Cheti cha kuzaliwa na uombaji chuo kikuu

Finder boy

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Posts
608
Reaction score
150
Kwa majina naitwa STEVEN PETER SAMSON, yaani STEVEN jina langu, PETER jina la baba, na SAMSON jina la babu. Shuleni naitwa STEVEN SAMSON PETER, yaani STEVEN(first name) SAMSON(S.) (initial/middle name) PETER(surname). Kwenye cheti changu cha kuzaliwa majina yangu yanasomeka hivi; Name if any:STEVENE, Name and surname of father😛ETER SAMSON. Kama unavyoweza kuona, kwenye cheti jina limeandikwa STEVENE, shuleni limeandikwa STEVEN, vilevile ktk cheti PETER limekuwa kati na SAMSON mwisho, shuleni SAMSON lipo kati ambapo linasimama kama initial na PETER lipo mwisho ambapo linasimama kama surname. Swali, je hii haitanisumbua ktk kuomba chuo (mkopo) kwa kudhani ni watu wawili tofauti?, je nifanye nini ili kutatua tatizo hili? Naombeni msaada wenu. ASANTENI!
 
Nenda RITA wakarekebishe makosa hayo katika cheti cha kuzaliwa.Nenda mahakamani ukaape kwa jina halisi. Hicho cheti cha shule ni ngumu kubadilisha, sana sana uwe unaambatanisha kiapo cha mahakamani popote unaposubmit vyeti vinavyotofautiana majina. TCU inakuwapo tatizo iwapo vyeti viwili vya shule (kama cha Form Four na Form Six) vimepishana hata herufi moja, ila kama vipo okay, hakuna taabu. Bodi ya mikopo sijui sana.
 
Omba mkopo, wakitia shaka, unaenda kula kiapo mahakamani, unaweka na barua za watendaji, kesi imeisha
Kwa majina naitwa STEVEN PETER SAMSON, yaani STEVEN jina langu, PETER jina la baba, na SAMSON jina la babu. Shuleni naitwa STEVEN SAMSON PETER, yaani STEVEN(first name) SAMSON(S.) (initial/middle name) PETER(surname). Kwenye cheti changu cha kuzaliwa majina yangu yanasomeka hivi; Name if any:STEVENE, Name and surname of father😛ETER SAMSON. Kama unavyoweza kuona, kwenye cheti jina limeandikwa STEVENE, shuleni limeandikwa STEVEN, vilevile ktk cheti PETER limekuwa kati na SAMSON mwisho, shuleni SAMSON lipo kati ambapo linasimama kama initial na PETER lipo mwisho ambapo linasimama kama surname. Swali, je hii haitanisumbua ktk kuomba chuo (mkopo) kwa kudhani ni watu wawili tofauti?, je nifanye nini ili kutatua tatizo hili? Naombeni msaada wenu. ASANTENI!
 
nenda rita kabadilishe jina la cheti cha kuzaliwa lifanane na kwenye vyeti vya taaluma
 
Nenda RITA wakarekebishe makosa hayo katika cheti cha kuzaliwa.Nenda mahakamani ukaape kwa jina halisi. Hicho cheti cha shule ni ngumu kubadilisha, sana sana uwe unaambatanisha kiapo cha mahakamani popote unaposubmit vyeti vinavyotofautiana majina. TCU inakuwapo tatizo iwapo vyeti viwili vya shule (kama cha Form Four na Form Six) vimepishana hata herufi moja, ila kama vipo okay, hakuna taabu. Bodi ya mikopo sijui sana.

Asante kwa hilo.
 
Back
Top Bottom