Chato yazidi kuneemeka; Serikali kujenga Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Ziwa

Chato yazidi kuneemeka; Serikali kujenga Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Ziwa

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2018
Posts
882
Reaction score
3,337
Serikali ya Tanzania itajenga Hospitali ya Rufaa wilayani Chato Mkoa wa Geita.
Akiwasilisha taarifa yake kwa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii leo Jumatatu Januari 20, 2020, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu amesema Serikali inatarajia kujenga hospitali hiyo kutokana na idadi kubwa ya watu kuwa eneo hilo.

“Tumefanya utafiti na kugundua kuna wagonjwa wengi Kanda ya Ziwa kwa hiyo tunajenga Zonal Hospital (hospitali ya Kanda) Chato,” amesema.

Amesema kuwa sababu ya kujenga hospitali hiyo Chato ni Mikoa ya kanda ya ziwa kuwa na watu zaidi milioni 15.

Baada ya Waziri Ummy kueleza hayo, baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CCM), Peter Serukamba walicheka.

Baadaye wajumbe wa kamati hiyo watapata fursa ya kuichangia na kama kutakuwa na maswali, mapendekezo watayatoa.

Chanzo: Mwananchi

Pia soma Serikali kujenga hospitali ya kikanda ya kitalii Geita
 
Serikali imesema ina dhamiria kujenga hospital ya kanda ya Ziwa huko Chato mkoani Geita

Waziri wa Afya jinsia na watoto amebainisha hilo leo

My take: kwa nini ijengwe Chato na si Mwanza kitovu cha kanda ya Ziwa au Geita makao makuu ya mkoa?

Source Mwananchi

Sent using Jamii Forums mobile app

Watu walipoanza kujenga Ma Hotel Makubwa makubwa Chatto tukawaona hamnazo kumbe wameshajipanga vya kutosha

Kila la Kheir wana Chato

Ila maendeleo yanatabia moja mbaya sana

Wageni na Wazawa hufukuzwa na maendeleo hayo hayo

Wazaramo wamebaki wa kutafuta K.koo

Mtwara mjini Wamakonde wameanza kuwa wapangaji kwenye nyumba za Wahaya na Wapemba

Dodoma mjini ukimuona Mgogo basi kuwa kaja kama sio kuuza ubuyu basi zabibu
 
😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂
Unamcheka Waziri au wazo lake

Me nachekea pembeni japo sijui kinachonichekesha
 
Ngoja na mimi nimcheke.
Kwani Bugando ni aje?
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
🤣 🤣
 
Back
Top Bottom