Cheo cha Makamu wa Rais hakina tija, tukiondoe, tubakishe cha Waziri Mkuu

Mkuu hivi hujui kuwa kama hii ofisi kama ikifutwa pesa zake za utawala zitahamia directly kwenye ofisi nyingine itakayokasimu majukumu yake?Mfano:
1.hiyo ofisi mpya italazimika kuongeza wafanyakazi maana majukumu yatakuwa mengi.
2.Ziara za hii ofisi mpya zitaongezeka so lazima budget pia iongezeke.
2.Shajala zitahitajika kwa wingi zaidi.

Yaani utakachookoa hapo ni mishahara wa mtu mmoja tu bas, mengine yataki Kama yalivyo.

1. kuna gharama za logistic za ofisi zitapungua mfano mashangingi, misafara etc
2.kuna gharama za ulinzi zitapungua
3.kuna mshahara, pensheni na perdiem zitapungua
4.kuna watu wanafanya majukumu yaleyale yanayofanana kwa mfano mwandishi wa hotuba za makamu wa raisi watapungua maana hatuwezi kuwa na watu wawili wafanye kazi moja
5.Kuna bajeti ya furniture, marupurupu ya makamu na watu wazito katika hiyo ofisi yatapungua

,
 
Nchi yetu ni nchi masikini, kutokana na hali hiyo ni muhimu kila senti inayopatikana ikatumika vizuri.
Leo hii nchi yetu ina viongozi wakubwa wafuatao
1. Raisi
2.Makamu wa raisi
3.Waziri Mkuu
4.Raisi wa Zanzibar
5.Makamu wa Kwanza wa raisi wa Zanzibar
6.Makamu wa pili wa raisi wa Zanzibar

Ukiangalia kwa muundo huu wa serikali zote mbili ya Muungano na ya Zanzibar, hii ni serikali kubwa sana, viongozi hawa wote kila ofisi yake ina bajeti kubwa tu inayopitishwa na bunge/Baraza la wawakilishi kila mwaka. Ili kubana matumizi tunahitaji serikali ndogo lakini yenye ufanisi wa hali ya juu!

Leo hii Waziri Mkuu ana bajeti, lakini ukikaa chini na kuchunguza utaona kimuundo Waziri Mkuu anatumika zaidi Upande wa Tanganyika kuliko Zanzibar (Sijiu ni ziara ngapi za kitendaji Waziri Mkuu amekwenda kufuatilia shughuli za kila siku za serikali huko Zanzibar kama afanyavyo katika mikoa ya huku Tanganyika).

Ukichunguza, utaona kwamba Mamlaka ya Waziri mkuu kwa huko Zanzibar yamekasimiwa kwa Makamu wa pili wa raisi wa Zanzibar (Cheo ambacho zamani kilikuwa ni Waziri kiongozi), Hata kwa mambo ambayo ni ya Muungano utaona kuwa kwa huko Zanzibar yanafanywa na ofisi hii badala ya Waziri Mkuu!. Sasa hapa tunapokuja katika Bajeti, huu ni mzigo mkubwa kwa Walipa kodi wa nchi hii, kuhudumia Ofisi mbili za mambo yaleyale!

Tukija kwenye ofisi ya Makamu wa Raisi, Utaona kwamba majukumu yake ni kumsaidia raisi pindi raisi akiwa hayupo ofisini na pia kuna majukumu machache tu ambayo katiba imempa, angalia ibara hii ya katiba hapa chini kuhusu madarka ya makamu wa raisi.

View attachment 975882

Katika mazingira haya, Je ni kitu gani kilishindikana Kuunganisha Majukumu haya machache ya ofisi ya makamu wa raisi ili yaingie katika ofisi ya Waziri Mkuu na hivyo kusaidia kupunguza matumizi ya pesa ya Umma kwenye kugharamia ofisi hii?

HOJA YA KULINDA MUUNGANO KWA MUUNDO HUU INA MANTIKI?

