Nimekaa chini nimepiga hesabu kutoka tar 20May mpaka Leo tar 16 June, wastani WA mwezi huo (28days), nimejikuta nimetumia kiasi Cha shilingi za kitanzania 70000, Kwa ajiri ya bundles hasa internet dakika ni kidogo sana.
Nimejilaumu sana sana Kwa sababu hata iyo internet niliyokuwa natumia ilikuwa sio Kwa ajiri ya kuzalisha Bali ni burudani tu, kama vile Instagram na tiktok Hawa ndo main eater wa bundles zangu.
Hivyo imenilazimu kupanga na kujipanga upya kuanzia Leo tar 16 June had 16/07, nimeadhimia!
1.Niwe angalau nimetumia kiasi Cha TSH 8000 tu Kwa ajiri bundle za internet na dakika
2.kufuta social network zote kama Instagram, TikTok na Facebook ( hili limefanikimiwa mana nimeshafuta tayari )
3. Kutumia mb zangu Kwa uangalifu zaidi, hasa kuepuka kuangalia video na picha
4. Kutunza mb nitadili zaid na kuangalia au kutafuta vitu zaidi vinavoletwa au kupostiwa Kwa maandishi kama humu Jamii forum, au searching kule chrome.
5. Kutodownload kitu chochote kinachozidi mb 50.
USHAURI
Tusipokuwa makini smartphone zinatutia umaskini bila kuelewa na hivi saizi Kasi ya internet ni kubwa kama yote, mb dakika sifuri zimeisha.
Alafu smartphone hasa internet sio nzuri sana Kwa sisi watafutaji pesa na muda zinatukomba saaaaana[emoji17][emoji45][emoji17][emoji45]