Chenga ya mwili: Walininukuu vibaya, sikusema nyongeza ni asilimia 23.3 kwa kima cha chini bali nyongeza ni sh 23,300/= kwa kima cha chini!

Chenga ya mwili: Walininukuu vibaya, sikusema nyongeza ni asilimia 23.3 kwa kima cha chini bali nyongeza ni sh 23,300/= kwa kima cha chini!

Haya ndo madhara ya kuwa na mbumbumbu wengi Bungeni, tuliendekeza ushabiki tukaacha kuwapa Wapinzani Ubunge sasa tunajionea nchi inapelekwa jinsi majizi yanavyotaka, 2025 Watanzania tuamke,tuwachague Wabunge radical ili watusemee mjengoni



Ni kweli mambo mengi hawaja raise any concern wamepigwa ha Kama yalivyo sasa kwenye utekelezaji inakuja kuwa surprise kwa wananchi kama hili la tozo za miamala ya kuchukua hela bank [emoji24][emoji24]

Umenena vema ni kweli kuchagua wabunge ambao wanaenda bungeni kama vacation/holiday ni shida!

Hawaendi kusoma makarabrasha, wao ni kupitisha kila kitu.

Lakini Magufuli ndivyo alitaka !
 
Huyu mama naona ameamua awe tu Kama jiwe ,hizi ni dharau kwa watumishi wa umma ni heri asingahidi kitu ile siku na tulishazoea kwa miaka km 6 ,Sasa inawezekana vipi unakaa kabisa unamwongeza mtu 20k kweli ?

Mama kuwa makini na washauri wako hasa huyo mwigulu najua anachokifanya kina maana yake na faida kwake ,utakuja kuelewa baadae Sana ukishazamishwa shimoni
 
Uchumi wa dunia umekumbwa na changamoto za UVIKO na vita vya Ukraine Mambo ambayo yameathiri uchumi wa Tanzania pia. Ongezeko la mshahara bila kuzingatia Hali ya halisi ya Uchumi kwa Sasa na kutazamia Hali ya baadae ni kosa ambalo linaweza kugharimu uchumi zaidi kuliko hata athari za UVIKO.

Binafsi naona ongezeko hili ni kwa ajili ya kutazamia hali ya uchumi kwa baadae na kama Hali itakuwa shwari naamini ongezeko halisi ya Hali halisi litakuja kuanzia mwaka ujao wa fedha
 
Duh sasa hii ni zaidi ya madharau, lakini kama kawaida yenu mtawapigia kura tuu hao hao, na wameongeza mikodi kwenye transactions itakayokula zaidi ya hizo 23,000 kwa mwezi, msiogope mabadiliko wafanyakazi wapeni wapinzani hata nusu ya viti vya ubunge hawa CCM ni wehu tuu na wana akili za kimaskini sana
2025 ipo wazi wapinzani watapata viti vingi Sana Bungeni,kama unataka kuingia bungeni kula kodi zetu anza mdogo mdogo kampeni ujenge jina kupitia upinzani.
 
Huyu mama naona ameamua awe tu Kama jiwe ,hizi ni dharau kwa watumishi wa umma ni heri asingahidi kitu ile siku na tulishazoea kwa miaka km 6 ,Sasa inawezekana vipi unakaa kabisa unamwongeza mtu 20k kweli ?

Mama kuwa makini na washauri wako hasa huyo mwigulu najua anachokifanya kina maana yake na faida kwake ,utakuja kuelewa baadae Sana ukishazamishwa shimoni
Alishaambiwa Sana kuhusu huyu msingida ndie kikulacho chake asikii.Asubirie matende
 
Mwigulu ni tatizo.
Hakuna kitu ana agizwa na Mh. Rais halafu aka fanya kama alivyo agizwa. Kumbukeni haya machache,
Tozo kwenye miamala ya simu.
Ruzuku kwenye mafuta ya magari
Gharama kwenyemafuta ya chakula. Na sasa mishahara.
Lengo la huyu rais wa mawe ni kumgombanisha Mh Rais na wananchi.
Kuna hitajika badiliko wizara ya fedha asap
Huyu waziri serikali ni ni tatizo wao wanampa uwaziri lakini Sii mzuri msimwone akivaa bendera kama mzalendo hypocrite
 