Utaratibu wa sasa unasema kuwa kama Rais atatoka upande mmoja wa muungano basi Makamu atoke upande wa pili, lengo hapa ni kuwa na uwakilishi wa pande mbili katika serikali, lakini cha kujiuliza Je haiwezekani tukawa na Utaratibu mwingine mzuri na ulionafuu kiuendeshaji kuliko wa sasa?- NAAMINI INAWEZEKANA, - Tuondoe cheo cha Makamu wa Raisi kupunguza gharama, kisha tuwe na Vyeo viwili tu vikubwa Cha Raisi wa JMT na cheo cha Waziri Mkuu, Lakini Waziri Mkuu huyu apatikane kutoka upande wa pili wa Muungano( Yaani kama raisi atatoka bara, Waziri Mkuu atoke Zanzibar) na athibitishwe na Mabunge yote mawili (Bunge la JMT na Baraza la Wawakilishi), Kama bunge moja kati ya hayo mawili litamkataa basi atafutwe mwingine.

FAIDA ZAKE NINI
  • Kutakuwa na Waziri Mkuu mtendaji, Mwenye Mandate ya kufanyia kazi mambo ya muungano kwenye pande zote mbili akiwa anajiamini kwa kuwa kapitishwa na mabunge yote mawili
  • Itapunguza gharama za uendeshaji wa serikali
  • Tutapunguza gharama za kuhudumia Wastaafu, tufahamu wazi kuwa Kila mstaafu katika wale viongozi wetu wakubwa yaani rais, makamu, waziri mkuu n.k wanaendelea kupata mishahara minono na stahiki nyingi sana, Tukiondoa cheo cha makamu wa rais tutapunguza gharama
HITIMISHO
  • Ukisoma majukumu ya Waziri mkuu na Makamu wa Raisi kwa mujibu wa katiba, kuna sehemu majukumu yao yanafanana, nayo ni "Kupangiwa kazi yoyote na raisi kadri atakavyoona inafaa", Sasa kama hili linawezekana maana yake ni kwamba inawezekana kabisa Waziri mkuu kufanya majukumu ya kawaida ya kila siku ya makamu wa raisi "kama akiagizwa na raisi", sasa kwa nini tuwape kazi ileile watu wawili wakati mmoja anaweza kuifanya?-TUTUMIE VIZURI KODI ZA WANANCHI TUONDOE CHEO CHA MAKAMU WA RAISI
  • Pili, Hiki cheo cha kungoja raisi asiweze kutimiza majukumu yake ili mtu ahesabiwe kuwa eti kusubiri kwake huko ni sehemu ya kazi yake halafu kila mwezi tuendelee kumlpia mshahara, mimi nadhani huu ni mzigo mkubwa kwa mlipa kodi
  • Hakuna chochote kile kinachofanywa na ofisi ya Makamu wa Raisi ambacho hakiwezi kufanywa na ofisi ya Waziri Mkuu mwenye mandate iliyoshiba ya nchi nzima, Kwa maoni yangu Cheo cha Waziri Mkuu kinatutosha, Cheo cha makamu wa rais kinaongeza mzigo kwa Taifa!
Sahihi mkuu hakina tija Kwa taifa na sioni km anawajibika ipasavyo Kwa taifa hili bora abakie waziri mkuu
 
Mkuu hivi hujui kuwa kama hii ofisi kama ikifutwa pesa zake za utawala zitahamia directly kwenye ofisi nyingine itakayokasimu majukumu yake?Mfano:
1.hiyo ofisi mpya italazimika kuongeza wafanyakazi maana majukumu yatakuwa mengi.
2.Ziara za hii ofisi mpya zitaongezeka so lazima budget pia iongezeke.
2.Shajala zitahitajika kwa wingi zaidi.

Yaani utakachookoa hapo ni mishahara wa mtu mmoja tu bas, mengine yataki Kama yalivyo.
Mleta mada kashauri majukumu ya ofisi ya makamu wa rais yatafanywa na ofisi ya waziri mkuu.
 
Kwenye suala la waziri mkuu hoja yako ni dhaifu na haina mashiko. Waziri mkuu ni mtu mdogo kwa Rais wa Zanzibar which means hawezi kuextend utendaji wake Both Tanganyika and Zanzibar
 
Nchi yetu ni nchi masikini, kutokana na hali hiyo ni muhimu kila senti inayopatikana ikatumika vizuri.
Leo hii nchi yetu ina viongozi wakubwa wafuatao
1. Raisi
2.Makamu wa raisi
3.Waziri Mkuu
4.Raisi wa Zanzibar
5.Makamu wa Kwanza wa raisi wa Zanzibar
6.Makamu wa pili wa raisi wa Zanzibar

Ukiangalia kwa muundo huu wa serikali zote mbili ya Muungano na ya Zanzibar, hii ni serikali kubwa sana, viongozi hawa wote kila ofisi yake ina bajeti kubwa tu inayopitishwa na bunge/Baraza la wawakilishi kila mwaka. Ili kubana matumizi tunahitaji serikali ndogo lakini yenye ufanisi wa hali ya juu!

