A
Anonymous
Guest
Katika mtaa wa Sikukuu, hali ya mazingira imeendelea kuwa mbaya kufuatia chemba za maji machafu kujaa na kutema maji yenye uchafu kama inavyoonekana kwenye picha hapa, hali iliyosababisha maji hayo kuingia barabarani na maeneo ya kufanyia biashara. Maji hayo yamechanganyika na taka zilizokuwa zimekusanywa ovyo njiani, na kuufanya mtaa uonekane mchafu kupita kiasi huku ukitoa harufu kali isiyovumilika.
Na viongozi wetu wanazidi kupongezana tu kama hawayoni haya, wakazi wa eneo hili, wanalazimika kupita katikati ya maji machafu na ukitazama ni kama mvua imenyesha hivi lakini hata hakuna mvua. Hivi viambatanisho hapa ni vya leo 7 Januari 2026, bila hata mvua kunyesha na viongozi wetu utawaskia hawana taarifa juu ya hili jambo as if wao hawaishi hapa na utadhani hawapelekewi hizi kero. Any way nilikuwa napita tu, hii ndio Tanzania bhana
Pia soma ~ Rais Samia: Wasimamizi wa soko la Karikoo zingatieni miundombinu ya majitaka na usafi