Kama nyongeza kwa kima cha chini ni sh 23,300/= maana yake nyongeza inapungua kwa kadri mshahara unavyokuwa mkubwa hadi nyongeza inakuwa chini ya sh 10,000/=. Na ndivyo watumishi mlivyopata kwenye mishahara yenu! Bila shaka sasa nimeeleweka!
.
FB_IMG_1658554812119.jpg
 
Acha kuandika ujinga kama huu.Mbona Mwendazake mlikuwa mnahusisha Kwa mabaya yote yaliyokuwa yaliyokuwa yakitokea hapa nchi.Hakika CHADEMA NI SHIDA KUBWA HAPA. NCHI
Hawa ni wapumbavu mkuu!

Kwa magu wakikuwa wanasema eti hataki ushauri, ila kwa huyu wanasema eti anashauriwa vibaya
 
Watu wengi hawajui Hili Mwigulu ni waziri wa fedha ambae ndie huumiza Watanzania ...mtu akijua hili hawez kumpenda huyo jamaa
Sidhani kama Mwigulu anaweza kufanya mambo nyeti kama haya ya mishahara peke yake. Yeye anawajibika kama waziri mwenye dhamana lakini nadhani baraza la mawaziri linajua mambo yote yalivyokwenda.
 
Wanaoandika humu ni wajinga wasio na kazi serikalini. Tumeridhika kwanza ametimiza ahadi ya kuongeza hata kama ni kidogo. Tulikaa miaka 7 bila hata ahadi.
Asante Mama tuna imani kikubwa kitakuja. MaCHADEMA kakimbieni barabarani.
Kwa hiyo unafurahia kuongozewa kodi na kudanganywa umeongezewa mshahara, inaonekana hata fisi wa ukweli kakuzidi akili
 
Hakuna kiongozi anayeongeza kodi kipindi cha kuelekea uchaguzi, Mwigulu ana nia mbaya na huyu mama, mama akishtuka Mwigulu itabidi arudi kijijini alipotoka
 
Sijui ni kwanini kuna mtafaruku huu. Miaka yote kinachotangazwa kama nyongeza huwa ni kima cha chini cha mshahara. Haijawahitokea waseme mishahara itaongezwa kwa asilimia fulani, bali husemwa kima cha chin kitaongezwa kwa asilimia kadhaa na kadiri unavypanda juu asilimia hushuka. Hauwezi kua sawa iongezwe asilimia 23 kwa wote kwani utakuta mtu mwenye m2 kwa mfano atapata hela nyingi sana na wa laki tatu atapata kidogo sana kitu ambacho kitaleta manung'uniko tena. Yatubidi wafanyakazi kuyaelewa matamko haya ya nyongeza za mishahara tangu mwanzo ili tusiwe na matumaini hewa na kukata tamaa uhalisia unapojitokeza. Serikali nayo iwe inatoa mapema circular ya mishahara kabla ya kutoa mishahara baada ya maboresho husika. Ukiweka sawa sawia kwa asilimia hii mwenye mshahara wa m10 atapata nyongeza ya 2,330,000 wakati mwenye laki tatu atapata 69,900 tu. Hii pia ingeleta malalamiko na mzigo mkubwa kwa serikali.
 
Maumivu ya chenga ya mwili kuhusu nyongeza ya mishahara mdogo mdogo yanaishia na maisha yataendelea!! Kila upande ujipange kiungwana kuongea!
 
Matarajio yalikuwa ni makubwa hasa kwa wenye mikopo ya mabenki kuwa angalau ka-teki homu kataongezeka lakini hola! inaumiza sana!
 
Ila kikubwa Mungu yupo!! Biblia inasema "msihangaikie mtakula nini wala mtavaa nini. Wangalieni ndege wa angani kuwa hawalimi wala hawakusanyi ghalani, lakini baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Je nyie si bora zaidi kuliko hao?"
 
Yaliyopita si ndwele tugange yajayo! Biblia inasema "mtu haishi kwa mkate tu, bali kwa kila neno litokalo kwa Mungu". Kwa muktadha huu "Mtu haishi kwa mshahara tu baki kwa kila Neno litokalo kwa Mungu" Watumishi wa umma jipeni moyo, Mungu atawalinda na hatawapungukia!
 
Back
Top Bottom