Ni muda sasa umepita toka taarifa za kikosi cha kwanza cha Everton kutua Dar tayari kukipiga na Gor Mahiya kutoka Kenya kwenye Mechi ya kirafiki itakayofanyika kesho alhamisi tarehe 13/07/2017.
Mpaka sasa tayari kikosi hicho cha Everton kimeshatua jijini Dar na mchezaji mwenye mvuto zaidi ulimwenguni Wayne Rooney.
Kwa upande wake Gor Mahiya ya Kenya ilitua jana Jumanne. Ni mtanange ambao utakuwa wa aina yake utakaochezwa katika uwanja wa taifa wa Dar es Salaam.
Kuonyesha umuhimu wa ujio huu, waziri wa habari sanaa, utamaduni na michezo Dr Harison Mwakiembe amefika uwanja wa ndege JKNI kuwapokea Everton.
Wayne Rooney akisalimiana na Dr mwakiembe