Leo hii Waziri Mkuu ana bajeti, lakini ukikaa chini na kuchunguza utaona kimuundo Waziri Mkuu anatumika zaidi Upande wa Tanganyika kuliko Zanzibar (Sijiu ni ziara ngapi za kitendaji Waziri Mkuu amekwenda kufuatilia shughuli za kila siku za serikali huko Zanzibar kama afanyavyo katika mikoa ya huku Tanganyika).

Ukichunguza, utaona kwamba Mamlaka ya Waziri mkuu kwa huko Zanzibar yamekasimiwa kwa Makamu wa pili wa raisi wa Zanzibar (Cheo ambacho zamani kilikuwa ni Waziri kiongozi), Hata kwa mambo ambayo ni ya Muungano utaona kuwa kwa huko Zanzibar yanafanywa na ofisi hii badala ya Waziri Mkuu!. Sasa hapa tunapokuja katika Bajeti, huu ni mzigo mkubwa kwa Walipa kodi wa nchi hii, kuhudumia Ofisi mbili za mambo yaleyale!

Tukija kwenye ofisi ya Makamu wa Raisi, Utaona kwamba majukumu yake ni kumsaidia raisi pindi raisi akiwa hayupo ofisini na pia kuna majukumu machache tu ambayo katiba imempa, angalia ibara hii ya katiba hapa chini kuhusu madarka ya makamu wa raisi.

View attachment 975882

Katika mazingira haya, Je ni kitu gani kilishindikana Kuunganisha Majukumu haya machache ya ofisi ya makamu wa raisi ili yaingie katika ofisi ya Waziri Mkuu na hivyo kusaidia kupunguza matumizi ya pesa ya Umma kwenye kugharamia ofisi hii?

HOJA YA KULINDA MUUNGANO KWA MUUNDO HUU INA MANTIKI?

Utaratibu wa sasa unasema kuwa kama Rais atatoka upande mmoja wa muungano basi Makamu atoke upande wa pili, lengo hapa ni kuwa na uwakilishi wa pande mbili katika serikali, lakini cha kujiuliza Je haiwezekani tukawa na Utaratibu mwingine mzuri na ulionafuu kiuendeshaji kuliko wa sasa?- NAAMINI INAWEZEKANA, - Tuondoe cheo cha Makamu wa Raisi kupunguza gharama, kisha tuwe na Vyeo viwili tu vikubwa Cha Raisi wa JMT na cheo cha Waziri Mkuu, Lakini Waziri Mkuu huyu apatikane kutoka upande wa pili wa Muungano( Yaani kama raisi atatoka bara, Waziri Mkuu atoke Zanzibar) na athibitishwe na Mabunge yote mawili (Bunge la JMT na Baraza la Wawakilishi), Kama bunge moja kati ya hayo mawili litamkataa basi atafutwe mwingine.

FAIDA ZAKE NINI
  • Kutakuwa na Waziri Mkuu mtendaji, Mwenye Mandate ya kufanyia kazi mambo ya muungano kwenye pande zote mbili akiwa anajiamini kwa kuwa kapitishwa na mabunge yote mawili
  • Itapunguza gharama za uendeshaji wa serikali
  • Tutapunguza gharama za kuhudumia Wastaafu, tufahamu wazi kuwa Kila mstaafu katika wale viongozi wetu wakubwa yaani rais, makamu, waziri mkuu n.k wanaendelea kupata mishahara minono na stahiki nyingi sana, Tukiondoa cheo cha makamu wa rais tutapunguza gharama
HITIMISHO
  • Ukisoma majukumu ya Waziri mkuu na Makamu wa Raisi kwa mujibu wa katiba, kuna sehemu majukumu yao yanafanana, nayo ni "Kupangiwa kazi yoyote na raisi kadri atakavyoona inafaa", Sasa kama hili linawezekana maana yake ni kwamba inawezekana kabisa Waziri mkuu kufanya majukumu ya kawaida ya kila siku ya makamu wa raisi "kama akiagizwa na raisi", sasa kwa nini tuwape kazi ileile watu wawili wakati mmoja anaweza kuifanya?-TUTUMIE VIZURI KODI ZA WANANCHI TUONDOE CHEO CHA MAKAMU WA RAISI
  • Pili, Hiki cheo cha kungoja raisi asiweze kutimiza majukumu yake ili mtu ahesabiwe kuwa eti kusubiri kwake huko ni sehemu ya kazi yake halafu kila mwezi tuendelee kumlpia mshahara, mimi nadhani huu ni mzigo mkubwa kwa mlipa kodi
  • Hakuna chochote kile kinachofanywa na ofisi ya Makamu wa Raisi ambacho hakiwezi kufanywa na ofisi ya Waziri Mkuu mwenye mandate iliyoshiba ya nchi nzima, Kwa maoni yangu Cheo cha Waziri Mkuu kinatutosha, Cheo cha makamu wa rais kinaongeza mzigo kwa Taifa!
You are right lakini vilevile kwa kuwa Rais ni executive, Makamu naye awe executive achukue madalaka yote ya Waziri Mkuu ili tusiwe na Waziri Mkuu kabisa huku succession ya nafasi ya urais ikibaki kama sasa.
 
