Uchaguzi 2020 CHAUMMA kushiriki Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 2020

Uchaguzi 2020 CHAUMMA kushiriki Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 2020

mkiluvya

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2019
Posts
809
Reaction score
729
1591512269920.png

Chama cha Upinzani cha CHAUMMA, kimetangaza rasmi kushiriki Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Mwenyekiti wake, Hashim Rungwe Spunda amesema wanavikaribisha vyama vingine kuungana nao wakati ambao CHAUMMA inaelekekea kuchukua dola.

Rungwe amesema, hivi karibuni Chaumma itatoa ratiba ya uchukuaji na urejeshaji fomu za wanachama wake watakaohitaji kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi huo.

Wakati huo huo, Rungwe amesema Chaumma imekamilisha kuandaa ilani yake ya uchaguzi na kwamba kiko katika mchakato wa kuiwasilisha katika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Aidha, Rungwe ameomba wananchi wenye mapenzi mema na chama hicho, kuchangia fedha kwa ajili ya kutekeleza shughuli za kampeni.
 
Basi sawa mzee wetu, lkn naona CHAUMMA wame base tu kwenye urais tu , je nafasi nyingine Kama udiwani na ubunge mbona Kama hajaliwekea mkazo..au mm tu ndo cjamuelewa???
 
Huyu M/Kitiwa mda mrefu lakini asakamwi kama Mbowe...

Ngoja nikachukue fomu nigombee ubunge na mimi
 
Huyu ndio alisema,
Nilishinda Urais ika kura zangu waliiba,

Umejuaje kama waliiba?

Sehemu nilikopiga kura na nikajipigia mimi mwenyewe matokeo yalipotoka ilionekana nimepata kura 0.

Hivyo ikiwa hata kura yangu niliyojipigia mimi mwenyewe wameiiba ni ngapi watakuwa wameiba?

MATAGA
 
Alisema alishangaa kupata pole nyingi kuliko kura alizopata.
 
Back
Top Bottom