Makundi ndani ya CCM waliokulia mjini na wale makuzi ya shamba.
Siasa Ufashisti dhidi ya siasa za umaarufu ndani ya CCM.
Katika pepa ya society for social anthropology
Ufashisti ni itikadi yetu dhidi yao inayowaunganisha wafuasi dhidi ya wale wanaoonekana kama wengine, nje ya uhalisia wao wenyewe wa mipaka ya kijamii, kimaadili, kimaadili, na kidini (Stanley 2020 [2018]).
Sio sawa na siasa za lebo ya umaarufu *(
populism). Kwa upana, populism inapendekeza kwamba wasomi wanapaswa kuondolewa madarakani na kwamba siasa inapaswa kufuata matakwa ya raia (Mudde na Kaltwasser 2017).
Jamii za vijijini, watu wasiojiweza kiuchumi, na wale wasio na digrii za chuo ni haraka kuorodheshwa kama watu maarufu (Hochschild 2016). Mara nyingi umashuhuri hutumika kama lebo rahisi kwa waandishi wa habari na wasomi kubadilisha jinsi wapiga kura wa vijijini wanavyotenda na kufikiria, bila kuzingatia mantiki changamano ya ndani na ujamaa tofauti wa jamii hizi. Populism haina faida katika kuelewa uundaji wa ufashisti unaoongezeka nchini Marekani, haswa wale wanaolenga kuongeza muundo wa mamlaka badala ya kudhoofisha.
Jumuiya za vijijini ambazo nimefanya kazi nazo hazikuwa na nia ya kukuza dhana ya bahati yaani kuteuliwa na Mungu au sauti ya watu wengi.
Walikuwa na nia ya kuendeleza
mapenzi ya Mungu kwa kukuza sauti yake kupitia uongozi wa kisiasa wenye mamlaka ambao ungeweza kuunganisha dini na Serikali. Source :
The Hybridity of Rural Fascism
CCM KUTOKA UFASHISTI HADI MAZINGIRA YA MARIDHIANO
Kwa Tanzania toka 2015 Tumeona kipindi cha wakuja ndani ya CCM kutumia sana viongozi wa dini katika kujijengea umaarufu wa kukubalika siasa hadi waliokulia mjini kina Abdulrahman Kinana, Nape Nnauye, January Makamba, Jakaya Kikwete na hata wa Kizimkazi ambapo ni kitongoji chenye umjini kutoridhika na jinsi washamba walivyokivamia chama.
Sasa waliokulia mjini wameongezwa kushika nafasi za maamuzi chamani Dr. Nchimbi, CPA Amos Makalla, Mongela, Jokate huku wazee wazima Abdulrahman Kinana, Jakaya Kikwete wakiona project ya kukirudisha chama kwa waliokulia mjini ndiyo wanaweza kutekeleza zile 4R vizuri kwa midahalo, hoja na maridhiano badala ya ubabe na kutumia dhana kiongozi amechaguliwa na Mungu.
Wale walioingia 2015 baada ya uchaguzi mkuu waliwateka nyara siyo tu raia wote wa Tanzania bali hata mawazo huru ya wanaCCM yalipigwa marufuku. Siasa za umaarufu kuwa najaza watu wengi hivyo hakuna haja ya shughuli za kisiasa kuendelea, wakabuni hapa ni kazi tu zilijikita mizizi. Baadhi ya wanaCCM waliotaka kupaza sauti walibanwa tukaona mazungumzo yao kurikodiwa bila ridhaa zao kisha yakatupwa ktk media kuwadhalilisha.
Kwa uungwana wa kukulia mjini wakatinga ikulu kumuomba msamaha kiongozi alitejijengea umaarufu kwa gharama kubwa ya kukosa demokrasia ndani ya chama, kuanzisha miradi mikubwa kwa mpigo wakijipigia jaramba kuwa bila wao haitaisha hivyo kutafsiri watawale milele ili miradi ikamilike hata ikiwa ni 2050.
Kwa kuwa ilani ya CCM ipo ktk kila meza za wakuu wa mkoa, mawaziri na maelekezo ya fikra za Mwenyekiti ya 4R, wateule hao katika utumishi wa serikali hadi ngazi ya maDED itabidi wafuate maagizo na matamamio ya viongozi hawa wapya wa chama kuwa zama za siasa za umaarufu zimekwisha, nchi hii ni ya wote bila kujali vyama.
ANTHROPOLOJIA Anthropolojia ni taaluma inayohusikana elimu ya binadamu hususan elimu inayohusu habari za asili na maendeleo yake ya awali .