Finder boy
JF-Expert Member
- Jan 20, 2012
- 608
- 150
Kwa majina naitwa STEVEN PETER SAMSON, yaani STEVEN jina langu, PETER jina la baba, na SAMSON jina la babu. Shuleni naitwa STEVEN SAMSON PETER, yaani STEVEN(first name) SAMSON(S.) (initial/middle name) PETER(surname). Kwenye cheti changu cha kuzaliwa majina yangu yanasomeka hivi; Name if any:STEVENE, Name and surname of father😛ETER SAMSON. Kama unavyoweza kuona, kwenye cheti jina limeandikwa STEVENE, shuleni limeandikwa STEVEN, vilevile ktk cheti PETER limekuwa kati na SAMSON mwisho, shuleni SAMSON lipo kati ambapo linasimama kama initial na PETER lipo mwisho ambapo linasimama kama surname. Swali, je hii haitanisumbua ktk kuomba chuo (mkopo) kwa kudhani ni watu wawili tofauti?, je nifanye nini ili kutatua tatizo hili? Naombeni msaada wenu. ASANTENI!