Chenge ashikiliwa polisi kwa ajali ya gari iliyosababisha vifo

...sasa saa tisa za usiku alikuwa anatoka wapi mzee wa visenti au ndio kwenye vikao vya mafisadi?
Inasikitisha, lakini hata hiyo Bajaj mbona huhoji ilikuwa inatoka wapi? Simtetei Chenge lakini naamini hivi:

"Kila jambo linalomkuta binadamu lina maana yake!"
 

simple question alikuwa anatoka kule ilikotoka BAJAJ, hivi mwenyezi Mungu anaweza kukutumia balaa na kupitia balaa hilo uwaangamize binadamu wenzio???? JAMANI SHANGAZI waonee huruma waliopoteza maisha yao.
 
hakyamama
Anyway mie nipo pamoja na ndugu wa marehemu. Mungu awafariji.
Inasikitisha na kuuma
 
Jamani, wana JF, mi siyo mwanasheria lakini kugonga mtu hadi kumuua si kesi itakayokulaza Keko. Tuache ushabiki. Hii ni road accident, na tuombe Mungu atuepushe na balaa kama hili, maana kugonga bajaji au mtu ni kitu ambacho kina uwezekano mkubwa kutokea ukiwa dereva Dar-es-Salaam. Pamoja na matatizo yote ya Chenge, this is not a time to gloat!

Nawapa pole ndugu wa marehemu na tunaomba kesi hii isikilizwe bila mizengwe ya eti alale Keko, bali sheria ifuate mkondo wake.

Pia naomba niseme hii kesi iko tofauti na ile ya Ditopile!
 
TISA UCKU??? LAZIMA ALITOKA KWA MGANGA HUYO, ushahidi tosha hata bungeni ucku alikuwa yeye akimwaga upupu ...

Haya si maneno ya kusema, hivi unataka sema kuwa huwezi kuwa na dharula 9 usiku?, hata kama mtu anatuhumiwa kwa ufisadi tunatakiwa kumpa haki zake kama binadamu wengine. Pia ajali ni ajali, yaweza kusababishwa na yoyote, labda kama atakuwa alilewa.

Mungu awazidishie nguvu wafiwa.
 
Hivi sheria za Bongo kuhusu maeneo ya ulevi na starehe zinasema mwisho ni saa ngapi yaani kufungwa kwa kumbi za burudani, vilevi na starehe nyingine zinazoruhusiwa kisheria.
 

Azimio Jipya naona nchi yetu haijafikia huko.
 

Alishalewa huyo! na baada ya tungi chakari, kibajaj hakukiona si unajuwa ulevi tena? Jee, polisi walimpeleka kupima pombe ngapi aligida?
 
kichwa cha habari na content tofauti....kaua kwa gari mara risasi
 
Alishalewa huyo! na baada ya tungi chakari, kibajaj hakukiona si unajuwa ulevi tena? Jee, polisi walimpeleka kupima pombe ngapi aligida?
Naona sasa Kova anaongea na waandishi.

Kumbe jamaa alikuwa anaendesha mwenyewe Toyota Hilux double cabin, aliigonga hiyo Bajaj na akaenda kulala kwanza, kaamua kujisalimisha mwenyewe.

Kwa mantiki hii, inawezekana kabisa mkuu Dar es Salaam uko sahihi alikuwa yuko bwii akaona aende baada ya kukaa sawa.
 
Acheni hizo. kama u dereva ajali ni ajali tu.

Mi naomba ahukumiwe kwa haki. Kama kosa ni la mwenye bajaj au lake lihukumiwe kwa haki.

Sometimes wenye bajaj wanaendesha hovyo sana, na kama wewe ni dereva lazima umeshanote hicho hapa Dar
 
road accident sio ajabu na kwa dereva adhabu ni kunyanganywa leseni....

Mkuu PM,

Una uhakika na ulichoandika hapo juu? Kuua watu ni kitu kikubwa mno hata kama ni ajali.

Suala la kuangalia ni ajali imesababishwa na nini. Kama mhusika alilewa, hilo ni kosa kubwa sana.

Kwa mtu kama Chenge na mambo yanayomkabili naona haifai kujiendesha mwenyewe kabisa. Anaweza akaitwa fisadi njiani, pressure ikapanda na baadaye kusababisha ajali.

Pole kwa walioathirika na hiyo ajali.
 
Nawapa pole sana ndugu na jamaa wa marehemu, Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi! Pia nampa Pole Mzee wa Vijisenti kwa kuwa na mwaka mgumu, Inshallah naye Mungu atamsaidia
 
- Hizi habari kama ni za kweli basi ni very disturbing news, my heart goes to familia ya marehemu dereva wa hiyo bajaji,

- Wenzetu US siku hizi wamezi-adjust sheria za barabara kwa hiyo kwao sasa ajali inaangaliwa case by case sio generalization kama hapa kwetu, inasikitisha sana.

William.
 

saa tisa usiku alikua anatoka wapi huyu nae, hana dereva kwani, au alikua amelewa?.
atalijua jiji
 
saa tisa usiku alikua anatoka wapi huyu nae, hana dereva kwani, au alikua amelewa?.
atalijua jiji

Walahi akachinje ng'ombe kwao, kwani ingekuwa milango ya saa tisa mchana kule Manzese au Tabatatabata vile tungeimba lahila hilalaaaaaaaaa x2 yaaaani wee acha tu!
 
saa tisa usiku alikua anatoka wapi huyu nae, hana dereva kwani, au alikua amelewa?.
atalijua jiji
Kwani wengine wanaokua barabarani saa 9 usiku wanaenda/wanatoka wapi?
Siku zote kiu yangu ya haki haitaisha kama AC atafungwa maisha kwa kosa lingine lisilokua 'kukwapua' vya watz
.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…