Chenge ashikiliwa polisi kwa ajali ya gari iliyosababisha vifo

inavyosemekana ni kuwa Chenge na marehemu vicky walikuwa ni marafiki wa muda mrefu.

ila siku ile ya tukio,walikuwa wakipata kinywaji pamoja akiwa na rafiki yake huyo waliepata ajali pamoja. ilipokuwa inakaribia hiyo saa kumi alfajiri walikorofishana chenge na huyo vicky,ndipo wakaamua kuchukua kibajaj waondoke zao kwa hasira. huyu bwana aliporudi akaambiwa jamaa wameshaondoka na kibajaj,ndipo akaamua kuwafukuza alipkuwa karibu kukifikia akajaribu kubloc kwa mbele ndipo ajali ikatokea.

Kwa hiyo habari ndiyo hiyo,mama nae kule mwanza kathibitisha mahusiano ya chenge na binti yake huyo kwa hiyo wasitupige changa la macho.!!!!!!
 

Hizi taarifa sasa zinaleta mkanganyiko mkubwa sana.......there must be something behind the scene!
 
Sasa na yule Bwana Constantine kaka wa marehemu Beatrice kwa nini alisema uwongo au why Beatrice alimwambia kaka yake kuwa rafiki yake huyo Vicky anakwenda Zanzibar kuolewa? Wakati mama wa marehemu anakana hakuna harusi? Nini kinaendelea jamani?
 

walikuwa wakinywa baa gani au hoteli gani???
 
Huo ndo utaratibu wa Bongo! Hizo sticker nimezinunua sana, na sijawahi kufanyiwa ukaguzi wowote, na sikutoa rushwa.
Hizo sticker ni njia ya kukusanya pesa tu hakuna lingine lolote.
Mheshimiwa Kang,

Kuzinunua hizo sticker bila ukaguzi ndio Rushwa yenyewe, Wewe unazinunua 5000 kukwepa kupeleka gari kukaguliwa, ungepeleka gari ungelipa 3000TShs, Hata kama ni mradi wa kukusanya pesa lakini ndio sheria, haijali kama ni mbaya au nzuri, Msheshimiwa na wewe ni miongoni wa watoa rushwa, ili kutokomeza rushwa inabidi kila mtu atimize wajibu wake.

Regards
Kipa
 
kuna jamaa alisema kwamba eneo la ajali hakukuwa na DAMU je kuna ukweli wowote? hii inaweza kuwa clue muhimu.

Ajali hii inaleta shaka kutokana na ukweli kuwa
1. Wahusika wa ajali wanafahamiana sana (Chenge na Vick)
2. Dereva wa bajaj hajapatikana
3. Mmiliki wa bajaj hajajitokeza licha ya kutakiwa na polisi tena kwa kutajwa jina (Zuwena)
4. Wahusika wote inaonekana walitoka eneo moja yaani bar au casino/kwenye ulevi
 
Msheshimiwa Mwiba,

Kweli Wadanganyika tuna safari ndefu, haya ngoja nijaribu na mimi kukuelimisha

Insurance ( Bima ) ndio iliyokwisha 2007 Zanzibar insurance company ni shirika mama la bima lilosajiliwa kwa ajili ya kutoa bima mbalimbali ikiwemo ya magari, shirika hili lina mawakala wako wanoliwakilisha, ukiangalia hiyo sticker iliyokwisha 2007 kwenye maandishi ya juu yaliyozunguka nusu duara utaona Zanzibar insurance.... na katikati ya hiyo sticker utaona jina la wakala wa zanziba insurance.Valididty yake ni mwaka mmoja

Road License ( ni leseni ya barabarani ) kwa kifupi ni ruhusa ya gari kutembea barabarani hii hulipiwa TRA ndio inayoonekana inaisha 2009 hapo kwenye sticker. Validity yake ni mwaka mmoja kama ilivyo bima

Tofauti zake: Wakati leseni ya barabarani inaruhusu gari kutembea barabarani lakini haiwezi kulipia fidia ikitokea ajali kazi ya fidia ni ya bima, zote hizi zinakuwa na details kama vile aina ya gari engine na chasis no tarehe ilipotengenezwa jina na anuani za mmiliki nguvu ya injini, BIMA inakwenda zaidi na kutaja thamani ya gari, Kwajili details hizi ni nyingi haziwezi kukaa zote kwenye sticker inayobandikwa kwenye gari basi hupewa karatasi nyingine yanye vitu hivyo hizo sticker zinakuwa na summary tu.

