Chato yazidi kuneemeka; Serikali kujenga Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Ziwa

Chato yazidi kuneemeka; Serikali kujenga Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Ziwa

Hii si sawa, kanda ya ziwa hospitali za rufaa mbili, kanda ya kusini hakuna, kanda ya magharibi hakuna. mmhh ukabila/ ukanda unapanda chati, umoja mshikamano utaporomoka tusipojisahihisha
... huko Kanda ya Kusini na Kanda ya Magharibi mko wangapi? Hamjazi hata kibaba ninyi! Hoja ya Waziri Ummy ni kwamba Kanda ya Ziwa wako wengi! Hata Prof. Kabudi aliwahi kulisemea hili nadhani kwenye Sherehe za Uhuru Mwanza (2019). Mtakapokuwa "wengi" mtajengewa! Ha ha ha.
 
Ni mtazamo tu nenda kwenye sensa ya 2012 utajua wako wangapi huko kusini na magharibi. kanda ya ziwa inajazwa na haohao kutoka kanda ya magharibi na kagera kwa kukosa huduma, daresalaam inajazwa kutoka kusini kwa kukosa huduma, narudia si haki, mshikamano wetu umetetereka
 
... dah! Umenikumbusha MATEMBEZI YA MSHIKAMANO! Sijui hii kitu iliishiaga wapi.
 
Na bado. Tukiingia muhula wa pili, hakuna rangi tutaacha kuona kuhusu "kupeleka" maendeleo kule. Vitafanyika hata vile ambavyo huwezi kutarajia vifanyike kule.
 
Mara, Simuyu, Kahama na Shinyanga wajisogeze Bugando na Sekou Toure!

Bukoba, Ujiji, Kigoma, Biharamulo wajisogeze Chato.

Toka Muingeleza ameondoka watu wa Kigoma na Kagera kila kitu mpaka wakifuate Daslam, Haiwezekani! Kabisa

Akimaliza hospitali aweke Chuo Cha Kimataifa Nyanza University.
Ukweli hatuna pesa hizo za mavitu makubwa mapya kila siku.
Kwanini tusiboreshe au kutanua miundombinu, vifaa tiba na rasilimali watu kwenye hospital hizo zilizopo tayari Mwanza, na pesa ya ziada tukaelekeza kwenye mambo mengine kama kuwapa mikopo watoto wa vyuo vikuu waliokosa mkopo kama yule ambae kakosa mkopo kisa mjomba wakati ana maisha nafuu alimsomesha sekondari shule binafsi?

Kwanini tusiweke kwenye madawa hiyo pesa ya ziada?
 
... kwa hiyo ni kanuni siku hizi kwamba huduma muhimu za kijamii - hospitali, vyuo, n.k. sharti viwe katikati? Kwamba "pembezoni" hawana chao?
Pembezoni ipi unayoisemea?! Daslam?, Zama hizo zimeisha.

Kwa takribani miaka 60 sasa wakazi wa Kigoma na Kagera wamekuwa wakifuata huduma za kijamii Daslam, Elimu ya juu, Hospitali, Usafiri wa Kimataifa na mengineyo. Haiwezekani hii lazima ifike ukomo kwa maendeleo ya taifa hili! U-Daslam lazima ufe.
 
... Ummy naye kashindwa kujenga hoja vizuri. Kama Kanda ya Ziwa ina "wagonjwa" wengi kuliko maeneo mengine kwanini Chato? Au Chato ni center ya kanda ile? Kwanini sio Kahama, au miji mingine mikubwa kama Shinyanga?
Naunga mkon hoja yako.
Waziri Ummy aje atetee hoja yake vizuri tuelewe juu ya hili suala maana linaweza kuleta muongozo mbaya sana siku za mbeleni.
 
Back
Top Bottom