Chege ajibu madai ya Juma Nature kulipwa laki 5 tamasha la Wasafi

🀣🀣Mkuu unawadevalue wasanii wetu sasaπŸ€”
Si kwamba nawa devalue, huo ndiyo ukweli mchungu.

Wewe huoni Diamond anavyojilazimisha kwenda kimataifa anabumbabumba Kiingereza lakini anagangamala hivyo hivyo tu?

Wewe unafikiri Watanzania wana uchumi wa ku book shows za $40,000 mpaka $75,000 bila kusuasua kwa uchumi wetu huu?
 
Hapana
Ila with time tutafika
Si ndo branding yenyewe
Tupende vya kwetu
Honor starts at homeπŸ™
 
Makubaliano yao yalikuwa yapi?...kama ndio yalikuwa makubaliano yao haina shida
 
Anaongeza pesa ndiyo hiyo laki tano? Ambayo hata watoto wa Chuo hawakai nayo wiki mbili?
Msanii kama Nature?
Ungekuwa wewe ni Nature ungekubali laki 5?
 
Anaongeza pesa ndiyo hiyo laki tano? Ambayo hata watoto wa Chuo hawakai nayo wiki mbili?
Msanii kama Nature?
Ungekuwa wewe ni Nature ungekubali laki 5?
Maliza maswali yako yote nikujibu kwa pamoja, maana nimeshakujibu sasa unaamisha magoli, Kwahiyo orodhesha maswali yako yote nikujibu kwa pamoja.

Laki tano ni mshahara mkubwa tu Tanzania.
 
Hapana
Ila with time tutafika
Si ndo branding yenyewe
Tupende vya kwetu
Honor starts at homeπŸ™
Wewe mwenyewe unasema tupende vya kwetu ila umemalizia Kiingereza.

Inawezekana kabisa ukapenda vya kwenu na kuongea Kiingereza hapo hapo.

Hususan kama unataka kuwatangazia vya kwenu watu wanaojua Kiingereza ambao huwezi kuwapata bila kujua Kiingereza.
 
Hapana
Ila with time tutafika
Si ndo branding yenyewe
Tupende vya kwetu
Honor starts at homeπŸ™
Diamond akitaka milioni 100 kwa Show ya ndani ya Tanzania ni amejibrand, ila Juma Nature akikataa kupokea laki 5 (na kuomba alipwe labda milioni 10) inaonekana ujinga na sio tena kujibrand. Hatutaki tuwe na wasanii wengi type ya Diamond kimtonyo?
 
Ukweli ni kwamba, kizazi cha mashabiki wa Sir Nature kimeshavuka umri wa kwenda kwenye matamasha ya mziki ya viwanjani.

Kwa audience ya wasafi festival ya sasa ambao wengi ni vijana wa vyuo na under 25, jina la Juma nature ni historia, Juma hana mashabiki tena pale.

Sasa ni kizazi cha kina rayvanny na wenzake, japo wanaimba ujinga, ila ndo vitu vijana wa sasa wanataka kuvisikia. Hii imewatoa wakongwe wengi kwenye game. Akina jay mo, profesa, afande sele na kina juma.

Kutunza heshima, ni kustaafu muziki na kufanya shughuli nyingine kama anavyofanya solo thanks au Mr paul. Wamebaki na heshima yao kwa kuusoma mchezo mapema.

Juma ukitaka kuendelea kubaki valid kwa umri huu utapotea. Sasa watoto wanataka kukulipa 500k. Unaanza kulalamika wanakuvunjia heshima. Huna shabiki wako pale kwenye show ya wasafi afsa, hata iyo 500k ni kama sadaka maana hakuna shabiki atakayeenda tamashani kwa vile wewe upo jukwaani.

Andaeni show ya wakongwe, kwneye mazingira ya watu wazima, sisi wazee tutakuja kuwasupport kwa kutukumbusha enzi za ujana wetu
 
Watu wasiojua Kiingereza uchumi wao unaishia Sirari.

Yani hata interviews za radio stations za Nairobi na Kampala zinaweza kuwapa shida.

Weee huoni hata Harmonize anajiongeza?
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mkuu, je, ni yeye Juma Nature ndio anaomba kuwepo tamashani au wasafi ndio wanamwomba awepo? Ikiwa yeye ndio anaombwa, ni wazi anakuwa ndiye mwenye nafasi ya kupanga bei, ni wazi kuwa umuhimu wake unakua umeonwa na hao waandaji wa tamasha.

Solo Thang na sio Solo Thanks.
 
Akawaimbie wazee mgambo wanaruka na kukanyagana,hao migambo wenyewe wanawatesa mama zetu,dada zetu,bibi zetu huko masokoni.
 
Binafsi naona haya matamasha ni sehemu tu ya wasanii kurudisha kwa jamii. Sio sehemu ya kutajirikia. Mfano tamasha kama wasafi festival, wanacharge kiingilii cha 10,000 kwa kichwa. Wakioata wahudhuruaji 10,000 ni mil 100.

Kuna wasanii 20 wanaoperform. Kila mmoja ukimpa hata 3M ni 60m iyo. Hapo umebaki na 40m. Iyo ipangie maandalizi, promotion, jukwaa na speakers, malazi na usafiri.

Hakuna kinachobaki. Mwisho wa siku mtaanza kuita watu wanjonyaji.
 
Ndomana tamasha lina wadhamini Kama kumi na mbili, sasa hapo ukute wadhamini wameambiwa msanii atalipwa 5M akajalipwa hiyo 3M
 
Nature aheshimiwe kwa maamuzi yake,kila msanii ana price tag yake ya kuperform jukwaani,Hata Mondi alikosana na Ruge kisa maslahi.
Umeambiwa nature ana wimbo gani hot unaostahili alipwe 10m..?.

Hata hiyo laki Tano ni kubwa
 
Kama matamasha yangetegemea viingilio bhasi mziki mnene ya E-fm isingewezekana kufanyika nchi nzima pasipo kuwatoza watu viingilio

Pesa ipo kwa sponsors na kiingilio ni extra kwa hiyo usipigie tu hiyo pesa ya viingilio, lazma ujue main sponsor katoa bei gani
 
Niulize swali ambalo wengi pengine hawajauliza, utaratibu wa kuchaguliwa kwenda kuperform ukoje? Unashangaa tu jina lako limeshatokea kwenye vyombo vya habari bila consent yako au bila mazungumzo ya awali ama inakuwaje!??
Sio kwamba ilibidi kuwa na mazungumzo, kukubalina kiwango na muda wa kutumbuiza, sehemu utakazotumbuiza na kama bei ni hiyo hiyo ama la na kisha kusaini makubaliano kwa pande zote mbili?

Kama haya yalifanyika inakuwaje JN anaikataa hela kama kulikuwa na makubaliano hapo awali? Kama hakukuwa na makubaliano basi mambo ya Diamond Platinumz yanaendeshwa kienyeji sana na sidhani kama ana Mameneja wanaojitambua.
 
Umeambiwa nature ana wimbo gani hot unaostahili alipwe 10m..?.

Hata hiyo laki Tano ni kubwa
Nimeambiwa na nani? Wapi nimeambiwa hivyo?

Nani amesema kua anastahili alipwe 10M? Hayo maneno wewe umeyatoa wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…