Hivi akihukumiwa kufungwa ,ule uchunguzi wa ufisadi dhidi yake utakuwepo au ndio itakuwa amesharuka ? Duniani kuna mipango mingi. Isije kuwa ni mishen town.
Naona sasa Kova anaongea na waandishi.
Kumbe jamaa alikuwa anaendesha mwenyewe Toyota Hilux double cabin, aliigonga hiyo Bajaj na akaenda kulala kwanza, kaamua kujisalimisha mwenyewe.
Kwa mantiki hii, inawezekana kabisa mkuu Dar es Salaam uko sahihi alikuwa yuko bwii akaona aende baada ya kukaa sawa.
saa tisa usiku alikua anatoka wapi huyu nae, hana dereva kwani, au alikua amelewa?.
atalijua jiji
- Hizi habari kama ni za kweli basi ni very disturbing news, my heart goes to familia ya marehemu dereva wa hiyo bajaji,
- Wenzetu US siku hizi wamezi-adjust sheria za barabara kwa hiyo kwao sasa ajali inaangaliwa case by case sio generalization kama hapa kwetu, inasikitisha sana.
William.
Kumbe hakuua ,yeye aliigonga bajaj kwa nyuma baada ya .bajaj kusimama kwa gafla kushusha kupakia abiria aliechelewa kuisimamisha ,na kwa ajili ya kutomwacha mteja huyo dereva akaziminya breki bila ya kuangalia kioo cha nyuma kama kuna mtu kakolea.
Kesi imemdandia dereva wa bajaji kwa kosa la uzembe.Habari kamili baadae
Kumbe hakuua ,yeye aliigonga bajaj kwa nyuma baada ya .bajaj kusimama kwa gafla kushusha kupakia abiria aliechelewa kuisimamisha ,na kwa ajili ya kutomwacha mteja huyo dereva akaziminya breki bila ya kuangalia kioo cha nyuma kama kuna mtu kakolea.
Kesi imemdandia dereva wa bajaji kwa kosa la uzembe.Habari kamili baadae
Sasa hapa ndio kesi inatakiwa iwe moto, sababu kwanza ni hit and run, pili ni lazima yeye aprove beyond resonable dought kwamba alikuwa sober. Nadhani hapa ndio mahala muafaka kwa kumfunga maisha huyu jamaa... Hii ingekuwa nchi za west District attorney angkuwa anashangilia, maana kubuild hii kesi ni simple.
Moja ameuwa bila kukusudia lakini akiwa amelewa
Pili, ni hit and run ambayo nadhani ni crime kwa Tanzania.
Combine hizi mbili then unaweza kumpeleka more than 20yrs jela.... Kama muendesha mashitaka kasoma sheria na sio kubabi hii kesi ni easy kushinda.
Kusimama Ghafla sio tatizo, kwani chenge yeye hajui sheria za barabarani? kuna Safe distance amboyo dereva wa gari la nyuma anatakiwa kuwa from the front vehicle, hapa pia kuna swala la speed, kuna uwezekano kabisa alikuwa kwenye speed kubwa. dereva wa Bajaji hakuhitaji kuangalia nyuma kama ulikuwa ni usiku, au mzee wa vijisenti alikuwa amezima headlights????
William walofariki ni abiria wasichana wawili walokuwa wamepanda bajaji hiyo na si dereva