Amepelekwa mahamani kwa mbwembwe na waandishi wengi walizuiwa kuingia mahakamani. Na tayari amepata dhamana kiulaini kabisa. Anakwenda kulala home kwake. A.lifika kwa gari la polisi hyundai na kuingia moja kwa moja kizimbani na hakimu akaingia saa hiyo hiyo kama walipanga muda na mchezo ukaisha. Upelelezi haujakamilika!!!!!
Chenge amesomewa mashtaka matatu likiwepo la kusababisha vifo vya watu wawili.
Ni kwa Hakimu Mkuu Mkazi wa Wilaya ya Kinondoni Emirius Mchaura.
Mwendesha Mashtaka Mrakibu Msaidizi wa Polisi David Mafimbo.
Chenge anadaiwa kufanya makosa hayo Machi 27 mwaka huu majira ya 10:30 alfajiri katika barabara ya Haile Selasie, karume eneo la Osterbay, Kinondoni.
Mafimbo: Katika shitaka la kwanza Chenge unashitakiwa kwa kusababisha kifo kupitia uendeshaji wa kizembe katika barabara ya umma, na maelezo ya kosa ni kwamba ukiwaunaendesha gari yenye Namba T. 513 ACE Toyota Hilux Double Cabin uliendesha gari hiyo kizembe na kushindwa kuchukuwa tahadhari kama inavyotakiwa huku ukiendesha upande wa kulia zaidi uliigonga Bajaji yenye namba T 736 AXC, kweli au si kweli?.
Chenge: Si kweli.
Mafimbo: Katika shitaka la pili, Chenge unashitakiwa kwa kusababisha vifo vya watu wawili, na maelezo ya kosa ni kwamba mnamo Machi 27 mwaka huu majira ya 10:30 alfajiri katika barabara ya Haile Selasie, karume Osterbay wilaya ya Kinondoni ukiendesha gari bila kuchukuwa taadhari uliigonga Bajaji na kusababisha vifo vya watu wawili Victoria Gorge na Beatrice Constantini, kweli au si kweli?
Chenge: Si kweli.
Mafimbo : Shitaka la Tatu ni kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha uharibifu wa bajaji, jibu kweli au si kweli?
Chenge: Si kweli.
Baada ya Chenge kukana mashtaka yake yote ASP Mafimbo alimweleza Hakimu Mchauru kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Hakimu Mchauru aliweka wazi masharti ya dhamana ambapo alimweleza mshtakiwa kuwa anatakiwa kusaini hati ya dhamana ya milioni 1/- NA kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini hati ya dhamana ya milioni 1/-.
Chenge alikamilisha masharti hayo ya dhamana aliyotakiwa kuyatekeleza na kesi imeahirishwa hadi 30 April mwaka huu.
Kesi iifanyika chumba kidogo cha mahamama alichukuwa takribani dakika 10 hadi 15 tangu Chenge alipowasili mahakamani hapo, ambapo alifika na kupitiliza moja kwa moja kwenye chemba na hakimu kuanza kuendesha kesi huku waandishi wa habari wakisikiliza kesi wakiwa nje ya chumba kutokana na chumba hicho kuwa na nafasi ndogo isiyotoshereza watu wengi kuingia.
Nje ya mahakama ndugu wa Chenge walisikika wakiwasema vibaya waandishi wa habari waliokuwa wakifuatilia kesi hiyo na kutaka kuwazuia wasimpige picha Chenge.
Hivi mnazani kwakumpigapicha ndugu yetu mtaondokana na umaskini? Kama mnadhani mtatajirika kutokana na kesi hii ya leo basi tutaona kama mtaondokana na umaskini, alisikika mmoja wa ndugu wa Chenge akiwaambia waandishi wa habari.
Umati wa watu ulifurika katika mahakama hiyo waliofika ili kumshuhudia Kiongozi huyo wa serikali akifikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashitaka yake.
Chenge alifikishwa mahakamani hapo majira ya saa 6 mchana akiwa kwenye gari ya polisi na baada ya kuachiwa kwa dhamana aliondoka na gari binafsi yenye namba T ASP 362.