Yule mama anatusaidia kweli kutuwakilisha huko nje. Sasa hivi kungekuwa na references kibao za font page, hiyo hiyo huko duniani.
Mama sio tatizo, tatizo huo wadhifa. Kwa kweli mie sioni umuhimu wake. Waziri mkuu anatosha. Hata wakuu wa wilaya sioni kazi yao, mkuu wa wilaya asiwepo, wakurugenzi wanatosha wataripoti kwa mkuu wa mkoa. Mbunge awakilishe wilaya yaani wilaya ndio iwe jimbo.
 
Halafu mtu mwenyewe Mzanzibar.

Mambo ya Tanganyika yanamhusu nini?
Mkuu hata mimi huwa nashangaa Watanganyika mambo ya Zanzibar yanawahusu nini ?
Kuna mashoga eti oo Zanzibar isijiunge na OIC na lazima tuungane nao..
mtaolewa
 
Tatizo wapo wanasiasa ambao hawataki kabisa uguse katiba ya 1964 na badae kuwa revised 1977 maana inawapa mandate ya utawala wa ku maintain status quo..Wananchi wengi walitoa maoni yao kuhusu muundo wa muungano na utawala wa Zanzibar na Tanganyika lakini hayo mapendekezo ya katiba ya Marehemu Adrian Mvungi na Warioba yatavuruga mfumo wa utawala wa ku maintain status quo wanaona bora tukae na katiba hii ya muundo wa chama kimoja.
 
Mleta mada kashauri majukumu ya ofisi ya makamu wa rais yatafanywa na ofisi ya waziri mkuu.
Sahihi.
Nami nikaongezea kuwa kitendo hicho kitaongeza majukumu na matumizi ya OWM kama niliyoainisha
 
Kwa maana hiyo ndiyo maana baba hataki kusafiri...

Anaweza kuta mambo yamepangwa vile asivyataka yeye...

Cc: mahondaw
 
Bajeti ya kuendeshea ofisi ya Makamu wa raisi ikiwekwa kwenye kujenga hata vyuo vya VETA kuna faida zaidi kwa Taifa kuliko ilivyo hivi sasa.
Hii kazi ya kusubiri raisi aumwe/asafiri ili ukaimu haina tija!
 
Nchi yetu ni nchi masikini, kutokana na hali hiyo ni muhimu kila senti inayopatikana ikatumika vizuri.
Leo hii nchi yetu ina viongozi wakubwa wafuatao
1. Raisi
2.Makamu wa raisi
3.Waziri Mkuu
4.Raisi wa Zanzibar
5.Makamu wa Kwanza wa raisi wa Zanzibar
6.Makamu wa pili wa raisi wa Zanzibar

Ukiangalia kwa muundo huu wa serikali zote mbili ya Muungano na ya Zanzibar, hii ni serikali kubwa sana, viongozi hawa wote kila ofisi yake ina bajeti kubwa tu inayopitishwa na bunge/Baraza la wawakilishi kila mwaka. Ili kubana matumizi tunahitaji serikali ndogo lakini yenye ufanisi wa hali ya juu!

Leo hii Waziri Mkuu ana bajeti, lakini ukikaa chini na kuchunguza utaona kimuundo Waziri Mkuu anatumika zaidi Upande wa Tanganyika kuliko Zanzibar (Sijiu ni ziara ngapi za kitendaji Waziri Mkuu amekwenda kufuatilia shughuli za kila siku za serikali huko Zanzibar kama afanyavyo katika mikoa ya huku Tanganyika).