Kwa mtaji huu WEWE NDIO ULIEDANDIA TRENI MBELE HUKU LIKIWA KWENYE MWENDO KASI ANGALIA UTAGONGWA.

Salaaam
Kipa
 


.......The Plot Thickens.....!
 

asante sana
 
Jamani hebu waandishi/familia idai kuona taarifa ya posmoterm.
Je, kifo kimesababishwa na ajali ya gari la Chenge, au kitu/gari lingine?
Je, dereva wa bajaji alikuwapo na aliumia na kuchukuliwa na polisi????
Je, gari alilosema Chenge lililokuwa nyuma yao ni la nani? Lilifanya nini?
Chenge alikuwa na kiongozi mwingine wa CCM toka kanda ya ziwa, walitoka wapi?
Bajaji haikugongana na gari la Chenge, iligongwa kwa nyuma, walikuwa wakifukuzana?
Wanafahamina, kwanini wengine walipanda bajaji, au waligombana?
 

...mungu wangu, kesi inazidi kuongezeka wigo. Wanaume wawili, wanawake wawili, walikuwa wanakunywa pamoja;

wanawake 'wakawatoroka' kwa kutumia usafiri wa Bajaj, wanaume wakawakimbiza kwa hilo Toyota,... Ajali, ...

au;

Walishauwawa kitambo, halafu hiyo bajaji ikaegeshwa hapo na miili (maiti) kisha Toyota ikaja igonga?

WHY? kwanini?
 

MImi ningekuwa ndo chenge nisingeongea neno hata limoja maana GIVING REASONS IS A VERY BIG WEAKNESS CHENGE...YOU ARE JUST TOO MUCH!!!!
 

Haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa yani kumbe hapa ni eneo la ajali na chenge anachekelea hivi???
 

Mkuu wangu Halisi,

Mbona makubwa hayo tena? Waligombana na kuanza kufukuzana?

Umri kama wa Chenge, saa 10 usiku bado anavinjari viwanja mjini?

Hawa wabunge wanakuwa majimboni kwao saa ngapi?
 
Habari zinasema leo angepelekwa mahakamani, jee hilo limefanyika? au anasubiriwa yule mwanasheria wake wa Marekani/Uingereza? Tupasheni habari mlio nazo
 
Habari zinasema leo angepelekwa mahakamani, jee hilo limefanyika? au anasubiriwa yule mwanasheria wake wa Marekani/Uingereza? Tupasheni habari mlio nazo

Amepelekwa mahamani kwa mbwembwe na waandishi wengi walizuiwa kuingia mahakamani. Na tayari amepata dhamana kiulaini kabisa. Anakwenda kulala home kwake. Alifika kwa gari la polisi hyundai na kuingia moja kwa moja kizimbani na hakimu akaingia saa hiyo hiyo kama walipanga muda na mchezo ukaisha.

Upelelezi haujakamilika!
 

Chenge amesomewa mashtaka matatu likiwepo la kusababisha vifo vya watu wawili.

Ni kwa Hakimu Mkuu Mkazi wa Wilaya ya Kinondoni Emirius Mchaura.
Mwendesha Mashtaka Mrakibu Msaidizi wa Polisi David Mafimbo.
Chenge anadaiwa kufanya makosa hayo Machi 27 mwaka huu majira ya 10:30 alfajiri katika barabara ya Haile Selasie, karume eneo la Osterbay, Kinondoni.

Mafimbo:
Katika shitaka la kwanza Chenge unashitakiwa kwa kusababisha kifo kupitia uendeshaji wa kizembe katika barabara ya umma, na maelezo ya kosa ni kwamba ukiwaunaendesha gari yenye Namba T. 513 ACE Toyota Hilux Double Cabin uliendesha gari hiyo kizembe na kushindwa kuchukuwa tahadhari kama inavyotakiwa huku ukiendesha upande wa kulia zaidi uliigonga Bajaji yenye namba T 736 AXC, kweli au si kweli?.

