Hiki cheo cha vice president kifutwe tu hakina kazi. Tangu aingizwe madarakani hakuna lolote lile tumesikia kutoka kwake zaidi ya kwenda airport kumsubiri mama ampokee. Anakula kodi zetu bure tu. Aina hii ya viongozi ni mzigo na hasara kwa taifa, sijui kwanini wasomi wa bongo akili zao hazileti matokeo chanya kwa taifa.
Huyu ni mwanauchumi wa makaratasi tu lakini utendaji ni zero kabisa, yupoyupo kuinama na kukunja mikono kumsalimia aliyemteua. Hii Safu kwanzia Rais, Makamu wake na waziri mkuu hapa tumepigwa hawafai hata kuwa monitor wa darasa la tatu. Ni unproductive wapo kuzunguka tu kila siku wanawaza kukutana na mzungu hali za wananchi zinazidi kuwa ngumu. Wananchi tusipobadilika kukataa viongozi wachumia tumbo tutaburuzwa maisha yetu yote.