Chemsha bongo: Shilingi 100 iko wapi?

Chemsha bongo: Shilingi 100 iko wapi?

Nidadavue kwanza.

Tuassume ulikopa 4900 kwa kila mmoja ambayo jumla ni 9800, Nguo ulinunua 9700, ukabaki na 100.

Kama ulikopa 10000, ukitoa 9800
[ambayo ni 9700(bei ya Nguo) + 100 ( kiasi kilichobaki) ]
Utapata 200 ambayo ni kiasi ulichowalipa kama ulikopa 10000.

JIBU: 100 ipi unayoitaika? Maana zote zimeisha. Usije ukadhani umeibiwa.[emoji38] [emoji38]
 
Kuna shs 50 ya dada na shs 50 ya kaka hukuijumlisha hapo.

MAELEZO:
Kama nguo imeuzwa 9700 tafsiri yake dada amechangia 4,850 na kaka 4,850.

Ukimpa dada 100 itakuwa 4,950 na ukimpa kaka 100 itakuwa 4,950.

dada 4,950 + kaka 4,950 = 9,900

9,900 ukiongeza 100 uliyobaki nayo unapata 10,000
 
Asa hapo hao dada na kaka ni wajinga watakubalije kulipwa mia katika helufu tano???... Ndo hapo walipokosea
 
Hiyo ni miamala miwili tofauti. Kaka na Dada walikukopesha jumla ya sh. 10,000 umewalipa Sh. 200 bado wanakudai sh. 9,800 jumla sh. 10,000. Kwa upande wa pili ulienda dukani na sh. 10,000 ukanunua nguo sh. 9,700 ukabakiwa na sh. 300 jumls sh. 10,000. Hakuna hata sent I iliyopotea. Hiyo sh
100 inaonekana kupotea kutoka na mantiki potofu ya kuchanganya machungwa na maembe.
 
Ngoja nijibu hili swali

Baada ya kulipa 200 na kubaki deni la 9800, hiyo 100 iliyobaki ni positive (+) na 9800 ni negative (-) kwakuwa ni deni, hivyo ukizijumlisha hubaki 9700 na sio 9900.

Umeelewa
 
We chizi kweli tangia lini mkopo ikajumlishwa na pesa iliyomkononi. Matumizi ndo yanaweza jumlishwa na pesa iliyo mkononi ili ujue kabla ya matumizi ulikuwa na kiasi gani. Mfano ukichukua 100 iliyobaki ukijumlisha na 9700 uliyotumia utapata 9800 uliyo
kopeshwa
Jamaa katoa chemsha bongo,katika waliojibu ndugu yangu nimekuelewa maana hata mimi jibu lilinizonga kwamba hakutakiwa kujumlisha pesa ya mkononi na deni bali ile 100 alitakiwa ajumlishe na pesa aliyonunulia shati..

Nimepata mwanga wa jibu kutoka kwako kwani 100 anayo yeye mwenyewe..
 
Eleza hiyo 100 imeenda wapi!
View attachment 445142
Umemlipa dada na kaka (tsh) 100 kila mmoja. Deni lililobaki kwenye (tsh) 10,000 uliyokopa kabla ni (tsh) 9,800. (Tsh) 100 uliyonayo mkononi imepatikana kwnye punguzo la bei ya nguo.

Hivyo, (tsh) 100 ni deni pia ambalo hujalipa kwasababu ulikua huna hela yoyote. Kama dada na kaka wanakudai (tsh) 9,800 - (tsh)100 salio la deni linakua (tsh) 9700 ambapo (tsh) 300 iliyopungua ni punguzo la bei.

Angalizo: (tsh) 100 inaonekana kupotea kwasababu unamtizamo kuwa ni faida kwako mathalani haukua na hela yoyote mwazo. Hivyo (tsh) 100 uliyonayo mkononi ni deni pia haitakiwi kuiongeza kwnye (tsh) 9,800 bali kuitoa na salio la deni kubaki (tsh) 9,700
 
Back
Top Bottom