Cheki Masanja anavyohaha, kweli kutunza mke si mchezo!

Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2016
Posts
8,658
Reaction score
15,793
Masanja huyu huyu aliyekuwa akiwacheka wenzake kuwa wamefulia, sijui wameloweka, hivi karibuni ameonekana 'akihaha' kutafuta pesa kwa udi na uvumba!

Huyu si ndo alikuwa anawachapa vijana viboko pale Jangwani ati kwa nini hawaoi? Unadhani kuoa ni swala la mchezo mchezo eeh? Sasa hivi vibiashara vya kupigia pesa 'unrealistically' vinaonesha zaidi kuwa akaunti ya Masanja imesinyaaa na huenda akafulia na kuuza Bima siku si nyingi 😀😀😀.

Embu ona hapa amelala na mke wake sijui ndio wameshauriana waje na hiki kiseminia? Eti semina juu ya kutunza pesa, tangu lini Masanja akawa na elimu ya kutosha ya mambo ya Finance kiasi cha kuwakalisha watu semina na kuwalipisha laki? Si bora tumchukue prof Lipumba aje atoe semina kama hiii?
Kweli maisha ni safari ndefu, unaweza ukawacheka wenzako kwa vile hujui ya kesho.

Masanja.jpg
 
Mkuu Kodofan mi naona kama anajoke hapo na kusema kuwa kama unalipishwa pesa kwenda kwenye semina ya jinsi ya kutengeneza pesa basi uwe na akili usiende. Wapi ametangaza semina, au umeamua kumchamba tu masanja leo?
 
masanja 2.jpg
We ni ki.l.a.za , amepost kama jokes huko Twitter, hujui hata jokes
Mkuu Kodofan mi naona kama anajoke hapo na kusema kuwa kama unalipishwa pesa kwenda kwenye semina ya jinsi ya kutengeneza pesa basi uwe na akili usiende. Wapi ametangaza semina, au umeamua kumchamba tu masanja leo?
Wala sio jockes, deep down anapima upepo. Akiona watu wengi wanamshobokea ndio analeta semina, ila akiona watu hawamshobokei ndio anajifanya eti ilikuwa jockes...
Si unakumbuka alifungua kakibanda ka kuuza ubwabwa kule Tabata afu kakabuma? Sasa kukafunga anaona aibu na kukaendeleza anaona hasara. Kabaki njia panda.
Magufuli keshasema wapiga dili wote kwishney....
 
Masanja anatania tu, mwe! hamtaniwi!!! ndio maana mtu akitania kuwa "mfayatue watoto kwa kuwa shule ni bure" na nyie kweli mnaenda kujipinda kutengeneza watoto
 
Masanja huyu huyu aliyekuwa akiwacheka wenzake kuwa wamefulia, sijui wameloweka, hivi karibuni ameonekana 'akihaha' kutafuta pesa kwa udi na uvumba!

Huyu si ndo alikuwa anawachapa vijana viboko pale Jangwani ati kwa nini hawaoi? Unadhani kuoa ni swala la mchezo mchezo eeh? Sasa hivi vibiashara vya kupigia pesa 'unrealistically' vinaonesha zaidi kuwa akaunti ya Masanja imesinyaaa na huenda akafulia na kuuza Bima siku si nyingi 😀😀😀.

Embu ona hapa amelala na mke wake sijui ndio wameshauriana waje na hiki kiseminia? Eti semina juu ya kutunza pesa, tangu lini Masanja akawa na elimu ya kutosha ya mambo ya Finance kiasi cha kuwakalisha watu semina na kuwalipisha laki? Si bora tumchukue prof Lipumba aje atoe semina kama hiii?
Kweli maisha ni safari ndefu, unaweza ukawacheka wenzako kwa vile hujui ya kesho.

View attachment 430837
Mkuu ni hivi Masanja anawaponda wale wanaotoa semina za kutunza pesa. Kwenye semina kama hizo unaambiwa uchangie 100,000 au 500,000......sasa somo zuri na la kwanza kuhusu kutunza pesa ni USIENDE KWENYE HIO SEMINA KWANI USIPOENDA UTAKUWA UMETUNZA HIO 100,000 au 500,000! Na si kwamba Masanja anatoa hayo mafunzo.
 
Back
Top Bottom