Chato yazidi kuneemeka; Serikali kujenga Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Ziwa

Chato yazidi kuneemeka; Serikali kujenga Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Ziwa

From Musoma to Chato kwenda kutibiwa
Serikali ya Tanzania itajenga Hospitali ya Rufaa wilayani Chato Mkoa wa Geita.
Akiwasilisha taarifa yake kwa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii leo Jumatatu Januari 20, 2020, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu amesema Serikali inatarajia kujenga hospitali hiyo kutokana na idadi kubwa ya watu kuwa eneo hilo.

“Tumefanya utafiti na kugundua kuna wagonjwa wengi Kanda ya Ziwa kwa hiyo tunajenga Zonal Hospital (hospitali ya Kanda) Chato,” amesema.
Amesema kuwa sababu ya kujenga hospitali hiyo Chato ni Mikoa ya kanda ya ziwa kuwa na watu zaidi milioni 15.

Baada ya Waziri Ummy kueleza hayo, baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CCM), Peter Serukamba walicheka.

Baadaye wajumbe wa kamati hiyo watapata fursa ya kuichangia na kama kutakuwa na maswali, mapendekezo watayatoa.

Chanzo: Mwananchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wacha Nyerere aitwe baba wa Taifa.
Ingawa nahisi watu wa 'Butihama' karibuni wataanza kumlaumu kwa kutotumia fursa.
Mzee Mwinyi na Kikwete mlikwama wapi mbona Mkoa wa Pwani haukupata mavitu makubwa haraka?
Hadi leo hakuna mataa ya kuongozea magari kama 'Chattle'
 
... Ummy naye kashindwa kujenga hoja vizuri. Kama Kanda ya Ziwa ina "wagonjwa" wengi kuliko maeneo mengine kwanini Chato? Au Chato ni center ya kanda ile? Kwanini sio Kahama, au miji mingine mikubwa kama Shinyanga?
 
Back
Top Bottom