Juzi niliandika hapa JF taarifa kuhusu maji taka yaliyokuwa yakitiririka eneo la Posta barabara inayotokea Kanisa la KKKT kuelekea Karimjee ambayo yalikuwa yanatoka katika chemba zilizokuwa zimefumuka.
Inadaiwa kuna maafisa wa Mamlaka ya Serikali wamefika na kutengeneza miundombinu iliyokuwa ikitiririsha maji taka hayo na kutusababishia kero sisi tunaotumia njia hiyo.
Napongeza ujumbe huo kufanyiwa kazi na ninatoa wito mamlaka ziendelee kuboresha miundombinu ya maji taka hasa chemba ambazo zimekuwa zikitoa maji machafu hasa kipindi cha mvua ili kuwaepusha wananchi na magonjwa pamoja na kero ya harufu mbaya.