Mwizukulu wa Buganda
Member
- Nov 19, 2024
- 94
- 307
Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) Mkoa wa Morogoro Ismail Rashidi Ismail amesema licha ya chama hicho kushindwa kufanya vizuri katika uchaguzi wa serikali za mitaa, lakini bado hawajakata tamaa ya ushiriki na kushinda katika uchaguzi mkuu ambao unatarajia kufanyika mwaka huu 2025.
Akizungumza na JAMBO TV mkoani Morogoro, amesema kuwa lengo la chama hicho ni kuhakikisha wanashika dola na kumfanya kila mwananchi kula ubwabwa na kuku kama chakula cha kawaida.
Mwenyekiti huyo ameongeza kwa kusema kuwa chama chake kinalenga kujenga mfereji wa maji utakaoipeleka bahari Dodoma na kujenga daraja kutoka Dar es Salaam kuelekea Zanzibar ambapo itawasaidia wananchi kutumia gharama nafuu za usafiri.
Pia soma
- LGE2024 - CHAUMA: Chagua viongozi wa CHAUMA na Sera ya Ubwabwa, huwezi kufanya maendeleo bila kushiba!