Cheti cha advanced education kipewe heshima inayostahili

Cheti cha advanced education kipewe heshima inayostahili

Mr Pixel3a

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2021
Posts
5,710
Reaction score
8,579
Imekaaje hiki cheti cha Diploma ni Dhahabu wakati cheti cha Advanced level ni Mkaa .Serikali ianze kuleta ubunifu kutoa kipaumbele cha Ajira kwa wenye Advanced Certificate.
 
Imekaaje hiki cheti cha Diploma ni Dhahabu wakati cheti cha Advanced level ni Mkaa .Serikali ianze kuleta ubunifu kutoa kipaumbele cha Ajira kwa wenye Advanced Certificate.

Kwanza tujue katika Upande wa ajira zipo za aina mbili: zinazohitaji ujuzi au maarifa fulan & na zisizo hitaji ujuzi mtu yoyote mweny aliki na utashi anaweza kupewa fursa ya ajira.
Kwa upande wa Advance certificate inatumika kama added advantage ambayo inaweza kisiangaliwe sana kwa baadh ya Sekta.
Kwa mtazamo wangu advanced certificate inakuongezea CV tu na sio kigezo sahh cha wewe kupata ajira
 
Hebu tuanzie hapa
Mimi nina karakana yangu,inahitaji Welders,Machinist na Technical Draughters
Na nitahitaji Administrator,awe anahusika na accounting, marketing na office adminstration kama Tax,Salaries na expenditures za kiofisi
Wewe na cheti chako cha advance utafiti wapi
 
Mtu wa ECA atakufaa kabisa.
 
Fani inamata zaidi kuliko Advanced level maana yule wa Diploma atakuwa na uwezo, ubobevu wa kuelewa kozi nyingi za fani yake practically akiwa field kuliko yule wa Advanced level ambapo wengi huwa wako theoretically sababu ya shule zetu nyingi huwa hazina physical training materials.

TZ is developing country (third world) but not developed (first world), hivyo basi changamoto kuu ni uchumi uliodorora.

Msomi mwenye cheti cha elimu ya Diploma anastahili zaidi kuajiriwa kuliko mwenye elimu ya Advanced level.
Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Tofautisheni kati ya level of education(General education) na profession.

O level na advance ni general education haikuandai na lolote zaidi ya nadharia nyingi na mbalimbali ambazo baadhi hazikusaidii kwenye maisha yako Wala kazini kwa hiyo elimu mwisho kidato Cha sita.

Ila ukija kwenye professional (Fani)
Nini Stashahada, ukiwa na Astashahada inatosha kabisa kukuwezesha kupata kazi na kuwa mtaalamu kwenye angle Fulani.

Siku hizi naona wanaandika
Level of education O-level/ A- level
Professional:
Basic Certificate
Certificate
Diploma
Higher Diploma
Advance Diploma/ Degree
Post graduate Diploma
Master's level(Second Degree)
Phd

Hivyo tofautisheni kati ya hivi vitu viwili, ndio maana Wazazi wanawalazimisha watoto wao wakimaliza kidato Cha nne na ufaulu uwe mkubwa au mdogo wajiunge na Vyuo vya elimu ya kati, Elimu ya juu na Vyuo vikuu kuokoa muda.

Au Serikari iweke sheria kwamba Uruhusiwi kujiunga na Chuo ama kiwe Cha kati, taasisi za elimu ya juu na Vyuo Vikuu mpaka pale utakapo kuwa umeimaliza kidato Cha Sita na watoe namba maalumu itakavyo kuwezesha kujiunga elimu tajwa hapo iwe Certificate, Diploma au Degree.
 
Sasa imagine wimbi la wanafunzi waende vyuo vya Kati hapatatosha ,na sasaivi kila mzazi from olevel to Diploma..
 
Yaan wewe hitaji kuajiri afisa hesabu, utamuajiri kijana aliyesoma ECA au utamuajiri kijana aliyesoma diploma ya accountancy?
 
Yaan wewe hitaji kuajiri afisa hesabu, utamuajiri kijana aliyesoma ECA au utamuajiri kijana aliyesoma diploma ya accountancy?
Hapo sawasawa na Ukitaka kuajiri Daktari uchukue kijana aliyemaliza PCB kidato Cha Sita huku ukitarajia awe competent kama aliyemaliza Diploma.

Uchukue PCM badala ya mwenye Diploma ya Engineering.

Naona wanajitekenya na kucheka wenyewe
 
Back
Top Bottom