Chenge: Si kweli.

Mafimbo: Katika shitaka la pili, Chenge unashitakiwa kwa kusababisha vifo vya watu wawili, na maelezo ya kosa ni kwamba mnamo Machi 27 mwaka huu majira ya 10:30 alfajiri katika barabara ya Haile Selasie, karume Osterbay wilaya ya Kinondoni ukiendesha gari bila kuchukuwa taadhari uliigonga Bajaji na kusababisha vifo vya watu wawili Victoria Gorge na Beatrice Constantini, kweli au si kweli?

Chenge: Si kweli.

Mafimbo : Shitaka la Tatu ni kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha uharibifu wa bajaji, jibu kweli au si kweli?

Chenge: Si kweli.
Baada ya Chenge kukana mashtaka yake yote ASP Mafimbo alimweleza Hakimu Mchauru kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Hakimu Mchauru aliweka wazi masharti ya dhamana ambapo alimweleza mshtakiwa kuwa anatakiwa kusaini hati ya dhamana ya milioni 1/- NA kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini hati ya dhamana ya milioni 1/-.

Chenge alikamilisha masharti hayo ya dhamana aliyotakiwa kuyatekeleza na kesi imeahirishwa hadi 30 April mwaka huu.

Kesi iifanyika chumba kidogo cha mahamama alichukuwa takribani dakika 10 hadi 15 tangu Chenge alipowasili mahakamani hapo, ambapo alifika na kupitiliza moja kwa moja kwenye chemba na hakimu kuanza kuendesha kesi huku waandishi wa habari wakisikiliza kesi wakiwa nje ya chumba kutokana na chumba hicho kuwa na nafasi ndogo isiyotoshereza watu wengi kuingia.

Nje ya mahakama ndugu wa Chenge walisikika wakiwasema vibaya waandishi wa habari waliokuwa wakifuatilia kesi hiyo na kutaka kuwazuia wasimpige picha Chenge.

“Hivi mnazani kwakumpigapicha ndugu yetu mtaondokana na umaskini? Kama mnadhani mtatajirika kutokana na kesi hii ya leo basi tutaona kama mtaondokana na umaskini,” alisikika mmoja wa ndugu wa Chenge akiwaambia waandishi wa habari.

Umati wa watu ulifurika katika mahakama hiyo waliofika ili kumshuhudia Kiongozi huyo wa serikali akifikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashitaka yake.

Chenge alifikishwa mahakamani hapo majira ya saa 6 mchana akiwa kwenye gari ya polisi na baada ya kuachiwa kwa dhamana aliondoka na gari binafsi yenye namba T ASP 362.
 
chenge kamgonga huyo mwanamke kwa makusudi ili amuue
MASWALI YA KUJIULIZA
1.chenge kila akienda mwanza hotel anapiga simu huyo muhudumu aje kumuhudumia hata kama ni usiku wa manane/hata kama yuko off.( maana yake ni uhusiano wa kimapenzi) je humu ndani wana JF ambao mmeajiriwa sehemu siyo mali yenu mnaweza mkafanya kwa mteja kiasi hicho?
2. huyo mfanyakazi bora mwanza hoteli( vicky marehemu) anakunywa baa moja na chenge usiku wa manane (huo ni uhusiano)
3. kwa wanaume wa JF, mwanamke ametoka Z'bar kununua vifaa vya saloon. Je hivi vifaa vya saloon sio chenge ndio amevinunua??? huyo mwanamke kwa kazi yake ya mwanza hoteli asingeweza kwenda Z'bar kununua vifaa vya saloon alafu awe anakula maisha usiku wa manane maana yake angemaliza mtaji wote wa saloon? Ni jambo la kawaida kwa wanaume tanzania kuwafungulia wanawake saloon, botique na vinginevyo.
4. Chenge kila siku akienda mwanza anampigia huyo mwanamke simu aje kumuhudumia, iweje ashindwe kumpa lift usiku ule? iweje ashindwe kumkodia tax ya maana usiku ule mpaka mwanamke kakimbilia cheap option bajaji? jibu UGOMVI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…