Chato yatangazwa kuwa kitovu cha Utalii Kanda ya Ziwa

Kwa yanayoendelea Chato ili Magufuli aeleweke anapaswa kupeleka miradi mikubwa pia kwa watangulizi wake tofauti na hapo dhana ya upendeleo itapata nguvu na kuwapa cha kusema wenye nia ovu.
“Wenye nia ovu” yaani hata haya mtu ukiyasema unakuwa na nia ovu? Kwa mfano wewe umekosoa japo sio direct, je una nia ovu, au ulitaka kusemaje mkubwa.
 
137032254_2005378632936951_505961696190857437_n.jpg
 
Serengeti tupa kule, na tutahakikisha inakufa maana ndio inazuia watalii wasije huku burigi kutalii.
 
Huu uongozi unataka watu kama hao. Watu makini kama Hussein Bashe, hafiki popote ataishilia naibu tu. Utwala wa kidini, kikabila unaoongozwa na akili ndogo. Rwanda leo uchumi unakuwa kwa asilimia 15% kwa sababu umewapa nafasi wasomi wake wa kweli. Sio hawa Madokta uchwara. Ukiangal[a programme zao utaona zinaendeshwa kisomi. Watoto wanatumia laptop, hata utalii wao utatushinda hivi karibuni ingawaje hawana vitu vingi. Sisi kazi ni kuwachukia wageni 'mabeberu' na kujifanya tuna kila kitu wakati umaskini ndiyo unazidi. Kazi kusifiana tu, ukisema ukweli unafungwa! Stupid kabisa.
 
Usilinganishe ka Rwanda kenye watu 14 ml. na Tanzania yenye 60 ml. Utakosea sana
 
Waziri wa Utalii na Maliasili, Dkt. Damas Ndumbaro akiwa ziarani Mkoani Geita ametangaza rasmi kuwa Chato ndio kitovu cha Utalii Kanda ya Ziwa

Amesema wamefikia uamuzi huo kwasababu kuna Utalii wa aina mbalimbali katika Wilaya hiyo ikiwemo wa Misitu, Maji, Hifadhi za Taifa na Uwindaji. Pia, Uwanja wa Ndege wa Chato utawezesha Watalii kusafiri kwa uhakika na urahisi

Vilevile, Waziri Ndumbaro ameielezea Chato kuwa eneo tulivu, hali ambayo inapendwa na Watalii.

Labda watalii wa ndani vingine ni ngumu kupata hawa wazungu maana haina kitu tofauti.
 
Kwa ujumla ukanda wa ziwa na kusini umesahaulika sana kiutalii. Kwa kuitangaza Chato kituo kikuu cha Utalii mimi ninaamini itachochea sana kukua kwa utalii kanda ya ziwa na nchini kwa kuusambaza maeneo mengine badala ya kutegemea Arusha pekee. Kwa msingi huo Mpango Kabambe ( Tourism Master Plan) nao iweke mikakati endevu ya kuboresha utalii kanda hii na kanda za kusini na Magharibi kwa dhati. Ni kweli kwenny kanda ya magharibi na ziwa kuna Serengeti, Sanane, Burigi Chato,Rumanyika, Gombe lakini zimemezwa na Utalii wa Arusha kwa sababu za kisiasa na historia. Ni wakati sasa kuangalia na maeneo mengine na TTB kuchukua jukumu la kuyatangaza ipasavyo badala ya kug'ag'ania eneo moja tu Arusha. Kwa msingi huo viwanja vya ndege vya kimataifa vya Mwanza, Chato vikamilishwe mapema hususan pax terminal ili kuwa sehemu ya kuboresha miundo mbinu ya kiutalii wa maeneo haya iwapo kuna nia ya dhati ya kuendeleza utalii kanda ya ziwa. Aidha maofisi ya hadhi ya kimataifa ya TANAPA,TTB na Vituo vya utalii wa kiutamaduni, waekezaji wa mahoteli ya nyota 3-5 wahamasishwe na wapewe maeneo wawekezaji makini kujenga, makampuni ya Tour operators yapewe nafuu ya kikodi kuwekekeza maeneo hayo.Kwa ujumla nia ya Serikali iendane na vitendo kuifanya Chato kituo cha Utalii kanda hii na na maeneo yanayozunguka eneo husika ili kujenga linkage. Aidha wananchi wahamasishwe ili kubadili mindset zielekee kwenye kukumbatia uchumi wa utalii. Bila hatua madhubuti itaishia kuwa hadaa kwa kauli za kisiasa. Tunataka vitendo.
 
Waziri wa Utalii na Maliasili, Dkt. Damas Ndumbaro akiwa ziarani Mkoani Geita ametangaza rasmi kuwa Chato ndio kitovu cha Utalii Kanda ya Ziwa

Amesema wamefikia uamuzi huo kwasababu kuna Utalii wa aina mbalimbali katika Wilaya hiyo ikiwemo wa Misitu, Maji, Hifadhi za Taifa na Uwindaji. Pia, Uwanja wa Ndege wa Chato utawezesha Watalii kusafiri kwa uhakika na urahisi

Vilevile, Waziri Ndumbaro ameielezea Chato kuwa eneo tulivu, hali ambayo inapendwa na Watalii.

Mpiga picha wako hajitambui! Alitakiwa kuchanganya picha za mapori ya asili ya burigi chato badala ya kuonyesha msitu wa kupandwa na watu mfyyyyuuuuu!
 
Waziri wa Utalii na Maliasili, Dkt. Damas Ndumbaro akiwa ziarani Mkoani Geita ametangaza rasmi kuwa Chato ndio kitovu cha Utalii Kanda ya Ziwa

Amesema wamefikia uamuzi huo kwasababu kuna Utalii wa aina mbalimbali katika Wilaya hiyo ikiwemo wa Misitu, Maji, Hifadhi za Taifa na Uwindaji. Pia, Uwanja wa Ndege wa Chato utawezesha Watalii kusafiri kwa uhakika na urahisi

Vilevile, Waziri Ndumbaro ameielezea Chato kuwa eneo tulivu, hali ambayo inapendwa na Watalii.

Hiyo airport ipo eneo gani kwa google map washirika
 
Back
Top Bottom