Haujui jinsi ya kutafsiri takwimu za mpira, hasa kuhusu ball possession! Kuna kitu kinaitwa "Football efficience" yaani ni kwa kiwango gani jitihada iliyotumika ilifanikiwa kufikia malengo yaliyokusudiwa. Kwenye mpira wa miguu lengo kuu ni kufunga goli na mwishoni kuweza kupata pointi Tatu muhimu. Na jitihada inayotumika ili kufikia lengo Hilo ni kutafuta nafasi na kupiga mpira golini (Shots on target). Kanuni yenyewe ni hii: football efficiency= Goals /(divide by) Shots on target *(times) 100. Kwa chelsea: Football efficiency=1/2=50%. kwa Man U : Football efficieny=0/2=0%.
Kwa hiyo Football Efficiency Chelsea 50% Man u 0%. Hii ni kwa sababu timu zote mbili zilipiga mashuti mawili golini (shots on target), lakini kwa Man jitihada hizo zilizaa goli sifuri (0), na kwa chelsea jitihada hizo zilizaa goli moja(1). Ndiyo maana mwisho wa siku inajulikana timu ipi ilinuna na ipi ilicheka! Kucheza mpira wa miguu kwa juhudi kubwa bila kufunga goli ni sawa na kuwalisha kuku wa mayai kwa juhudi kubwa lakini wasitage yai hata moja. Halafu mfugaji wa jinsi hiyo akijisifu kuwa ni mtaalam wa kuwalisha kuku akiambiwa akapime akili atakuwa amesaidiwa sana!