Chato yazidi kuneemeka; Serikali kujenga Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Ziwa

Chato yazidi kuneemeka; Serikali kujenga Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Ziwa

Ukweli hatuna pesa hizo za mavitu makubwa mapya kila siku.
Kwanini tusiboreshe au kutanua miundombinu, vifaa tiba na rasilimali watu kwenye hospital hizo zilizopo tayari Mwanza, na pesa ya ziada tukaelekeza kwenye mambo mengine kama kuwapa mikopo watoto wa vyuo vikuu waliokosa mkopo kama yule ambae kakosa mkopo kisa mjomba wakati ana maisha nafuu alimsomesha sekondari shule binafsi?

Kwanini tusiweke kwenye madawa hiyo pesa ya ziada?
Miundombinu isipojengwa sasa unataka ijengwe lini?! Watu walishamaliza haya masuala wapo wanabuni kuishi sehemu nyingine.

Namibia, Botswana, Rwanda wanamaliza, je unataka kuanza kujenga Hospitali 2050? Unataka uanze kujenga Reli 2070? Itakuwa aibu kwa Taifa hili!

Nigeria kila Kanda/State inachuo level za kimataifa same South Africa same Morocco hadi Ghana?! Haiwezekani

Lazima tuyafanye sasa, japo 2025 tuanze urutubishaji na ujenzi wa vinu vya nyuklia.
 
Baada ya Waziri Ummy kueleza hayo, baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CCM), Peter Serukamba walicheka.
yah..... na mimi nimei bold hapa chini!

Baada ya Waziri Ummy kueleza hayo, baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CCM), Peter Serukamba walicheka.
 
Ni mtazamo tu nenda kwenye sensa ya 2012 utajua wako wangapi huko kusini na magharibi. kanda ya ziwa inajazwa na haohao kutoka kanda ya magharibi na kagera kwa kukosa huduma, daresalaam inajazwa kutoka kusini kwa kukosa huduma, narudia si haki, mshikamano wetu umetetereka
Kuepeusha kujazajaza Daslam na Mwanza lazima tupeleke maendeleo sehemu nyingine, hii ndio tiba pekee.

Baada ya Hospital hii ya Kanda Mh. Magufuli asisahau chuo cha Kimataifa.
 
Chato inatokana na neno la kifaransa Chateau-
Château
A château is a manor house or residence of the lord of the manor or a country house of nobility or gentry, with or without fortifications, originally—and still most frequently—in French-speaking regions.
 
Pembezoni ipi unayoisemea?! Daslam?, Zama hizo zimeisha.

Kwa takribani miaka 60 sasa wakazi wa Kigoma na Kagera wamekuwa wakifuata huduma za kijamii Daslam, Elimu ya juu, Hospitali, Usafiri wa Kimataifa na mengineyo. Haiwezekani hii lazima ifike ukomo kwa maendeleo ya taifa hili! U-Daslam lazima ufe.
... sawa Mkuu. Nakubaliana na wewe, elimu ya juu, hospitali, usafiri wa kimataifa vijengwe CHATO sasa badala ya Dar-es-Salaam au maeneo mengine ya nchi. Sawa sawa kabisa.
 
Hii si sawa, kanda ya ziwa hospitali za rufaa mbili, kanda ya kusini hakuna, kanda ya magharibi hakuna. mmhh ukabila/ ukanda unapanda chati, umoja mshikamano utaporomoka tusipojisahihisha
Kusini inajengwa sasa, magharibi walisema watajenga Tabora baada ya kusini kuisha..

Typed Using KIDOLE
 
Kuepeusha kujazajaza Daslam na Mwanza lazima tupeleke maendeleo sehemu nyingine, hii ndio tiba pekee.

Baada ya Hospital hii ya Kanda Mh. Magufuli asisahau chuo cha Kimataifa.
... sawa. Kurundika maendeleo Chato ndio mwarobaini wenyewe!
 
Sawa mkuu.
Lakini Mwanza ndio katikati na hufikika kirahisi kutoka maeneo ya wilaya na mikoa jirani.
Mwanza tayari kuna Bugando na Sokou Toure sijui?

Kwanini zisihimarishwe hizo au isijengwe mpya Mwanza?

Ila mimi sio adui ni mtu ninae litakia mema taifa na kiongozi wetu mpendwa.
Mtu mzuri ni yule anaye kukumbusha na kukuambia ukweli unapokuwa unakosea jambo.
Mwambieni ukweli huyo waziri alie peleka wazo la kupeleka Hospital hiyo Chattle kwamba anakosea pakubwa.
Hizo Hospital za Mwanza ni bora labda kuongezewa vifaa na wataalamu. Lakini kusema aikomalie Mwanza yatatokea ya U-Daslam ambayo hatutaki kuskia.

Tunaratajia kufikia 2030 kila Mkoa uwe na Hospital ambayo inamaliza kila kitu kwa maendeleo endelevu ya Tanzania na Africa kwa ujumla.

Tumechelewa Sana, tujaribu kwenda na kasi sasa.
 
Kuepeusha kujazajaza Daslam na Mwanza lazima tupeleke maendeleo sehemu nyingine, hii ndio tiba pekee.

Baada ya Hospital hii ya Kanda Mh. Magufuli asisahau chuo cha Kimataifa.
Chatoooo
tapatalk_1577999380187.jpeg


dodge
 
Kuepeusha kujazajaza Daslam na Mwanza lazima tupeleke maendeleo sehemu nyingine, hii ndio tiba pekee.

Baada ya Hospital hii ya Kanda Mh. Magufuli asisahau chuo cha Kimataifa.

Naona umechachamaa hatari kujibu ..
Hakuna alopinga huduma za jamii kuwepo kila nyanda.. Hoja hapa ni Hivi kweli ni Chato tuu? Hapa hakuhitaji hata akili ya darasani kuelewa kuna upendeleo kwa chato(tusitaje yalowekwa chato ) ambako sehem nyingine penye uhitaji zaidi hapakupewa kipaumbelele

Huduma ya jamii inatakiwa iwe sehem yenye kuhitajika sana na kufikaka kwa urahisi yaan umbali na miundo mbinu bora jee kwa kanda ya Ziwa nzima hapo chato ndo katikati et? Au tutete tuu ilimradi ugali uwepo mezani siku ziende...
 
Kwahiyo wajumbe walicheka hivo na sisi tucheke kwanza kidogo?


Sent from my iPhone using JamiiForums
... cheka kidogo mkuu; itasaidia japo kupandisha "hapiness index" ya nchi kama nchi zenye furaha zaidi duniani. Tunaweza kuzipiku Scandinavia kimasihara! Ha ha ha ha ha ha ha ha ha!
 
Back
Top Bottom