Ukichunguza, utaona kwamba Mamlaka ya Waziri mkuu kwa huko Zanzibar yamekasimiwa kwa Makamu wa pili wa raisi wa Zanzibar (Cheo ambacho zamani kilikuwa ni Waziri kiongozi), Hata kwa mambo ambayo ni ya Muungano utaona kuwa kwa huko Zanzibar yanafanywa na ofisi hii badala ya Waziri Mkuu!. Sasa hapa tunapokuja katika Bajeti, huu ni mzigo mkubwa kwa Walipa kodi wa nchi hii, kuhudumia Ofisi mbili za mambo yaleyale!

Tukija kwenye ofisi ya Makamu wa Raisi, Utaona kwamba majukumu yake ni kumsaidia raisi pindi raisi akiwa hayupo ofisini na pia kuna majukumu machache tu ambayo katiba imempa, angalia ibara hii ya katiba hapa chini kuhusu madarka ya makamu wa raisi.

View attachment 975882

Katika mazingira haya, Je ni kitu gani kilishindikana Kuunganisha Majukumu haya machache ya ofisi ya makamu wa raisi ili yaingie katika ofisi ya Waziri Mkuu na hivyo kusaidia kupunguza matumizi ya pesa ya Umma kwenye kugharamia ofisi hii?

HOJA YA KULINDA MUUNGANO KWA MUUNDO HUU INA MANTIKI?

Utaratibu wa sasa unasema kuwa kama Rais atatoka upande mmoja wa muungano basi Makamu atoke upande wa pili, lengo hapa ni kuwa na uwakilishi wa pande mbili katika serikali, lakini cha kujiuliza Je haiwezekani tukawa na Utaratibu mwingine mzuri na ulionafuu kiuendeshaji kuliko wa sasa?- NAAMINI INAWEZEKANA, - Tuondoe cheo cha Makamu wa Raisi kupunguza gharama, kisha tuwe na Vyeo viwili tu vikubwa Cha Raisi wa JMT na cheo cha Waziri Mkuu, Lakini Waziri Mkuu huyu apatikane kutoka upande wa pili wa Muungano( Yaani kama raisi atatoka bara, Waziri Mkuu atoke Zanzibar) na athibitishwe na Mabunge yote mawili (Bunge la JMT na Baraza la Wawakilishi), Kama bunge moja kati ya hayo mawili litamkataa basi atafutwe mwingine.

FAIDA ZAKE NINI
  • Kutakuwa na Waziri Mkuu mtendaji, Mwenye Mandate ya kufanyia kazi mambo ya muungano kwenye pande zote mbili akiwa anajiamini kwa kuwa kapitishwa na mabunge yote mawili
  • Itapunguza gharama za uendeshaji wa serikali
  • Tutapunguza gharama za kuhudumia Wastaafu, tufahamu wazi kuwa Kila mstaafu katika wale viongozi wetu wakubwa yaani rais, makamu, waziri mkuu n.k wanaendelea kupata mishahara minono na stahiki nyingi sana, Tukiondoa cheo cha makamu wa rais tutapunguza gharama
HITIMISHO
  • Ukisoma majukumu ya Waziri mkuu na Makamu wa Raisi kwa mujibu wa katiba, kuna sehemu majukumu yao yanafanana, nayo ni "Kupangiwa kazi yoyote na raisi kadri atakavyoona inafaa", Sasa kama hili linawezekana maana yake ni kwamba inawezekana kabisa Waziri mkuu kufanya majukumu ya kawaida ya kila siku ya makamu wa raisi "kama akiagizwa na raisi", sasa kwa nini tuwape kazi ileile watu wawili wakati mmoja anaweza kuifanya?-TUTUMIE VIZURI KODI ZA WANANCHI TUONDOE CHEO CHA MAKAMU WA RAISI
  • Pili, Hiki cheo cha kungoja raisi asiweze kutimiza majukumu yake ili mtu ahesabiwe kuwa eti kusubiri kwake huko ni sehemu ya kazi yake halafu kila mwezi tuendelee kumlpia mshahara, mimi nadhani huu ni mzigo mkubwa kwa mlipa kodi
  • Hakuna chochote kile kinachofanywa na ofisi ya Makamu wa Raisi ambacho hakiwezi kufanywa na ofisi ya Waziri Mkuu mwenye mandate iliyoshiba ya nchi nzima, Kwa maoni yangu Cheo cha Waziri Mkuu kinatutosha, Cheo cha makamu wa rais kinaongeza mzigo kwa Taifa!
Ni kweli ni gharama kubwa kuwe na Rais kisha Rais wa Zanzibar awe makamu wa Rais na Waziri mkuu anayepenya mpaka Zanzibar kwani Zanzibar kenyewe ni kadogo kuliko hata wilaya ya Bagamoyo iweje kawe na utitiri wa Viongozi wakati Tanganyika ndiyo hutaabika kuwahudumia
 
