta mradi wowote tangu Dkt. Magufuli afariki dunia

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Wana Chato wamejiapiza kwamba uchaguzi wa ubunge unaokuja, wanakwenda na Katwale.
Wanachato wanasema kwamba Katwale alikuwa chaguo lao lakini JPM alimpandikiza Kalemani.

Gumzo kubwa wilayani Chato ni kwamba miradi yote wanayoiona Chato ni kazi ya JPM. Mbunge wao Kalemani hajafanikisha mradi wowote ule tangu awe mbunge, zaidi ya kujikinga jua kwenye miradi iliyoletwa na JPM.

Tangu JPM afariki, hakuna mradi wowote ulioletwa na mbunge wao, badala yake wanaona mkuu wao wa Wilaya akihangaika huku na kule kuhakikisha Chato haikosi miradi ya maendeleo.

Hivi karibuni Mkuu wa Wilaya amepambana kuhakikisha mradi wa maji wa Buzirayombo unaanza. Mradi huo utasambaza maji sehemu mbalimbali, ikiwemo Bwanga, Katende na Buzirayombo pamoja na Buziku.

Kalemani ni sehemu ya wabunge waliokuwa wanawekwa na JPM, wananchi watake wasitake, na kura zake huwa hazijulikani mpaka Leo hii
 
Wana Chato wamejiapiza kwamba uchaguzi wa ubunge unaokuja, wanakwenda na Katwale.
Wanachato wanasema kwamba Katwale alikuwa chaguo lao lakini JPM alimpandikiza Kalemani...
Kama mnataka umeme hamisheni huo uwanja wa ndege mlio jengewa na mungu wenu uletwe Mbeya wewnye tija. Hasara mliyo tupa ninyi watu ni kubwa mno.

Naskia mmewekewa taa za barabarani wakati mnamilikik baiskeli. Fungueni hizo taa za barabarani mkaweke majumban kwenu.
 
Omba kura kabisa
Uchaguzi wa wajumbe wa mkutano mkuu CCM taifa kutoka chato, jamaa alizoa kura za kutisha mpaka Kalemani akalalamika eti kwa nini anagombea, anatishia ubunge wake, mara....ohhhh, sijui nini.

Sasa tunakuja kwenye ubunge, hiyo ilikuwa taa ya njano kuashiria apishe njia, le shing'weng'we lashikaga
 
Kwahiyo akiwa.Waziri wewe ndio utakosa Ubunge wa Chato?
Namuona Katwale akiwa Naibu Waziri nishati, kabla ya kuchukua uwaziri kabisa ili akachimbue mambo ya Kalemani pale wizarani, na kuyaanika
 
Mleta mada ni mh katwale mwenyewe. Shida ya kalemani huwa hapokei simu za wanna chato
 
Kalemani atakuwepo Chato, wewe mlamba asali tafuta na chumvi ulambe.
 
Kalemani hawezi kutoka Chato kwa kunyimwa kura na wananchi, labda afanyiwe figisu ndani ya chama.
 
Back
Top Bottom