Machame Juu
JF-Expert Member
- Jul 25, 2013
- 1,514
- 3,363
Tangu Chelsea inunuliwe kutoka kwa billionare Roman Abrahamovich chini ya mwaka imeshafukuza makocha watatu Frank Lampard, Thomas Tuchel na sasa Graham Potter kabla ya mikataba yao kuisha na kuwalipa fidia ya mamilion ya pounds.
Na kabla ya hapo walishawafukuza makocha wengine kabla ya mikataba yao kuisha Jose Mourinho, Antonio Konte na Mauricio Petechinno, Thomas Tuchel, Steve Holland, Guus Hiddink, Sarri na kuwalipa mamilion ya fidia.
Huyu Graham Potter wa karibuni kufukuzwa na Chelsea alipewa kitita cha paundi million 27 yeye na team yake ya ukocha alipokuwa anaifundisha Brighton ambayo aliiacha na inafanya vizuri. Pia akasaini mkataba wa miaka mitano ya paundi million 50 ambazo atafidiwa baada ya Chelsea kuvunja mkataba wake na kumfuza.
Miezi sita iliyopita Graham Potter hakuwa millionare lakini sasa hivi ni millionaire.
Chelsea inachezea sana pesa.