Unajua kuwa katiba mpya inataka serikali nyingine ya tatu. Yaani raisi, makamu raisi, na wabunge nadhani wa Tanganyika.

Yaani kila mwanasiasa apate fursa. [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Biko Kila Mtu Apate 😀😁😃😂
 
Ni wazo la kuliangalia. Kwa maoni hayo Katiba ya sasa lazima ibadilishwe na muundo wa Muungano uwe mwengine kabisa, nao ni wa Serikali tatu kwani moja haikubaliki kwa Wazanzibari. Kwa muundo wa sasa Waziri Mkuu ana majukumu ya Kimuungano tu kwa Zanzibar na ndio maana haendi sana kule. Sio kweli kwamba Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar anafanya kazi za Waziri Mkuu wa JMT. Hili tulitafakari na kulifikiria kwa makini.

Kipindi cha Nyerere ujue Rais wa Zanzibar ndiyo alikuwa makamu wa Rais, wachenjii juu kwa juu mbona katiba yenyewe magufuli huwa haifuati? Katiba inaruhusu mikutano ya siasa kwa Wapinzani lakini yeye kapiga marufuku, mahakama hazipo huru inaingiliwa ni mara mia afanye kupunguza viongozi ili ile kauli yake ya kubana matumizi ilete maana
 
Moja ya mambo ya hovyo aliyotuachia Mwl Nyerere.
Muungano ufe kila mmoja akae kwake kwani pesa inayotumika kuubembeleza kuulea muungano, kuwalipa mishahara utitiri wa watumishi Zanzibar ikibakia Tanganyika ujue kuwa Tanganyika itakuwa Nchi tajiri kuliko Nchi zote barani Africa kwani pesa inayotumika huko Zanzibar ni kubwa mno kupita wanachozakisha wao kama visiwa, Hazina ya Tanganyika inamenyeka kuwalisha Zanzibar ambao huwa hawana shukrani na mda wote hulalamika na wanataka muungano Ufutike ili waolewe na kufunga ndoa na Oman wakidhani Zanzibar itakuwa kama Dubai wana ndoto nyingi za asubuhi saa 12 .
 
Mkuu hata mimi huwa nashangaa Watanganyika mambo ya Zanzibar yanawahusu nini ?
Kuna mashoga eti oo Zanzibar isijiunge na OIC na lazima tuungane nao..
mtaolewa

Zanzibar iachwe maana mda mwingi hudai talaka ndoa yao na Tanganyika ni ndio ya mkeka wameichoka
 
Muungano ufe kila mmoja akae kwake kwani pesa inayotumika kuubembeleza kuulea muungano, kuwalipa mishahara utitiri wa watumishi Zanzibar ikibakia Tanganyika ujue kuwa Tanganyika itakuwa Nchi tajiri kuliko Nchi zote barani Africa kwani pesa inayotumika huko Zanzibar ni kubwa mno kupita wanachozakisha wao kama visiwa, Hazina ya Tanganyika inamenyeka kuwalisha Zanzibar ambao huwa hawana shukrani na mda wote hulalamika na wanataka muungano Ufutike ili waolewe na kufunga ndoa na Oman wakidhani Zanzibar itakuwa kama Dubai wana ndoto nyingi za asubuhi saa 12 .

Tatizo ukivunja Muungano, Je unaujua mpaka wa Tanganyika na Zanzibar ulipo?

Baada ya Muungano kufa ama ni vita ya kugombea mpaka wa maji baharini baina ya Tanganyika na Zanzibar au ni kwa Tanganyika kupata kaeneo kadogo ka bahari katika uelekeo wa bahari ya zanzibar na Pemba!. Yaani ili kuipata Bahari kuu kutokea Tanga na Dar lazima ushuke hadi mtwara huko ndo uitafute, La sivyo utalazimika kupita ama katika maji ya Kenya au katika maji ya nchi ya Zanzibar
 
Back
Top Bottom