Chawa wa mama: Namshukuru mama Samia kwa tope la Hanang

Chawa wa mama: Namshukuru mama Samia kwa tope la Hanang

Kuna msemo ya kiswahili usemao "kuchamba kwingi......"
Sasa hata sifa zikizidi hupelekea dhihaka.

Mwaka 2016 kitovu cha kupatwa kwa mwezi dunia nzima kilikuwa mkoani Njombe eneo la Wanging'ombe. Wageni mbalimbali toka pande zote za dunia walikwenda Njombe ili kuona tukio la kupatwa kwa jua na kuchukua picha zake.

Mwananchi mmoja aliposogezewa microphone na media alisikika akimshukuru sana rais Magufuli kwa tukio lile. Watu wakabakia midomo wazi kwa mshangao.

Leo huko Hanang mwancnhi mmoja baada ya kupokea msaada wa godoro amesikika akimshukuru mama Samia kwa tope lililotokea nakupelekea watu/makampuni/serikali kutoa misaada mbalimbali huko.

N.B . Siyo kila sifa ni sifa.
Mie naishukuru sana serikali kwa kukuletea mvua naamini mwaka huu tutavuna mazao mengi sana
 
Ķwa kweli kujiondoa akili kabisa, ubakie kichwa kitupu kabisa, ujifanye mwehu kabisa, kama anavyofanya Lucas Mwashamba, kunahitaji ujasiri wa ajabu. Ni sawa na mtu uambiwe, siku wanapocheza simba na Yanga, kabla ya mechi, wewe uende katikati ya uwanja uvue nguo zote usalie kama ulivyozaliwa! Siyo jambo rahisi, lakini kuna watu ni majasiri hasa. Fikiria mtu kama Lucas anatumia jina lake halisi, anaweka na namba yake, halafu toka mwanzo mpaka mwisho, anaandika upuuzi mtupu!!!
Jamaa yule nishmadharau, wakati mwingine anachoandika sijishughulishi hata kusoma.
Mungu anisamehe ila machawa huwa naona kama ni MAPUNGA zeze.
 
Back
Top Bottom