Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Nchi yetu ni nchi masikini, kutokana na hali hiyo ni muhimu kila senti inayopatikana ikatumika vizuri.
Leo hii nchi yetu ina viongozi wakubwa wafuatao
1. Rais
2. Makamu wa Rais
3. Waziri Mkuu
4. Rais wa Zanzibar
5. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
6. Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar
Ukiangalia kwa muundo huu wa serikali zote mbili ya Muungano na ya Zanzibar, hii ni serikali kubwa sana, viongozi hawa wote kila ofisi yake ina bajeti kubwa tu inayopitishwa na bunge/Baraza la wawakilishi kila mwaka. Ili kubana matumizi tunahitaji serikali ndogo lakini yenye ufanisi wa hali ya juu!
Leo hii Waziri Mkuu ana bajeti, lakini ukikaa chini na kuchunguza utaona kimuundo Waziri Mkuu anatumika zaidi Upande wa Tanganyika kuliko Zanzibar (Sijiu ni ziara ngapi za kitendaji Waziri Mkuu amekwenda kufuatilia shughuli za kila siku za serikali huko Zanzibar kama afanyavyo katika mikoa ya huku Tanganyika).
Ukichunguza, utaona kwamba Mamlaka ya Waziri mkuu kwa huko Zanzibar yamekasimiwa kwa Makamu wa pili wa raisi wa Zanzibar (Cheo ambacho zamani kilikuwa ni Waziri kiongozi), Hata kwa mambo ambayo ni ya Muungano utaona kuwa kwa huko Zanzibar yanafanywa na ofisi hii badala ya Waziri Mkuu!. Sasa hapa tunapokuja katika Bajeti, huu ni mzigo mkubwa kwa Walipa kodi wa nchi hii, kuhudumia Ofisi mbili za mambo yaleyale!
Tukija kwenye ofisi ya Makamu wa Raisi, Utaona kwamba majukumu yake ni kumsaidia raisi pindi raisi akiwa hayupo ofisini na pia kuna majukumu machache tu ambayo katiba imempa, angalia ibara hii ya katiba hapa chini kuhusu madarka ya makamu wa raisi.
Katika mazingira haya, Je ni kitu gani kilishindikana Kuunganisha Majukumu haya machache ya ofisi ya makamu wa raisi ili yaingie katika ofisi ya Waziri Mkuu na hivyo kusaidia kupunguza matumizi ya pesa ya Umma kwenye kugharamia ofisi hii?
HOJA YA KULINDA MUUNGANO KWA MUUNDO HUU INA MANTIKI?
Utaratibu wa sasa unasema kuwa kama Rais atatoka upande mmoja wa muungano basi Makamu atoke upande wa pili, lengo hapa ni kuwa na uwakilishi wa pande mbili katika serikali, lakini cha kujiuliza Je haiwezekani tukawa na Utaratibu mwingine mzuri na ulionafuu kiuendeshaji kuliko wa sasa?- NAAMINI INAWEZEKANA, - Tuondoe cheo cha Makamu wa Raisi kupunguza gharama, kisha tuwe na Vyeo viwili tu vikubwa Cha Raisi wa JMT na cheo cha Waziri Mkuu, Lakini Waziri Mkuu huyu apatikane kutoka upande wa pili wa Muungano( Yaani kama raisi atatoka bara, Waziri Mkuu atoke Zanzibar) na athibitishwe na Mabunge yote mawili (Bunge la JMT na Baraza la Wawakilishi), Kama bunge moja kati ya hayo mawili litamkataa basi atafutwe mwingine.
FAIDA ZAKE NINI

- Kutakuwa na Waziri Mkuu mtendaji, Mwenye Mandate ya kufanyia kazi mambo ya muungano kwenye pande zote mbili akiwa anajiamini kwa kuwa kapitishwa na mabunge yote mawili
- Itapunguza gharama za uendeshaji wa serikali
- Tutapunguza gharama za kuhudumia Wastaafu, tufahamu wazi kuwa Kila mstaafu katika wale viongozi wetu wakubwa yaani rais, makamu, waziri mkuu n.k wanaendelea kupata mishahara minono na stahiki nyingi sana, Tukiondoa cheo cha makamu wa rais tutapunguza gharama
- Ukisoma majukumu ya Waziri mkuu na Makamu wa Raisi kwa mujibu wa katiba, kuna sehemu majukumu yao yanafanana, nayo ni "Kupangiwa kazi yoyote na raisi kadri atakavyoona inafaa", Sasa kama hili linawezekana maana yake ni kwamba inawezekana kabisa Waziri mkuu kufanya majukumu ya kawaida ya kila siku ya makamu wa raisi "kama akiagizwa na raisi", sasa kwa nini tuwape kazi ileile watu wawili wakati mmoja anaweza kuifanya?-TUTUMIE VIZURI KODI ZA WANANCHI TUONDOE CHEO CHA MAKAMU WA RAISI
- Pili, Hiki cheo cha kungoja raisi asiweze kutimiza majukumu yake ili mtu ahesabiwe kuwa eti kusubiri kwake huko ni sehemu ya kazi yake halafu kila mwezi tuendelee kumlpia mshahara, mimi nadhani huu ni mzigo mkubwa kwa mlipa kodi
- Hakuna chochote kile kinachofanywa na ofisi ya Makamu wa Raisi ambacho hakiwezi kufanywa na ofisi ya Waziri Mkuu mwenye mandate iliyoshiba ya nchi nzima, Kwa maoni yangu Cheo cha Waziri Mkuu kinatutosha, Cheo cha makamu wa rais kinaongeza mzigo kwa Taifa!