Ukweli ni kwamba, kizazi cha mashabiki wa Sir Nature kimeshavuka umri wa kwenda kwenye matamasha ya mziki ya viwanjani.
Kwa audience ya wasafi festival ya sasa ambao wengi ni vijana wa vyuo na under 25, jina la Juma nature ni historia, Juma hana mashabiki tena pale.
Sasa ni kizazi cha kina rayvanny na wenzake, japo wanaimba ujinga, ila ndo vitu vijana wa sasa wanataka kuvisikia. Hii imewatoa wakongwe wengi kwenye game. Akina jay mo, profesa, afande sele na kina juma.
Kutunza heshima, ni kustaafu muziki na kufanya shughuli nyingine kama anavyofanya solo thanks au Mr paul. Wamebaki na heshima yao kwa kuusoma mchezo mapema.
Juma ukitaka kuendelea kubaki valid kwa umri huu utapotea. Sasa watoto wanataka kukulipa 500k. Unaanza kulalamika wanakuvunjia heshima. Huna shabiki wako pale kwenye show ya wasafi afsa, hata iyo 500k ni kama sadaka maana hakuna shabiki atakayeenda tamashani kwa vile wewe upo jukwaani.
Andaeni show ya wakongwe, kwneye mazingira ya watu wazima, sisi wazee tutakuja kuwasupport kwa kutukumbusha enzi za ujana wetu