CHECHEFU MAHAKAMANI TENA
Safari hii ni kampuni ya NAS HAULIERS iliyokopa bilioni 50 ikakataa kulipa na kukimbilia mahakamani ikiishitaki benki iliyofanikisha mkopo
- ikitetewa na wakili yule yule mzee wa Mikopo chechefu, Mahakama ikaipa ushindi
- Leo inapandishwa kizimbani Mahakama ya Rufaa mbele ya majaji watatu
- Mbivu na mbichi ni mbele ya Jaji Mkuye, Jaji Mwampashi na Jaji Muruke watakaoketi kusikiliza kesi
- Jamvilahabari kuupasha umma mwanzo mwisho
Na. Mwandishi wetu,
Mahakama ya Rufaa chini ya majaji watatu Mkuye, Mwampashi na Jaji muruke leo wanataraji kuketi kusikiliza shauri la aina yake baina ya benki ya Equity dhidi ya kampuni ya NAS HAULIERS shauri la madai linalopinga hukumu iliyowapa ushindi kampuni ya NAS dhidi ya benki hiyo hukumu inayotajwa kuwa na mazongezonge kwa kuruhusu mkopaji kutokulipa mkopo licha ya kukiri mahakamani kuwa alikopa na benki hiyo ndio iliyomfanilishia upatikanaji wa mkopo huo kwa yenyewe kutoa hati ya barua (Later of credit) kwa mkopeshaji aliyepo nje ya nchi
Ni katika kesi ambayo hukumu yake inapingwa mahaka ya Rufaa na kutaraji kusikilizwa leo ndipo mlalamikaji NAS HAULIERS anakiri kupokea mkopo wa kiasi cha dola milioni 16 (wastani za bilioni 40) za kitanzania ambazo anaeleza kuwa alizitumia kufuta mikopo aliyokuwa anadaiwa na mabenki kadhaa hapa nchini na kiasi kingine kukitumia kama mtaji wa uendeshaji (working Capital) lakini mahakama ikamtangaza mkopaji huyo kuwa hadaiwi na hastahili kulipa mkopo huo
Katika mazingira yanayotiliwa shaka na kuuweka hatiani weledi na heshima ya Mahakama, ni pamoja na kitendo cha mkopeshaji anayefahamika kama Lamar kutoka Dubai kukiri mbele ya mahakama kuwa aliikopesha kampuni ya NAS kwa kudhaminiwa na Banki ya Equity kwa kutoa letter of Credit na kwamba NAS HAULIERS waliposhindwa kurudisha mkopo kama ilivyokubaliana katika makubaliano yao Equity walikuwa na wajibu wa kuulipa mkopo huo, bado mahakama haikuona kama kuna haja ya NAS kulipa mkopo huo na badala yake akapewa ushindi
Rufaa hiyo inayotaraji kusikilizwa leo inategemewa kuvuta hisia za wafuatiliaji wengi kutokana na ukweli kwamba hukumu ya kesi hiyo imestaajabisha watu wengi sana nchini na ndani ya nchi
" Ni bahati mbaya tu jambo lipo Mahakamani hivyo si vyema kulijadili na kulichambua, ila ukweli usemwe tuu. Ukisoma hukumu ile unaweza usiamini kama ni jaji anayetegemewa na jamii kutenda haki ndio ametoa hukumu ile. Havieleweki kwa kweli". Anasema Josh Manga mtaalam wa Sheria za kodi
"hata wakili mwalongo alipojitokeza hadharani kufanya alichokiita kuwanasua wateja wake, haikupaswa kuwa ilivyokuwa. Wakili ameibua maswali mazito kuliko majibu aliyotaraji kutoa". Ameongeza
Ameongeza kuwa Mahakama ya Rufaa ni sehemu ya mwisho katika mfumo wa utoaji wa haki na kwamba namna yotote ya kuona haki imechezewa huku chini, basi mahakama ya Rufaa inategemewa kusimama imara kutenda haki
Hivi karibuni gazeti hili lilipoti kuwa
Jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kukaribisha na kuhamasisha uwekezaji wa ndani na kutoka nje ya nchi kuja kuwekeza nchini unaelezwa kutiwa kigingi na tabia chafu inayozidi kuota mizizi ya baadhi ya wafanyabiashara wakubwa kushirikiana na baadhi ya majaji wa mahakama kuu wasio waaminifu kuyatapeli mabenki ya ndani na nje ya nchi kwa na hivyo kuwanyima fursa wafanyabiashara wadogo na wakati kushindwa kuaminiwa na kupata mikopo.
Orodha ya wafanyabiashara wanaotumia mahakama kutapeli na kudhulumu mabenki iliyofanyiwa uchunguzi na kuthibitishwa na gazeti hili, inaonyesha kuwa wengi kati ya wafanyabiashara hao wanajihusisha na biashara za Mafuta na ushafirishaji ambapo wastani wa shilingi za kitanzania Trilioni 1.3 wamekopa katika benki mbalimbali za ndani nan je ya nchi na kukataa kulipa kisha kukimbilia mahakamani ambako pia wanadaiwa kupata ushindi kwa njia zisizo za kawaida ZAIDI.
Gazeti hili litaendelea kuweka wazi mchezo wote