PreGE2025 CHAUMMA yawateua Mrema, Ruge kuwa Wakurugenzi wa Habari na Uchumi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kamati Kuu ya Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) imefanya uteuzi wa wakurugenzi wa idara mbalimbali ya chama hicho akiwemo John Mrema kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Taarifa kwa Umma.

Mrema atasaidiwa na Ipyana Samsom ambaye awali alikuwa akiiongoza Idara hiyo.

Aidha, Catherine Ruge ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Uchumi, Fedha na Mipango.

Uteuzi huo umetangazwa na Katibu Mkuu wa Chaumma, Salum Mwalimu baada ya kumalizika kikao hicho kilichofanyika leo Jumamosi Mei 24, 2025 jijini Dar es Salaam na kuongozwa na mwenyekiti wake, Hashim Rungwe.

Mwalimu amesema walioteuliwa wana uzoefu mkubwa kwenye maeneo yao hivyo hana shaka watatumika vilivyo.

Kuna watu wanajiona wamekuja duniani kuongoza tu, akiwekwa pembeni hukasirika kama mrema
 
Hahhahahh hii nchi inanifurahishi hivi wakiitwa upinzani na Chauma wataenda?
 
Kamati Kuu ya Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) imefanya uteuzi wa wakurugenzi wa idara mbalimbali ya chama hicho akiwemo John Mrema kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Taarifa kwa Umma.

Mrema atasaidiwa na Ipyana Samsom ambaye awali alikuwa akiiongoza Idara hiyo.

Aidha, Catherine Ruge ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Uchumi, Fedha na Mipango.

Uteuzi huo umetangazwa na Katibu Mkuu wa Chaumma, Salum Mwalimu baada ya kumalizika kikao hicho kilichofanyika leo Jumamosi Mei 24, 2025 jijini Dar es Salaam na kuongozwa na mwenyekiti wake, Hashim Rungwe.

Mwalimu amesema walioteuliwa wana uzoefu mkubwa kwenye maeneo yao hivyo hana shaka watatumika vilivyo.

Mungu ibariki CHAUMMA.Mungu mbariki Mzee Hashimu Rungwe Spunda
 
Back
Top Bottom