Da Dona
JF-Expert Member
- Dec 16, 2025
- 1,220
- 672
Klabu ya Chelsea FC imemfuta kazi kocha wake mkuu, Liam Rosenior, kufuatia mwenendo mbaya wa matokeo ndani ya klabu hiyo.
Uamuzi huo umechukuliwa leo Jumatano Aprili 22, 2026 baada ya Chelsea kupoteza michezo mitano mfululizo ya ligi bila kufunga hata bao moja, hali iliyozua shinikizo kubwa kutoka kwa mashabiki.
Rosenior anaondoka darajani hapo baada ya kudumu kwa chini ya miezi minne tangu alipoteuliwa kuchukua mikoba ya Enzo Maresca, licha ya kusaini mkataba wa miaka sita na nusu.
Kwa wale ambao labda wamepitwa na dondoo za EPL, Rosenior alipewa timu mwezi Januari akirithi mikoba ya Enzo Maresca. Lakini kibarua kimemshinda baada ya kuandikisha rekodi mbaya ya vipigo vitano (5) mfululizo bila timu kufunga bao hata moja! Kichapo dhidi ya Brighton ndicho kimekuwa msumari wa mwisho kwenye jeneza lake, huku ripoti zikidai kocha huyo aliwashambulia wachezaji wake hadharani akihoji kiwango chao cha kujituma na upambanaji.
Nani anashika usukani kwa sasa?
Uongozi umemteua Calum McFarlane, aliyekuwa kocha wa kikosi cha vijana (Under-21s), kukaimu nafasi hiyo mpaka mwisho wa msimu. McFarlane anaingia na kibarua kigumu mbele yake, akianza na mchezo dhidi ya Leeds United kwenye michuano ya FA Cup. Hii ni mara ya pili kwa McFarlane kukaimu msimu huu; katika mechi zake mbili za awali aliambulia sare dhidi ya Manchester City na kupoteza mbele ya majirani zao Fulham.
Kwenye taarifa yao rasmi, Chelsea imemshukuru Rosenior kwa weledi wake lakini imeweka wazi kuwa matokeo na viwango vya timu vimekuwa chini ya matarajio ya klabu huku kukiwa bado na malengo ya kupigania msimu huu (kama kufuzu michuano ya Ulaya na kusonga mbele FA Cup).
Taarifa zinadai kuwa kwa sasa, uongozi utachukua muda "kujitathmini" (self-reflection) badala ya kufanya maamuzi ya haraka ya kutafuta kocha mpya wa kudumu.
Kulingana na mwendo wao tangu Todd Boehly aichukue timu, tatizo la Chelsea ni makocha au sera za uongozi?
Je, wachezaji wa sasa wa Chelsea wana hadhi ya kuipambania nembo ya klabu au Rosenior alikuwa sahihi kuwalaumu kwa kukosa kujituma?
Unadhani ni kocha gani wa daraja la dunia anayewafaa The Blues msimu ujao?